Umeme Tanzania: Kikwete ndiyo tatizo? Jisomee 'ngonjera' zake tangu 2005-2011bila utatuzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme Tanzania: Kikwete ndiyo tatizo? Jisomee 'ngonjera' zake tangu 2005-2011bila utatuzi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachanchabuseta, May 13, 2011.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  "Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni, Dodoma, 30 Desemba 2005

  Mheshimiwa Spika:

  Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele katika kuboresha na kuendeleza upatikanaji wa nishati ya uhakika na rahisi vijijini na mijini.

  Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani.

  Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini
  .

  Mheshimiwa Spika:


  Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo ndivyo tutakavyofanya.

  Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa Mto Rusumo na Stigler’s Gorge. Tutaharakisha pia upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.

  Mheshimiwa Spika:


  Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.

  [FONT=&quot]Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye Baraza la Eid-el-Fitr, Arusha, tarehe [/FONT][FONT=&quot]24 Oktoba, 2006[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Bahati mbaya sana kwa upande wa tatizo la umeme hakuna majawabu ya papo kwa papo. Hata kwa umeme wa dharura imetuchukua miezi isiyopungua mitano tangu tuanze mchakato wa kukodi mitambo ya kuzalisha umeme.

  Ni sasa tu ndipo baadhi ya mitambo imewasili na baadhi kuanza kazi. Ni matumaini yetu kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao au hata katikati karibu mitambo yote ya kukodi itakuwa imewasili na kuanza kuzalisha umeme.

  Mitambo hii itakapoanza kuzalisha umeme, tutakuwa tumepata nafuu. Lakini, jawabu hasa litakuwa limepatikana hapo mwakani wakati mitambo mipya ya TANESCO ya Ubungo na Tegeta itakapokuwa imeanza kutoa umeme[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Watanzania, [/FONT]
  [FONT=&quot]tarehe 31 Desemba, 2006

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa aina yake. Upande mmoja ulikuwa mwaka wa mafanikio mengi mazuri na kuipatia Serikali yetu pongezi na sifa nyingi. Upande mwingine ulikuwa mwaka uliokuwa na matatizo machache makubwa ambayo yalileta usumbufu mkubwa na adha kwa watu wengi nchini.

  Baadhi ya matatizo hasa ya ujambazi na umeme yaliwafanya baadhi ya wananchi kupunguza imani yao kwa utendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo vyake. Bahati nzuri, kwa majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunaumaliza mwaka, matatizo ya ukame, njaa na umeme yakiwa hatunayo tena na ujambazi tumeudhibiti.

  Tarehe 31 Januari, 2006, nilipoongea na Watanzania kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam nilieleza kuwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa yetu ulipungua kutoka megawati 561 hadi megawati 167.5 tu.

  Nilitahadharisha kuwa mgao wa umeme hauepukiki. Niliwasihi Wananchi wenzangu kuzidisha kumuomba Mungu atujalie mvua za kutosha ili baa la njaa liishe na tatizo la umeme lisichukue muda mrefu kuisha.

  Kutokana na kujirudia kwa tatizo la mgao wa umeme unaoleta usumbufu mkubwa kwa watu na kuathiri uchumi wa taifa letu changa, nilielezea dhamira ya Serikali ya kuanza kuchukua hatua za dhati za kupunguza kutegemea mno umeme wa maji.

  Nilieleza uamuzi wa Serikali wa kuongeza matumizi ya gesi asilia na makaa ya mawe kuzalisha umeme. Nafurahi kusema kuwa tumekwishachukua hatua muafaka.

  [/FONT]

  Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Nane Wa CCM, Ukumbi wa Kizota, 03 Novemba 2007

  Nishati

  Mwezi mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Nne ianze kazi ya kuwatumikia Watanzania, tulikumbana na tatizo kubwa la aina yake la ukosefu wa umeme.

  Tatizo hilo lilisababishwa na ukame ambao haujawahi kutokea kwa miaka mingi hapa nchini. Maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme yalikauka, hivyo uzalishaji umeme ukapungua sana na kwa baadhi ya vituo kusimama.

  Kwa rehema za Mwenyezi Mungu mvua kubwa zilizonyesha Desemba, 2006, tatizo la umeme limeisha. Ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tulifanya uamuzi wa makusudi wa kuongeza wigo wavyanzo vya kuzalisha umeme badala ya kutegemea mno maji.

  Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa tumeongeza kwa asilimia 60 umeme unaozalishwa kutokana na vyanzo vingine.

  Kutokana na jitihada hizi, sasa hivi tuna ziada ya umeme kwenye gridi ya Taifa. Sio rahisi sasa katika miaka michache ijayo nchi yetu kupata tatizo la upungufu wa umeme kama lile labda kutokee dharura aina nyingine.


  Changamoto iliyobakia sasa ni kuyaingiza maeneo mengi zaidi kwenye Gridi ya Taifa na kuwasambazia kwa umeme watu wengi zaidi. Mpaka sasa ni asilimia 10 tu ya Watanzania wanapata umeme, hivyo kuna kazi kubwa ya kufanya katika eneo hili.

  Katika kutekeleza Ilani, tumeongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini kwa kuanzisha Mfuko wa Nishati Vijijini. Mwaka huu, tumetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili hiyo

  Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akiwahutubia Wananchi wa Dodoma na Wabunge kwenye Ukumbi wa Kilimani, Dodoma tarehe 10 Juni, 2009

  Mwisho kabisa, nawasihi viongozi wenzangu na wananchi kwa ujumla, tuwe wavumilivu na tuiunge mkono Serikali katika kutekeleza mkakati huu.

  Tangu mwaka 2006, mambo hayakuwa mepesi sana, tumepitia misukosuko mikubwa kwa uchumi wetu: mgao mkubwa wa umeme
  , njaa, bei kubwa ya mafuta na bei kubwa za vyakula na sasa msukosuko huu wa aina yake.

  Kwa kila tatizo tumepambana nalo kiume na kwa umakini mkubwa na kuvuka salama. Mshikamano wetu, umoja wetu ndiyo uliotufikisha hapo.


  [FONT=&quot]Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Somanga-Fungu, 16 Agosti, 2010[/FONT]

  [FONT=&quot]Nakushukuru Mheshimiwa William Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini kwa kunialika katika hafla hii ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Somanga Fungu.

  Mradi huu wa umeme ambao umezinduliwa leo, ni mwendelezo wa hatua za Serikali za kutekeleza sera zake za msingi za kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya uhakika, yenye gharama nafuu, na isiyoharibu mazingira yetu

  Changamoto ya kwanza iliyo mbele yenu ni ujenzi wa nyumba bora ili muweze kuunganishiwa umeme majumbani kwenu.

  Serikali itafarijika sana endapo baada ya muda mfupi tutaambiwa kuwa, umeme huu ambao leo unaonekana ni mwingi kuliko mahitaji yenu, hautoshi kwa kuwa matumizi yamekuwa makubwa kuliko umeme uliopo. Hiyo itakuwa changamoto nzuri kwani itadhihirisha kuwa malengo ya mradi huu yamefikiwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Kikwete aahidi umeme mikoa ya Kusini[/FONT]
  [FONT=&quot]Lindi,19 October 2010[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete, amesena tatizo la umeme lililokuwa linaikabili mikoa ya kusini sasa litabaki historia baada ya kufanikiwa kupatikana kwa umeme wa gesi ya asilia kutoka Songosongo.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Alisema wilaya ya Kilwa ambayo ilikuwa ina tatizo la umeme kwa muda mrefu, sasa ina umeme wa uhakika baada kupatikana kwa umeme huo

  [/FONT]
  [FONT=&quot]Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Ibada ya Kumweka Wakfu Askofu Mteule Gervas John Nyaisonga wa Jimbo Katoliki Dodoma, tarehe 19 Machi, 2011, Dodoma[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Jambo lingine ninalowaomba viongozi wa dini muendelee kuiombea nchi yetu ipate mvua za kutosha, mabwawa yajae, umeme upatikane na nchi iwe na chakula cha kutosha.

  Kadhalika msichoke kuiombea nchi yetu amani na upendo miongoni mwa wananchi wake. Jambo kubwa la kusisitiza hapa ni kuwataka watu wapendane, washirikiane na kamwe wasibaguane kwa rangi, kabila, dini, jinsia, maeneo wanayotoka au itikadi za kisiasa.

  Haya ni miongoni mwa mambo ya tunu ambayo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alituachia Watanzania. Ndiyo siri ya amani na utulivu wa nchi yetu. Hatuna budi kuyaenzi na kuyaendeleza."[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT][FONT=&quot]My take: Hizi Ngonjera hizi za Rais sio nzuri kwa mstakabali wa Taifa tokea 2005 mpaka sasa ni mikakati kwenda mbele.
  [/FONT]
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kichefu chefu kama ze-comedy
   
 3. a

  andry surlbaran Senior Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui nimuitaje?
  Malenga wapya au mrisho mpoto?
  Maana ana tenzi nzuri ajabu kama Grace Matata.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii itakuja kusisha lini maana kila mwaka mipango mipango
   
 5. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Alafu naona anasisizita sana swala la kumuomba Mungu kutatua kero ya umeme, huwa anamaanisha
  Mungu gani,huyu huyu ambaye huwa anakwenda kutoa kafara na kumuwashia ubani kwenye viduku...
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Technologia imetusaidia kuwaumbua watawala waongo na makanjanja.. kama kuna mtu ana audio ya ahadi za Kikwete 2010 naomba atusaidie kuzibandika hapa na ikiwezekana Mod aziweke juu kabisa kama alivyofanya kwenye mswada wa katiba ili tuendelee kuwakusha kama wamesahau...!
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Yawezekana kabisa hajawahi kupitia aliyoyatamka kwenye hotuba zake za awali, na wasaidizi katika hotuba zake nao pia yaonekana hawajali wala kutilia maanani umuhimu wa kutorudia rudia yaleyale ambayo yanazidi kugeuka ahadi hewa. Ni kitu gani la msingi jamani ambalo tutaonekana tumeweza kwa asilimia mia na kutamba nalo ndani ya miaka kumi hivyo kuupongeza uongozi wa Mh. Kikwete katika kulifanikisha??

  - Umeme: Tatitzo sugu, ni ahadi tu zimebaikia, kero zinazidi

  - Kilimo kwanza: Kimebakia kwenye manifesto tu, mbolea, pembejeo bado aghali, mazao bado yanaozea mashambani.

  - Ufisadi: Tumebakia kuambiwa ni kujivua magamba tu, hatuoni sheria zikitumika kuwaadhibu waliwo jivalisha magamba hayo.

  - Muungano: This is a time bomb! Kuchomeana makazi na biashara kumeshaanza...

  - Katiba: Bila ya wananchi na Wanachadema kugangamala tungebakia kubambikizwa Katiba kufuru kwa Taifa letu, huku CCM wakibakia kupiga makofi na vigelegele Bungeni!! Katika hili, Mh. Kikwete ana nafasi nzuri ya kujiwekea kumbukumbu ya kutukuzwa katika historia, as long as atabadilika na kuanza kutumikia kiapo alichotoa pale uwanja wa Taifa!!
   
 8. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280

  AUDIO YA NGOJERA ZA UMEME WA UHAKIKA TANZANIA

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ya kawaida kabisa ukiona nchi inaongozwa na kiongozi ambaye ni malaya basi lazima ufahamu kuna tatizo kubwa. Mtikisiko ambao tunakumbana nao ni kutokana na kuwa na rais ambaye sifa yake kubwa ni hiyo, sasa atapata wakati lini kutatua maswala ya kitaifa? Natumaini wengi wanafahamu nini kinaendelea kule Italy ambako wana tatizo kama letu lakini wenzetu wako mbali zaidi ndio sababu hawana mkwara mkubwa kama wetu. Keki yetu ni ndogo na ni hiyo hiyo anayotumia kuwahonga mafisadi sasa hatuwezi kufika mbali ni machungu tu yataendelea hadi pale tutakapoweza kumng'oa kutoka pale magogoni na kumrudisha Msoga.
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sijui kama Rais huwa anarudia hotuba zake kusoma aliyoyaandika
   
 11. bily

  bily JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2014
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 8,019
  Likes Received: 3,917
  Trophy Points: 280
  Kwa kua Mh Rais anakaribia muda wake wa kuondoka madarakani si vibaya tukamkumbusha alichoahidi na hajakifanyia kazi. Back Tanganyika.
   
 12. m

  mumburya JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2015
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 268
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 45
  "Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
  wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  Bungeni, Dodoma, 30 Desemba 2005
  Mheshimiwa Spika:
  Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini.
  Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele
  katika kuboresha na kuendeleza upatikanaji wa
  nishati ya uhakika na rahisi vijijini na mijini.
  Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme
  na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya
  kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi
  mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa
  huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani.
  Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu
  matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa
  umeme nchini.
  Mheshimiwa Spika:
  Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005
  inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne
  itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka
  makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo
  ndivyo tutakavyofanya.
  Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua
  mipango ya umeme wa Mto Rusumo na
  Stigler’s Gorge . Tutaharakisha pia upatikanaji
  wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.
  Mheshimiwa Spika:
  Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni
  kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji
  mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa,
  kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini
  kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na
  kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma
  katika gridi ya Taifa.
  Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  kwenye Baraza la Eid-el-Fitr, Arusha, tarehe
  24 Oktoba, 2006
  Bahati mbaya sana kwa upande wa tatizo la
  umeme hakuna majawabu ya papo kwa papo.
  Hata kwa umeme wa dharura imetuchukua
  miezi isiyopungua mitano tangu tuanze
  mchakato wa kukodi mitambo ya kuzalisha
  umeme.
  Ni sasa tu ndipo baadhi ya mitambo imewasili
  na baadhi kuanza kazi. Ni matumaini yetu
  kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao
  au hata katikati karibu mitambo yote ya
  kukodi itakuwa imewasili na kuanza
  kuzalisha umeme .
  Mitambo hii itakapoanza kuzalisha umeme,
  tutakuwa tumepata nafuu. Lakini, jawabu hasa
  litakuwa limepatikana hapo mwakani wakati
  mitambo mipya ya TANESCO ya Ubungo na
  Tegeta itakapokuwa imeanza kutoa umeme
  Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya
  Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
  Muungano wa Tanzania kwa Watanzania,
  tarehe 31 Desemba, 2006
  Mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa aina yake.
  Upande mmoja ulikuwa mwaka wa mafanikio
  mengi mazuri na kuipatia Serikali yetu pongezi
  na sifa nyingi. Upande mwingine ulikuwa
  mwaka uliokuwa na matatizo machache
  makubwa ambayo yalileta usumbufu mkubwa
  na adha kwa watu wengi nchini.
  Baadhi ya matatizo hasa ya ujambazi na
  umeme yaliwafanya baadhi ya wananchi
  kupunguza imani yao kwa utendaji wa Serikali
  na baadhi ya vyombo vyake. Bahati nzuri, kwa
  majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunaumaliza
  mwaka, matatizo ya ukame, njaa na umeme
  yakiwa hatunayo tena na ujambazi
  tumeudhibiti.
  Tarehe 31 Januari, 2006, nilipoongea na
  Watanzania kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es
  Salaam nilieleza kuwa uzalishaji wa umeme
  katika mabwawa yetu ulipungua kutoka
  megawati 561 hadi megawati 167.5 tu.
  Nilitahadharisha kuwa mgao wa umeme
  hauepukiki. Niliwasihi Wananchi wenzangu
  kuzidisha kumuomba Mungu atujalie mvua za
  kutosha ili baa la njaa liishe na tatizo la
  umeme lisichukue muda mrefu kuisha.
  Kutokana na kujirudia kwa tatizo la mgao
  wa umeme unaoleta usumbufu mkubwa
  kwa watu na kuathiri uchumi wa taifa letu
  changa, nilielezea dhamira ya Serikali ya
  kuanza kuchukua hatua za dhati za
  kupunguza kutegemea mno umeme wa
  maji.
  Nilieleza uamuzi wa Serikali wa kuongeza
  matumizi ya gesi asilia na makaa ya mawe
  kuzalisha umeme. Nafurahi kusema kuwa
  tumekwishachukua hatua muafaka.
  Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
  Jakaya Mrisho Kikwete, Kwenye Ufunguzi
  wa Mkutano wa Nane Wa CCM, Ukumbi wa
  Kizota, 03 Novemba 2007
  Nishati
  Mwezi mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Nne
  ianze kazi ya kuwatumikia Watanzania,
  tulikumbana na tatizo kubwa la aina yake la
  ukosefu wa umeme.
  Tatizo hilo lilisababishwa na ukame ambao
  haujawahi kutokea kwa miaka mingi hapa
  nchini. Maji katika mabwawa ya kuzalishia
  umeme yalikauka, hivyo uzalishaji umeme
  ukapungua sana na kwa baadhi ya vituo
  kusimama.
  Kwa rehema za Mwenyezi Mungu mvua kubwa
  zilizonyesha Desemba, 2006, tatizo la umeme
  limeisha. Ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii
  tulifanya uamuzi wa makusudi wa kuongeza
  wigo wavyanzo vya kuzalisha umeme badala ya
  kutegemea mno maji.
  Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa tumeongeza
  kwa asilimia 60 umeme unaozalishwa kutokana
  na vyanzo vingine.
  Kutokana na jitihada hizi, sasa hivi tuna
  ziada ya umeme kwenye gridi ya Taifa. Sio
  rahisi sasa katika miaka michache ijayo
  nchi yetu kupata tatizo la upungufu wa
  umeme kama lile labda kutokee dharura
  aina nyingine.
  Changamoto iliyobakia sasa ni kuyaingiza
  maeneo mengi zaidi kwenye Gridi ya Taifa na
  kuwasambazia kwa umeme watu wengi zaidi.
  Mpaka sasa ni asilimia 10 tu ya Watanzania
  wanapata umeme, hivyo kuna kazi kubwa ya
  kufanya katika eneo hili .
  Katika kutekeleza Ilani, tumeongeza kasi ya
  kusambaza umeme vijijini kwa kuanzisha Mfuko
  wa Nishati Vijijini. Mwaka huu, tumetenga
  shilingi bilioni 10 kwa ajili hiyo
  Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
  Kikwete, wakati akiwahutubia Wananchi wa
  Dodoma na Wabunge kwenye Ukumbi wa
  Kilimani, Dodoma tarehe 10 Juni, 2009
  Mwisho kabisa, nawasihi viongozi wenzangu na
  wananchi kwa ujumla, tuwe wavumilivu na
  tuiunge mkono Serikali katika kutekeleza
  mkakati huu.
  Tangu mwaka 2006, mambo hayakuwa mepesi
  sana, tumepitia misukosuko mikubwa kwa
  uchumi wetu: mgao mkubwa wa umeme, njaa,
  bei kubwa ya mafuta na bei kubwa za vyakula
  na sasa msukosuko huu wa aina yake.
  Kwa kila tatizo tumepambana nalo kiume na
  kwa umakini mkubwa na kuvuka salama.
  Mshikamano wetu, umoja wetu ndiyo
  uliotufikisha hapo.
  Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
  katika Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa
  Umeme wa Gesi wa Somanga-Fungu, 16
  Agosti, 2010
  Nakushukuru Mheshimiwa William Ngeleja,
  Waziri wa Nishati na Madini kwa kunialika
  katika hafla hii ya uzinduzi wa Mradi wa
  Umeme wa Gesi wa Somanga Fungu.
  Mradi huu wa umeme ambao umezinduliwa
  leo, ni mwendelezo wa hatua za Serikali za
  kutekeleza sera zake za msingi za
  kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
  nishati ya uhakika, yenye gharama nafuu,
  na isiyoharibu mazingira yetu
  Changamoto ya kwanza iliyo mbele yenu ni
  ujenzi wa nyumba bora ili muweze
  kuunganishiwa umeme majumbani kwenu.
  Serikali itafarijika sana endapo baada ya
  muda mfupi tutaambiwa kuwa, umeme huu
  ambao leo unaonekana ni mwingi kuliko
  mahitaji yenu, hautoshi kwa kuwa
  matumizi yamekuwa makubwa kuliko
  umeme uliopo . Hiyo itakuwa changamoto
  nzuri kwani itadhihirisha kuwa malengo ya
  mradi huu yamefikiwa.
  Kikwete aahidi umeme mikoa ya
  Kusini Lindi,19 October 2010
  Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Jakaya
  Kikwete, amesena tatizo la umeme lililokuwa
  linaikabili mikoa ya kusini sasa litabaki
  historia baada ya kufanikiwa kupatikana kwa
  umeme wa gesi ya asilia kutoka Songosongo.
  Alisema wilaya ya Kilwa ambayo ilikuwa ina
  tatizo la umeme kwa muda mrefu, sasa ina
  umeme wa uhakika baada kupatikana kwa
  umeme huo
  Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
  wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
  katika Ibada ya Kumweka Wakfu Askofu
  Mteule Gervas John Nyaisonga wa Jimbo
  Katoliki Dodoma, tarehe 19 Machi, 2011,
  Dodoma
  Jambo lingine ninalowaomba v iongozi wa dini
  muendelee kuiombea nchi yetu ipate mvua
  za kutosha, mabwawa yajae, umeme
  upatikane na nchi iwe na chakula cha
  kutosha.
  Kadhalika msichoke kuiombea nchi yetu amani
  na upendo miongoni mwa wananchi wake.
  Jambo kubwa la kusisitiza hapa ni kuwataka
  watu wapendane, washirikiane na kamwe
  wasibaguane kwa rangi, kabila, dini, jinsia,
  maeneo wanayotoka au itikadi za kisiasa.
  Haya ni miongoni mwa mambo ya tunu
  ambayo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere
  alituachia Watanzania. Ndiyo siri ya amani na
  utulivu wa nchi yetu. Hatuna budi kuyaenzi na
  kuyaendeleza."
   
 13. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2015
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  we' nawe untuwekea vitu gani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...