Umeme ukikatika dar, raia wanashangilia: C C M C C M SI SI EMU SI SI EMU!

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Habari za asubuhi wadau
Asubuhi ya leo nimepigiwa simu na rafiki akaniambia jambo la kushangaza sana.
Katika baadhi ya maeneo ndani ya jiji la Dar, kila wakati umeme unapokatika utasikia makelele mengi ya washangiliaji.
Wote kwa lugha moja wanasema C C M C C M SI SI EMU SI SI EMU SI SI EMUUUU
Ningependa kusikia wakazi wa jiji hilo wanasemaje? Je kuna ukweli ndani yake au ni ugeni wa rafiki tu aliyefika mjini?
Kama kuna ukweli nadani yake naomba tujadiri au tujifikirishe kuhusu haka katabia; je
kana maana gani?
kana tupeleka wapi?
kameasisiwa na nani?
kana tija kweli?
kana maudhui gani?
kanawakera kera kweli wadau?
n.k n.k!!
 
mkuu wadanganyika miyeyusho tu wanajifanya wanahasira halafu hamuna lolote..
bora waroho wamadaraka wabadilike tu kuliko kusikiliza hawa raia kwani wanaboa mbaya..
 
Kwa hiyo huo ni mkwara tu ambao hauna tija?
Kama ndivyo kuna haja gani ya kuendelea kupiga makelele?
Kwa mantiki hiyo unaniaminisha kuwa watanzania wote ni wanafiki?

mkuu wadanganyika miyeyusho tu wanajifanya wanahasira halafu hamuna lolote..
bora waroho wamadaraka wabadilike tu kuliko kusikiliza hawa raia kwani wanaboa mbaya..
 
CCM ndio wametufikisha kwenye mgao inabidi washangiliwe kila umemeunapokatika
 
kwani wao ccm hawautumii huo umeme? Au ccm ndo wanaokausha mabwawa ya vyanzo vya umeme?,, hao raia wajitokeze panapohusika waeleze jinsi ccm inavyoshiriki kwa kukatika kwa umeme nchi,, maoni yao labda yatamaliza hili tatizo
 
Mbona hata mechi za Yanga huwa wanashangilia CCM! CCM! Hao ni magamba tu hawana jipya. Hasira zao ni pale umeme unapokatika tu, baadae wanasahau.
 
kwani wao ccm hawautumii huo umeme? Au ccm ndo wanaokausha mabwawa ya vyanzo vya umeme?,, hao raia wajitokeze panapohusika waeleze jinsi ccm inavyoshiriki kwa kukatika kwa umeme nchi,, maoni yao labda yatamaliza hili tatizo

Inatubidi tuisifu ccm kwa kuendesha tz kwa miaka 34, bila mgao wa umeme. Kamgao ka mwaka mmoja tu kanatupagawisha!
 
Mkuu Kiti ,zamani umeme ukikatika watu walijiuliza kuna nini leo lakini siku hizi Umeme ukiwaka siku tatu mfululizo watu wanajiuliza kwanini umeme haujakatika yaani imekuwa ajabu umeme kutokatika,.Haya ni matokeo ya Utawala wa kizembe wa CCM HAKUNA WAKUWAJIBIKA,WALA KUMUWAJIBISHA MKOSAJI KWANI WOTE WAKOSAJI TU.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom