Umeme: kipindi mwaka 2000 - 2012 hakuna bwawa jipya la umeme lilojengwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme: kipindi mwaka 2000 - 2012 hakuna bwawa jipya la umeme lilojengwa?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by bagamoyo, Oct 9, 2012.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 2,119
  Trophy Points: 280
  Wanabodi ya JamiiForums,
  Tanzania ina upungufu mkubwa wa umeme, lakini tukiangalia miaka ya awamu ya kwanza chini ya Mwl. J.K Nyerere, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kulikuwa na juhudi za makusudi kuongeza vyanzo vya umeme utokanao na maji ili kukidhi mahitaji ya umeme nchini.

  Kila mmoja anajua kuwa kuna chanzo cha Stielger Gorge (Tanzania: Stiegler's Gorge Power Project MOU Signed allAfrica.com: Tanzania: Stiegler's Gorge Power Project MOU Signed ) chenye uwezo-tajwa 2100MW lakini hakuna juhudi au kelele nyingi za serikali ya awamu hii ya 2005-2015 kufanikisha ujenzi na kisha uzalishaji wa umeme kuondoa kabisa tatizo la umeme.

  Umeme wa Stielger Gorge 2100 MW pamoja na vyanzo vya umeme utokanao na gesi pamoja na makaa ya mawe ungeweza kuiweka Tanzania katika chati ya nchi zisizo na tatizo la nishati na kuwezesha kuleta mapinduzi ya viwanda, usafiri wa treni, mabasi ya umeme(trams) na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa.

  Basi tutizame vyanzo vya sasa vya umeme utokanao na vyanzo vya maji na miaka miradi hiyo ilipokamilika:

  Historia ya ujenzi wa mabwawa ya umeme:
  • 1964- Hale uwezo megawati 21MW
  • 1965 - Nyumba ya Mungu megawati 8MW
  • 1979- Mtera megawati 80MW
  • 1980s- Kidatu (Phase I & II) megawati 204MW
  • 2000 - Lower Kihansi megawati 180MW

  Wanabodi, tatizo ni nini hasa hata kuifanya serikali isiwe na mshawasha wa kumaliza tatizo la nishati na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo hapa Tanzania?

  [​IMG]

  Sources;
  Welcome to TANESCO
  The United Republic of Tanzania – Ministry of Energy and Minerals
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  bwawa la maji?
   
Loading...