UMEME: Tanesco, Ngeleja OMBENI MSAMAHA Kwa KAKOBE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UMEME: Tanesco, Ngeleja OMBENI MSAMAHA Kwa KAKOBE

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by werawera, Jul 21, 2011.

 1. w

  werawera Senior Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyu mtumishi Kakobe, alizungumza kwa maneno yake kabisa kuwa kwa tukio la Ngeleja na Tanesco Nchi itakuwa Giza.. Yaani hakuna UMEME... na mengineyo. Na huu ni Mwanzo tu.
  Ngeleja nenda hata kisiri kaombe msamaha.. Akikataa kisiri poa tu, hata ikitangazwa inadhuru nini wajameni.
   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Kwa kiburi alichonacho Ngereja sidhani kama ataomba msamaha.
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ngeleja na wenzake wasidhani Mungu atawaacha ipite hivi hivi yeye na wote walioshusha na kuchukua kwa mbwembwe bendera mbili za Mungu (Mabango mawili ) pale kwenye Kanisa la Mungu wa Kakobe na yale mengine yote yaliyotangulia tukio hilo la kebehi na dharau kwa Mungu!!!!. Ni ajabu kwamba mpaka leo hii hata viongozi wa ngazi za Ngeleja na walio juu yake kwa ishara zote hizi bado hawajatambua kwamba Mungu anayehubiriwa na Kakobe ndiye Mungu aliyehubiriwa na Mitume akina Petro, Yohana, Paulo, nk.; hata wafanye dhihaka zote zile walizofanya halafu wategemee kunusurika hivi hivi!!!!!!!! . Pole Tanzania kwa haya matokeo ya laana itokanayo na vitendo vya viongozi wanaotegemea nguvu za majini kuwalinda!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! YETU NI MACHO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ngeleja na ccm ni wabaya sana ila siungi mkono hoja ya kuamini kuwa MUNGU ANAWAHUKUMU WATANZANIA WOOTE WAKE KWA WAUME, YATIMA KWA WAJANE, WALEMAVU NA VICHANGA, MAASKOFU, MAPADRI, MASHEHE NA WAUMINI WAO KWA KUWAPA ADHABU YA KUKAA GIZANI NA KUBEBA MATATIZO MENGI YATOKANAYO NA MGAO ETI KISA NGELEJA KAKOSANA NA KAKOBE, NAWASI HI MSIFIKIRI HILO KWANI MUNGU NI WETU SOTE NA HAWEZI KU2ADHIBU WOOTE KWA KOSA LA NGELEJA, KM KAKOBE ALILAAN KUWE NA STATIZO LA UMEME WATZ WATESEKE BAS NAAMINI NAYY AMELAANIWA KWANI IMEANDIKWA USILAANI USIJE UKALAANIWA, NAOMBA MSIMSINGIZIE MUNGU UZEMBE NI WA JK, NGELEJA NA SERIKALI YA CCM
   
 5. E

  Evergreen Senior Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angel,Mungu anaweza kufanya hata zaidi ya hivyo,alishawahi kuingamiza dunia kwa maji/gharika kwa sababu ya dhambi za Wachache!! Mungu huyohuyo amewahukumu wanawake wote kuzaa kwa Uchungu hadi leo kwa kosa la Mwanamke mmoja zaidi ya Miaka 2000 iliyopita,the same applies to the punishment he has given to men!! Adhabu za Mungu wakati Mwingine huenda kizazi kwa kizazi kwa kizazi!! Shetani naye kwa hila baada ya kumuasi Mungu aliiga utaratibu huu,eg aliigiza kuuwawa kwa watoto wote wa Kiume katika Israel chini ya Miaka 2 Ili kumpata Mtoto Yesu ambaye alimwona kuwa tishio kwa Utawala wake!! Katika namna hiyohiyo pia alimtafuta Mtoto Musa alipozaliwa!! Namfahamu Askofu Kakobe,nilishawahi kuabudu katika Kanisa lake,najua kwamba ni Mtumishi wa Mungu wa Viwango vya Juu sana sema tu km alivyosema Yesu Mwenyewe "Nabii akubaliki kwenye Mji wake" Kwa sababu hii,aliposema Umeme hautowaka nilijua kwa Hakika itakuwa hivyo;i had no doubt!! Ngeleja ameiwakilisha Serikali,wameifanyia dhihaka huduma ya Mungu kwa Kungo'a Mabango mawili na Kupitisha Umeme Mkubwa karibu na kanisa sehemu ambayo maelfu hukusanyika,ile ni hila ya shetani kutaka Kuangamiza Askofu na Waumini siku za Usoni na ndiyo maana Bishop alisimama Kidete kupinga Umeme kupitishwa pale,haikuwa tu Ubabe,Ubishi au hamu ya kusuguana na Serikali,ana macho ya rohoni!! Mwingine atasema,"Kwani huo Umeme umepita karibu na Kanisa la Kakobe peke yake?" jibu lipo hapo juu,Shetani anaweza kuangusha ndege yenye abiria 50 lakini ampate Mmoja tu anayemtaka!! Anaweza kuunguza nyumba zote karibu na Umeme ule lakini target ni Full Gospel Kakobe in particular!!! Hakuna Mamlaka yeyote dhalimu aliyowahi kushinda Mbele ya Mamlaka ya Nuru!! Ngeleja aache Majivuno na Kiburi,akafumie miwaya yake aiweka katikati au apitishie upande wa Mlimani City na Akatubu na kumwangukia Bishop abarikiwe otherwise ule mradi ndiyo basi na pesa zetu wavuja jasho zimekwenda na Maji!!! Majini ya Shehe Yahay hayawezi kufua dafu pale!!!
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ameeeeeeen
  Ila
  Sasa akiomba msamaha umeme ndo utakuja.? nadhani tutofautishe mambo ya imani na utendaji.

  Mungu katupa akili zaidi ya wanyama wengine tutatue matatizo yetu.
   
 7. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwanza ungetuonesha biblia inayohalalisha kupitisha umeme mwingi H.T. kwenye kanisa la kakobe bila ridhaa ya walokole ?!
   
 8. samito

  samito JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na watu wote tuseme amina. umenena vema sana. ngeleja katubu kwa bishop kakobe
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sijawah na wala siwezi kuthubutu kusema kuwa biblia imeandika kuwa tanesko wapitishe umeme kwenye kanisa la kakobe kwani imeandikwa usiongeze wala kupunguza neno nami siwezi kupinga neno la mungu, kwanini mnasema kakobe alilaani umeme usiwake kwa watz wote? Je yy ni nani mbele ya mungu awezaye kulaani taifa zima liteseke?
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo Tanzania kuwa giza Kakobe ndio kasababisha? Haya mimi napita tu! na nchi kukosa chakula kasababisha Babu wa Loliondo?
   
 11. w

  werawera Senior Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hivi relate vitu unavyoongea! Hivi BABU yupo juu tena baada ya Kupigwa chini na Kakobe? Babu ni Kushney.

  ninavofahamu ni kwamba Mungu anaweza kuangamiza hata dunia nzima kwa makosa ya wachache.

  Mi naona hamjaelewa. Ngeleja haadhibiwi yeye kama Ngeleja, anaadhibiwa kama WAZIRI WA NISHATI NA MADINI. hivyo laana ikiwepo kwa waziri maana yake ni pamoja na Wizara na taasisi ndani yake.
   
 12. w

  werawera Senior Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Je MUNGU alikupa akili kuzidi zake? Sasa kama unaamini wewe umetoka kwa Mungu inamaana kila kitu unachokijua ni cha Mungu. Na kama unaamini kuwa kuna MUNGU basi hapo tayari ni IMANI. So conclusion ni kwamba KILA KITU CHAKO ni IMANI.
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kakobe aliacha hy laana lini na tatizo lilianza lini? Na hz nch nyingine zenye matatizo ya umeme ni laana za watu aina ya kakobe, utawala mbovu au ni miundombinu?
   
 14. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Werawera, nimefanya research yangu ndogo, kuhusu issue hii ya umeme; na mimi pia nimeanza kuwa convinced kwamba hapa kuna laana ya Mungu. Yesu aliulaani mtini, ukanyauka! Laana za Watumishi wa Mungu, ziko!


  Tarehe 9.3.2010, ndiyo siku ambayo TANESCO walipoweka nguzo za High Tension kwenye Kanisa la Kakobe. Siku hiyohiyo usiku, kulikuwa na blackout nchi nzima, baada ya milipuko TANESCO Ubungo. Tarehe 19.3.2010, TANESCO wakazidi kuwa kichwa ngumu, wakaondoa mabango ya Kanisa, huku askari wakielekeza juu mitutu ya bunduki. Baada ya kuyang'oa mabango ya Kanisa kwa ubabe huo, yakaburutwa mpaka TANESCO.


  Katika mahubiri ya Kakobe, Jumapili iliyofuata ya tarehe 21.3.2010, yenye kichwa, "USIWAOMBEE WATU HAWA WAPATE HERI", Kakobe alisema TANESCO na Wizara ya Nishati, wamemuonyesha Mungu mitutu ya bunduki, wakati wanang'oa mabango ya Kanisa, kama vile wana nguvu kuliko Mungu na kwamba wanaweza kumpiga risasi Mungu. Akasema, wamekufuru; na hivyo, they were going to pay the price!


  Tangu wakati huo, ndiyo ukaanza mgao wa umeme, na blackouts, kwa proportions zilizokuwa zinaongezeka kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele. Mara kadha, Badra Masoud wa TANESCO, aliwahi kuulizwa, je, hili halina uhusiano na laana ya Kakobe? Akawa anajibu kwa jeuri kwamba ni matatizo ya kawaida tu ya kiufundi! CLOUDS FM, walikuwa na mijadala mingi juu ya jambo hili la laana ya Kakobe.


  Alhamisi tarehe 8.7.2010, mbunge mmoja Bungeni, aliuliza swali bungeni akihusisha mambo ya umeme na Kakobe. Akijibu swali hilo siku hiyo, Ngeleja alisema kwa jeuri, kwamba mambo ya umeme hayahusiani na mambo ya imani; wao wanafanya mambo kisayansi. Kakobe naye akajibu mapigo ya Ngeleja kwa mahubiri yake Jumapili iliyofuata ya tarehe 11.7.2010, yaliyokuwa na kichwa,"BABA WA SAYANSI ZOTE". Katika mahubiri hayo, Kakobe akasema Mungu ndiye author wa sayansi zote, pamoja na umeme. Akasema, Ngeleja na TANESCO, watajua jambo hili kivitendo, wasipotubu!


  Tangu wakati huo hali ya umeme, na mgao wa giza, imezidi kuwa mbaya mpaka kufikia hali hii tuliyo nayo sasa. Siyo kweli kwamba Tanzania imekuwa na ukame wa kutisha mwaka huu. Mvua imenyesha ya kutosha tu Mbeya, na kwingineko ambako ni vyanzo vya maji ya Mtera! Lakini suprisingly, pamoja na mvua hiyo, maji katika bwawa la Mtera, badala ya kujaa, yamekuwa yakipungua kila kukicha!


  Wajameni, Ngeleja na TANESCO, Mungu yuko; na Watumishi wa Mungu aliye hai, kama Eliya; bado wako duniani hata leo! Let this give you food for thought! Inawapunguzia nini kuomba msamaha kwa Kakobe, for your sake, and for the sake of Tanzanians? Vilevile, kwa Watanzania wenzangu, tuache kejeli katika jambo hili! Kisasi cha Mungu kinatisha! Labda giza halijatosha, litakapotosha labda ndipo TANESCO watakapomwogopa Mungu, kama Kakobe alivyowaambia katika T-Shirt zake, katika sakata lake na TANESCO!
   
 15. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo lilianza 2006 na likaendelea mpaka likawa kubwa kias kilichofikia sasa, siamini kuwa ni laana ya kakobe ila sipendi kuendelea kupinga imani za wa2 juu ya laana ya kakobe na tatizo la umeme, tufunge na kuomba mungu atatusaidia
   
 16. l

  lily JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa wewe unaendika hapa umemem unao wewe! pls be the 1st to say sorry 2 kakobe
   
 17. w

  werawera Senior Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hapa tunaongelea Tanzania....
   
 18. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Angel, mbona uko very out of date? Hujajua kwamba Babu wa loliondo alikwisha kazi kitambo? Tafuta Mwananchi Mei 29, 2011, utaona picha kubwa front page, Babu wa loliondo akijenga nyumba, na chini ya picha kuna caption, "Babu wa loliondo amerudia kazi yake ya zamani ya ujenzi wa nyumba, baada ya kukosa wateja".
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ukweli utabaki palepale nch zote znazokumbwa na tatizo la umeme ikiwemo tz tatizo ni 1.miundombinu ambapo mitambo ya zamani isiyoweza kuzalisha umeme wa kutosha 2. upungufu wa mvua na lzm tatizo lijitokeze sbb hakuna vyanzo vngne vya uzalishaji wa umeme eg: upepo 3.utawala mbovu kwa viongozi kushindwa kulismamia tatizo kwa uzito unaostahili au yote 3 kwa pamoja. Kati ya hayo 3 je hakuna linalohusika na tatizo la hapa TZ?
   
 20. E

  Evergreen Senior Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawasawa Werawera,Unajua tunatofautiana viwango vya Ufahamu wa Neno la Mungu,Tofauti hizi zinaweza kusababishwa na Factors mbalimbali zikiwemo uwezo wa akili wa Mtu husika lakini muhimu zaidi ni nani alikuwa Mwalimu wako wa neno la Mungu!! Kama mtu ulifundishwa na Mwalimu ambaye yeye mwenyewe ni Mwanafunzi basi kwa Mafundisho hayo Manyonge mtu huyaendea maisha yake yote ya Mwili na ya kiroho!! Kama alivyouliza hapo ANGEL MSOFFE,Kwamba kwa nn mnasema Kakobe alilaani?,Wakati Kakobe anasema Maneno hayo hakuongea Kiyunani wala Aramaic language,aliongea Kiswahili!! Hapa swali lilitakiwa liwe unabii wake Umetimia? Jibu ni NDIYO,UMETIMIA!! Pale kanisani kwake zimepita nyaya tu,hakuna Umeme!!! Mungu anaweza kuangamiza Taifa zima kwa dhambi za Wachache na Mungu huyohuyo anaweza Kulisamehe Taifa zima kwa sababu ya "Mwenye Haki" Mmoja tu kama alivyowasamehe wana wa Israel kwa ajili ya Musa tu!! Kilichotokea hapo sio kipya kwa ss ambao tunachukua muda kuyachunguza Maandiko,Hakuna Jipya,Nabii Elia aliizuia Mvua katika Israel isinyeshe kwa Miaka 3 licha ya jitihada za Wachawi na Waganga wa Israel kutaka kuzuia maombi yake,Mvua haikunyesha mpaka walipomuangukia Elia!! Ipo mifano Mingi!! Sasa Leo hatuna akina Elia,tunao akina Kakobe ni imetokea!! Kakobe alisema ule Umeme uliopita katika kanisa lake hautowaka na nchi itakuwa gizani na IMEKUWA HIVYO!! Need I say More Angel Msoffe? Elia alionyesha Nguvu ya Mungu anayemwabudu mbele ya Waganga na wachawi wa Israel na ikadhihirika!! Tusemeje sasa,kwamba Askofu Kakobe alikuwa na Hamu tu ya Kugombana na serikali? Ni mjinga tu asiyejua anachokisema? Kwamba hakuwa sahihi kupinga kupitisha Umeme Mkubwa kiasi kile karibu kabisa na Kanisa lake? Hoja kwamba eti Kakobe ni nani mpaka atoe laana haina Mashiko,swala hapa hiyo laana haijaipiga nchi? Babu wa Loliondo anapata wateja kama Mwanzo? au ndiyo tuseme kwamba watu wenye magonjwa aliyekuwa anatibu yamekwisha au kwamb hawana nauli kwenda Samunge au tutasema Wanahabari hawampi Coverage? The devil's mission has been accomplished at Samunge,tusubiri tu vilio kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja!! Its illusory healing!!Kama hiyo dawa yake ni hakika si Ulimwengu wote ungehamia Tanzania? Au imesikika tu kwa Wacongo,wanyarwanda na waganda wachache? Mkakati wa Muda Mrefu wa Lucipher behind that project ni kuja kuliangamiza kanisa lile kwa mOto mkubwa liwe Majivu na strategically ajali ya namna hiyo lazima itokee Jumapili!! "Msiache kuzijua Njia zake yule Mwovu",The devil is profoundly strategic and tricky",kwa nje unaonekana ni mradi wa Maendeleo lakini hiyo kwake yeye ni "by-product" yeye anayo makusudi yake!! Ataangamiza hata na majengo na watu wengine ku-disguise kwamba si yeye at work!!! Tumeagizwa kutokumpa shetani NAFASI! Kuruhusu Umeme Mkubwa namna ile ni kumpa nafasi Shetani,Kuruhusu wanaume wageni au hata wenyeji kulala chumba kimoja na watoto wako ni kumpa Shetani nafasi,Kukaa faraghani na mwanamke asiye wa kwako ni kumpa shetani nafasi,kujenga miundombinu mibovu ya barabara unampa shetani nafasi nzuri ya kuandaa ajali,kuendesha wakati umelewa ni kumpa shetani nafasi;Kutembea Usiku wa Manane peke yako ni kumpa shetani nafasi n.k!! Tunaweza kuandika hapa mifano,hali na mazingira mengi yahusuyo kuweka mazingira ya lazima kwa shetani kufanya kazi zake,itoshe tu kusema Bishop Kakobe na wote tuliojifunza neno vizuri tunajua fika kwamba Shetani hafanyi kazi unless apewe nafasi,KUKOSA MAARIFA YA MAMBO YA ROHONI!! Katika Afrika Shetani ana-operate kirahisi na anaonekana dhahiri akiwa kazini kuliko sehemu yeyote ya dunia kwa sababu huku maisha yetu kwa ujumla yanamtengenezea CONDUCIVE ENVIRONMENT kwa yeye kutekeleza majukumu yake on day to day basis!!! Nonetheless,si busara kuendelea kubishana saaaana,ni kujilisha upepo,skeptics walikuwepo hata wakati wa Yesu mwenyewe!! Wenye Masikio na Wasikie,Ule Umeme pale Sam Nujoma Hautowaka kamwe,ndiyo watamjua Kakobe ni nani until wakaiondoe Midubwasha yao pale!!
   
Loading...