Umeme nao sasa tuudai kwa nguvu, kwa shinikizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme nao sasa tuudai kwa nguvu, kwa shinikizo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by bensonlifua92, Dec 9, 2010.

 1. b

  bensonlifua92 Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kwa muda wa zaidi ya miaka mitano tunashuhudia Tanzania ya majiji na mijini kukumbwa na adha ya umeme. Hicho kinacho itwa umeme wa mgao kimekuwa ni adha kubwa mno kwa watu wengi isipokuwa kwa hao wanaokula nchi hii kwa raha zao.:frown:

  Unarudi nyumbani labda tuseme jioni angalau ufurahi na watu wa nyumbani kwako, unakaribishwa na giza nene toka mlangoni hadi ndani. Ni jambo la kusikitisha pale ambapo waziri anatoa ahadi za kitoto kuwa umeme wa mgao Tanzania utakuwa ni historia halafu huoni jitihada za kweli katika hilo isipokuwa blablaaa Tu!!!.

  Hivi thinkers tatizo ni maji/ukame/uchumi au ni uwezo wa mkuu wa kaya ya TZ (au basi na hao wengine) wa kujua nini kifanyike ili umeme uwepo muda wote????? Au ndo njia ya hao vigogo mafisadi kuendelea kufisadi watanzania kwa njia hii ya IPTL, Dowans, Richmond, n.k???

  Nionavyo mimi Hii kitu umeme wa uhakika hautaweza kupatikana hadi pale watanzania tutakapoweka shinikizo la kuudai kwa nguvu. Pengine tuitishe maandamano kila mahali TZ nzima kwa siku kadhaa hadi kieleweke. Kama tunavyotaka kuweka shinikizo la kudai Katiba mpya na Tume huru basi yapo mambo mengi (umeme ukiwepo) ambayo hatuwezi kupata ila kwa shinikizo kubwa la NGUVU YA UMMA!!!!!

  Asanteni thinkers

  Benson
   
 2. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hiyo ni sawa kabisa mkuu,tunalipa hivyo tuna haki ya kuhudumiwa na huduma yenyewe lazima iwe bora,hivi hata kama ni mgao mbona huwa wanawasha na kuzima hovyo hovyo bila kujali hatari wanayoisababisha majumbani mwetu.hii ni haki yetu hatuhitaji kuambiwa kwamba kina cha maji kimeshuka kwenye mabwawa,kwani nchi zenye ukame wao umeme wanaupata wapi.
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,757
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu tatizo lipo kwenye ushindani................TANESCO hawana mshindani...........NAKUMBUKA ENZI ZA TTCL...... Zamani TTCL ukiataka kupata simu ilikuwa ni bonge la mlolongo na TIME consuming...... lakini leo hii ukitaka simu toka TTCL it will hardly take a week if not within two days. Ni shirika pekee ambalo halitumii opotunities za biashara ilizonazo tena za wazi
   
Loading...