Umeme: TANESCO yatahadharisha kuwapo kwa mgao!

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Wana-JF,

Pamoja na Waheshimiwa Wabunge kuukataa muswada wa kurekebisha sekta ya umeme nchini, ili kuleta ushindani zaidi na unafuu wa bei kwa mteja, Waheshimiwa Wabunge wameukataa muswada huo, kwa mantiki kwamba hauna manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Lakini kinachoshangaza, labda kufurahisha pia, ni kwamba, kinyume na kauli yao ya awali (hili sikumbuki kama ni TANESCO au Wizara ya Nishati waliosema) kwamba hakutakuwa na mgao wa umeme nchini kutokana na kuwapo kwa mvua za kutosha na kujaa kwa mabwawa ya kuzalishia maji ya Kidatu, Kihansi na Mtera, sasa TANESCO wanageuka na kusema kwamba - tena mapema - mgao huenda ukawapo.

Tafadhalini nendeni mkasome habari hizo hapa http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/20/habari3.php.

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limeonya kutokea kwa mgawo wa umeme kutokana na kutokuwapo kwa mvua za kutosha pamoja na kuhitaji sh trilioni 1.6 kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

Hivyo, shirika hilo limeiomba serikali kutoa fedha mapema, ili kuweza kununua mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL ambao utabadilishwa mfumo wa kutumia mafuta hadi gesi, ili taifa liweze kukabiliana na tatizo la mgawo wa umeme.

Akiwasilisha mada kuhusu mpango wa TANESCO kujikwamua kiuchumi katika semina ya wabunge kuhusu miswada ya sheria za umeme na biashara ya mafuta, Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, alisema tatizo kubwa linalowakabili ni kutokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha, hali inayowalazimisha kununua umeme kutoka katika kampuni mbalimbali binafsi.

Alisema hivi sasa wanafanya mipango ya kununua baadhi ya hisa katika kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas, ili waweze kupunguza gharama za uzalishaji.

Alisema endapo watafanikiwa katika mpango huo dhidi ya Songas watakuwa wakiokoa kiasi cha sh bilioni moja kwa mwezi, fedha ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha umeme maeneo ya vijijini.

“Tuna tatizo kubwa la uzalishaji wa umeme, lakini pia kuna uwezekano wa mwakani kukawa na mgawo wa umeme hivyo tunaiomba serikali itusaidie kutupa fedha, ili tuweze kuinunua IPTL,” alisema Dk. Idris.

Katika hatua nyingine, Dk. Idris alisema menejimenti iliyoondoka ya Net Group Solution kwa kiasi kikubwa ilisaidia kupunguza hasara iliyokuwa ikiipatia shirika hilo.

“Kusema ukweli menejimenti ile kwa kiasi kikubwa imetusaidia kupunguza kupata hasara, kwani tangu waje hasara imekuwa ndogo zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali,” alisema Dk. Idris.

Aidha, alisema kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe wa Kiwira ambao unategemewa kutoa megawati 200 utakuwa mkombozi wa tatizo la umeme.

Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, lakini havitumiki ipasavyo, jambo ambalo linakwamisha juhudi za TANESCO kuwapatia umeme watu wengi zaidi.

Alisema mpaka hivi sasa ni asilimia 10 tu ya Watanzania Bara wanaotumia huduma hiyo huku wale Zanzibar wakipata umeme kwa asilimia 98.

“Tunajipanga kuhakikisha wananchi wa bara nao wanapata umeme kwa idadi kubwa kama ilivyo kwa watu wa visiwani, lakini hali hii haitawezekana kama hatutapata fedha,” alisema Idris.

Aidha, alisema kama fedha zilizoombwa hazitatolewa kwa wakati kuna hatari ya migodi ya Buzwagi na mingineyo kutopata umeme kwa kiasi kinachohitajika.

Alisema TANESCO mwaka jana imeongeza wateja hadi kufikia 32,000 na imepanga kuwa kila mwaka kuongeza wateja 100,000 sambamba na kwamba ifikapo mwaka 2012 ianze kuuza umeme katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Awali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema serikali itaendelea kuisaidia TANESCO, ili iimarike kiutendaji na kibiashara na ijiendeshe bila ya kuitegemea serikali.

Alisema kuna mpango wa kuliwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lifanye biashara ya mafuta, ili kutathmini na kuisawazisha (checks and balances) biashara hiyo nchini inayofanywa pia na mashirika na makampuni mengine.

Waziri Mkuu Pinda alisema katika kuiimarisha TANESCO serikali pia inaazimia kuondoa ukiritimba wa shirika hilo.

Kuhusu TPDC, alisema shirika hilo litasaidia kuifanya serikali itathmini na kuiweka sawa biashara ya mafuta kwa sababu ni rahisi kupitia hesabu za shirika hilo na kuweza kubaini udanganyifu wowote katika biashara hiyo.
Tujadili.

(Mtazamo wangu: Kama JK ataruhusu kuwapo kwa hali hii, ambayo itawaathiri zaidi Watanzania, kwani umeme kwa sasa ni sawa na anasa kutokana na kutozwa kwa bei ya juu sana, basi, hali hii ni mojawapo ya sababu zitakazochangia yeye kutoruhusiwa kugombea tena Urais mnamo 2010... ambayo haiko mbali sana!)

Tumetahadharishwa!

./MwanaHaki
 
Kuna haja ya kuangalia mambo makubwa ya kuangalia ikibidi haya maswala yawekwe kwenye mambo ya dhalula: Kuna hatari tunakoelekea tusifike, Jk sijui anaona haya. Mkapa, Lowassa, Aziz na wengine wotwe waliosaini mikataba ya umeme itabidi tushitane masharti either wanataka hawataki.

Umeme kupanda kwa asilimia 200
2008-03-20 08:39:53
Na Joseph Mwendapole


Shirika la Umeme nchini (TANESCO), linakusudia kupandisha bei za umeme kwa asilimia 200, endapo litaendelea kupata hasara na kulemewa na madeni.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk. Idris Rashid, wakati wa semina ya wabunge kuhusu Muswada wa Sheria za Umeme na Biashara.

Alisema gharama za uzalishaji ni kubwa sana na kwamba bei za umeme wanazotoza kwa sasa haziwezi kufidia gharama za uzalishaji huo.

Alisema shirika hilo limekuwa likipata hasara kila mwaka, hasara ambayo imekuwa ikiongezeka, na kwamba ili kulinusuru linatakiwa kuongeza bei ya umeme kwa wateja wake.

Alitoa mfano kuwa mwaka juzi Shirika lilipata hasara ya Sh. bilioni 183, mwaka jana Sh. bilioni 72, mwaka 2005 Sh. bilioni 0.9, mwaka 2004 Sh. bilioni 15.6, mwaka 2003 Sh. bilioni 177 na mwaka 2002 Sh. bilioni 72.

Alisema mwaka jana waliomba kuongeza bei kwa asilimia 40 wakaruhusiwa kuongeza asilimia 21 tu.

Alisema shirika hilo linatumia asilimia 90 ya mapato yake kununua umeme kutoka makampuni yanayoliuliza umeme shirika hilo.

Makampuni ya wawakezeji ambayo yamekuwa yakiliuzia umeme TANESCO ni pamoja na IPTL, Songas, Richmond na AGGREKO.

Kamati ya Bunge ya Richmond ilionyesha kwamba mikataba ambayo serikali kupitia TANESCO iliingia na makampuni hayo ina upungufu ambao unawanufaisha zaidi wawekezaji na kuwaumiza wananchi wanaolipia bei kubwa ya umeme.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilipendekeza mikataba hiyo ipitiwe upya.

``Hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi mwakani tutaomba tuongeze bei kwa asilimia 200 ili angalau wakipunguza waturuhusu tuongeze kwa asilimia 100 kunusuru shirika,`` alisema Dk. Rashid.

Alisema kama serikali haitaki shirika hilo lipandishe bei ya umeme ililipe shirika hilo fedha zinazotumika kuzalisha umeme.

Alisema hatokubali shirika hilo lijiendeshe kwa hasara na kwamba kila ikibidi watalazimika kuongeza bei kwa wateja.

Aidha, Dk. Rashid, alisema kuwa Sh. bilioni 300 ambazo Shirika hilo lilikopeshwa na benki mbalimbali hivi karibuni, zilitumika kulipa madeni ambayo shirika limeyarithi.

Alisema katika miaka mitano ijayo, Shirika hilo linahitaji mtaji wa Sh. trilioni 1.5 ili liweze kumudu kuboresha mfumo wa usafirishaji umeme na usambazaji.

Dk. Rashid alisema ifikapo mwaka 2012 shirika linakusudia liwe na uwezo wa kuwaunganishia umeme wateja 100,000 kila mwaka kulinganisha na sasa ambapo kwa mwaka ni wateja 32,000 wanaounganishiwa.

Alisema asilimia kumi tu ya watanzania ndio wanapata umeme kwa sasa na kwamba miaka mitano ijayo wamepanga kuwaunganishia umeme asilimia 25 ya wateja.

Alisema wanakusudia pia kupunguza kiwango cha umeme kinachopotea kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 23 hadi kufikia asilimia 13 mwaka 2012.

Katika hali iliyowashangaza wabunge waliohudhuria mkutano huo, Dk. Rashid alisema Tanesco inanunua nguzo kutoka Afrika kusini na India kwa kuwa zinauzwa bei rahisi kuliko zinazotoka Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Alisema wanalazimika kuagiza kutoka nchi hizo kwa kuwa shirika halina uwezo wa kununua nguzo za Tanzania.
 
Naweza kusema kuwa mgao wa umeme ukianza Tanzania tena rasmi (kwani huko mikoani mgao unaendelea kama kawa), Kikwete ataanza tena safari nje ya nchi na wala hatafanya chochote zaidi ya kutafuta karichmond kengine ..... haya ni maoni yangu tu but watch this space wana JF
 
Why are we then paying IPTL, RICHMOND, SONGAS hefty monies....still kuwepo na mgao....something is really wrong.........naanza kuuamini msemo wa Mkuu Nyani.....hivyo ndivyo tulivyo!!.....damn!
 
Why are we then paying IPTL, RICHMOND, SONGAS hefty monies....still kuwepo na mgao....something is really wrong.........naanza kuuamini msemo wa Mkuu Nyani.....hivyo ndivyo tulivyo!!.....damn!

Inawezekana serikalini huko ndio wanaendeleza na kuthibitisha msemo wa ndivyo tulivyo.... kinachoumiza zaidi ni kuwa come the election, tunawachagua hawa hawa baada ya kupewa chumvi .. kwa hiyo tena theory ya FMES kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe inakuwa proved!
 
Ndivyo tulivyo = maana yake watanzania wengi wetu ni wajinga sana tena sana, na hatujui kitu + na uoga na unafiki juu
Wewe pamoja na kukamuliwa pesa zote hizo bado tunaambiwa mgao unakuja??
Wakati huo mh. Aliahidi kipindi kile kuwa wanakodisha generreta za muda lakini serikali itanunua zake mapema ili kuzuia hile hali ya kipindi kile isitokee tena, haya tulitoka wapi, na tulikinga vipi na mgao wa kipindi kile
Na tunashindwa kuwawajibisha hawa watu ndo sababu

Ndo tulivyo!!!!!!
tuna'natural gas' ambayo mwenyezi mungu ametujalia.
Kwa nini tulipishwe bei ghali?
Kwa nini tupate mgao wa umeme?
 
Najua hiyo bill imekataliwa na sio popular kwa wengi humu JF,lakini kuendelea kuipa monopoly Tanesco na kutobadilisha sheria za umeme za sasa sio solution,na umeme utendelea kutopatikana na kuwa bei mbaya kila siku....no energy=no economy!
 
tuna'natural gas' ambayo mwenyezi mungu ametujalia.
Kwa nini tulipishwe bei ghali?
Kwa nini tupate mgao wa umeme?

....sheria za sasa haziruhusu yeyote zaidi ya Tanesco kufanya biashara ya umeme,na Tanesco hawana uwezo wa kutumia hiyo gas kuzalisha umeme ndio maana wamebaki kuingia mikataba ya kitapeli kila siku,cha ajabu hawawezi kununua power plant(which is cheaper) kutumia hiyo gas kuzalisha umeme lakini wanaweza kununua bogus and expensive contracts kuliko hiyo mitambo.
 
Najua hiyo bill imekataliwa na sio popular kwa wengi humu JF,lakini kuendelea kuipa monopoly Tanesco na kutobadilisha sheria za umeme za sasa sio solution,na umeme utendelea kutopatikana na kuwa bei mbaya kila siku....no energy=no economy!

Koba,

hii bill bado haijakataliwa rasmi na kuna uwezekano mkubwa kuwa itapita tu kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha umeme. Tatizo kubwa hapa ni kuwa ni kitu gani kifanyike kwa kina IPTL na wenzake?
 

Je mwajua hili?

Website ya TANESCO inasema 'Serikali imeamua kuibinafsisha TANESCO'
 
Naomba usome kwanza tundiko lote ndio uende kwenye hizo kurasa ulizo niuliza.

http://www.tanesco.com/reforms.html

Hapo wao wenyewe wanasema kwamba serikali iliamua kutaifisha TANESCO.

Na uthibitisho ni kwamba Serikali ilishaipa tenda kampuni ya Ki-South kushauri jinsi ya kubinafsisha na kuipanga upya TANESCO. Na hii nimeipata hapo hapo kwenye website: http://www.tanesco.com/mancontractor.html

Kama bado hawajaibinafsisha ina maana mapesa yetu ya huu mkataba yalitupwa bure. (Nielewe, sisemi wabinafsishe au wasibinafsishe).

Mwisho, ukarasa wa kwanza kabisa wa website yao unasema TANESCO ni kampuni ya Serikali. Kwa maana nyingine, hali yake ya sasa hivi hata wao wenyewe hawaielewi!

Halafu hawawezi hata kurekebisha michongo yao wenyewe iendane. Inawezekana Serikali ilishabadili mawazo na tangazo likatolewa kuhusu mwelekeo wa TANESCO lakini TANESCO wakaacha michongo za zamani ibaki hivyo hivyo kwenye website yao.


Unaona nchi yetu inavyo endeshwa?
 
Naomba usome kwanza tundiko lote ndio uende kwenye hizo kurasa ulizo niuliza.

http://www.tanesco.com/reforms.html

Hapo wao wenyewe wanasema kwamba serikali iliamua kutaifisha TANESCO.

Na uthibitisho ni kwamba Serikali ilishaipa tenda kampuni ya Ki-South kushauri jinsi ya kubinafsisha na kuipanga upya TANESCO. Na hii nimeipata hapo hapo kwenye website: http://www.tanesco.com/mancontractor.html

Kama bado hawajaibinafsisha ina maana mapesa yetu ya huu mkataba yalitupwa bure. (Nielewe, sisemi wabinafsishe au wasibinafsishe).

Mwisho, ukarasa wa kwanza kabisa wa website yao unasema TANESCO ni kampuni ya Serikali. Kwa maana nyingine, hali yake ya sasa hivi hata wao wenyewe hawaielewi!

Halafu hawawezi hata kurekebisha michongo yao wenyewe iendane. Inawezekana Serikali ilishabadili mawazo na tangazo likatolewa kuhusu mwelekeo wa TANESCO lakini TANESCO wakaacha michongo za zamani ibaki hivyo hivyo kwenye website yao.

Unaona nchi yetu inavyo endeshwa?
Oh, {mancontractor}!

Mbona hii web ya TANESCO haifunguki kwangu? I was so interested on reading these stuffs.
 
Naweza kusema kuwa mgao wa umeme ukianza Tanzania tena rasmi (kwani huko mikoani mgao unaendelea kama kawa), Kikwete ataanza tena safari nje ya nchi na wala hatafanya chochote zaidi ya kutafuta karichmond kengine ..... haya ni maoni yangu tu but watch this space wana JF
Mimi natka kujua kitu kimoja,hivi kwa gharama hizo inazotoa Tanesco hazitoshelezi kununua mitambo yake yenyewe ya kuzalishia umeme,kuliko kuingia gharama zote hizo.naombeni msaada wenu kimawazo
 
Mimi natka kujua kitu kimoja,hivi kwa gharama hizo inazotoa Tanesco hazitoshelezi kununua mitambo yake yenyewe ya kuzalishia umeme,kuliko kuingia gharama zote hizo.naombeni msaada wenu kimawazo

Kama Tanesco ikiweza kuzalisha umeme wake kisha kina Rostam Azizi watakula wapi na richmonduli yao?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom