Umeme Vijijini: Wananchi Wanakumbushwa Kutuma Tathmini Zao Za Miradi Ya REA

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,246
1,113
Wizara ya Nishati na Madini itafanya tathmini ya MIRADI YA REA siku ya Alhamisi, 07.07.2016. Watakaofanyiwa tathmini ni WAKANDARASI, WAFANYAKAZI WA REA na TANESCO. Tuma maoni yako kupitia: pa_mem@mem.go.tz au Box 2000 DSM. REA AWAMU ya III - tunazo fedha nyingi, zaidi ya Tshs Trilioni 1. kwa hiyo maoni yako ni muhimu sana. Tusilalamike bila kutoa maoni. S Muhongo, WNM

INDUSTRIAL MINERALS: Tunahitaji kuanza kuchimba kwa wingi madini yanayoitajika Viwandani na Teknolojia Mpya - sisi tunayo! Geological Survey itengeneze Ramani na Ripoti za kukaribisha uchimbaji wa madini hayo - mfano: (1) Graphite (2) Lithium (3) REE (4) Soda Ash na (5) Gypsum. Soda Ash inatumika kutengeneza glass, sabuni, karatasi na kusafisha maji. Gypsum inatumika kama mbolea, kutengeneza saruji, wallboard na plasters. Viwanda ni Madini.

S. Muhongo
 
Huu mradi wa REA mimi siuelewi. Kama ni huduma vijijini sioni kwanini baadhi ya vijiji vinarukwa.
Kwa mfano Jimbo la Vunjo kuna kijiji kinaitwa Kiria kata ya Mamba kusini. Ni kweli kipindi cha nyuma kuna watu na taasisi zilijivutia umeme toka njia kuu ya barabara ya Marangu. Huu umeme ulipita barabara kuu ya Mamba zamani ikiitwa Mrema road.
Lengo langu ni kwamba walio pata umeme ni walio karibu na hiyo njia tu!! Wale walioko ndani hawana huduma za umeme, tukiulizia kwanini REA haitufikii tunaambiwa sisi tulikuwa na umeme zamani ambayo siyo sahihi.
Kwa mfano kitongoji za Shokoni chenye zaidi ya kaya 800 hakujawahi kuwa na umeme kitongoji chote.
Huu mradi ulipo anza TANESCO walifanya survey kwenye hiki kitongoji cha Shokoni na alama za nguzo zika wekwa, mbona sasa hatupatiwi umeme?? Halafu tukipita vijiji vya jirani tunaona kuna walio kuwa na nguzo za zamani na huu mradi wa REA upo. Je tuamini kina double standards au?????
Vijana wetu walioko huko mjini wanalipa bill za umeme na kukatwa michango ya REA ila sisi hatuko kwenye mradi.
Meneje wa TANESCO Himo hana la kutueleza. Inauma sana.
 
Mkuu tuma malalamiko yako kwa address walizozitaja hapo juu
 
kiujumla kuna ubabaishaji mwingi. wananchi wanachangishwa hela nyingi kulipia meter lakini hazifiki kwa wakati. pia mpaka leo umeme huo haujawashwa maeneo mengi hasa maguu,litembo na maeneo ya namtumbo kule mkoani RUVUMA.
 
Umeme Vijijini: Wananchi Wanakumbushwa Kutuma Tathmini Zao Za Miradi Ya REA

Sawa tumekupata tatizo ni hiyo email yako, ebu tutumie tena, pia hii miradi ya REA, kwa kweli tunazunguka vijijini sana, wengine hatujaona tofauti kabisa, ila wale ma boss wa REA wanaokaa karibu yetu na wengine tunaotambulishwa mitaani, wamenona kweli, majumba ya kifahari, ma VXi na mashingingi yametanda majumbani kwao, sasa wanaofaidi huu mradi sana sana naona ni wahusika REA na sio vijijini..
 
Back
Top Bottom