Umeme Juuu next week! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme Juuu next week!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Aug 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Inaelezwa kuwa gharama za kulipia umeme zitakwea hewani kwa asilimia tatu zaidi kuanzia Septemba mosi, mwaka huu, ili kulipia Mfuko wa Umeme Vijijini (REA), imefahamika.

  Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), wateja wote wanaotumia umeme na wananchi wote kwa ujumla, watatakiwa kulipa ushuru wa asilimia tatu kwa ajili ya mfuko huo.

  Tangazo hilo lililosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari jana, lilisema kuwa ushuru huo unatozwa kwa kuzingatia Tangazo la Serikali (GN) la Agosti Mosi, 2009 na ainisho la sheria ya Bunge kuhusu Wakala wa Umeme Vijijini (Rural Energy Act of 2005), kifungu namba 19 (3) ( c ) na (d).

  “Ushuru huu ni kwa ajili ya Mfuko wa Umeme Vijijini ambao matumizi yake ni pamoja na kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini na mafunzo kwa wajasiriamali ili kuboresha maendeleo ya jamii kwa kutumia nishati bora vijijini.

  “Ushuru huu utakuwa ni asilimia tatu (3%) ya thamani ya umeme uliotumiwa katika mwezi husika, yaani juu ya gharama ya matumizi ya umeme,” ilisema sehemu ya tangazo hilo.

  TANESCO kupitia tangazo lake hilo, imeeleza kuwa yenyewe itakuwa ni mkusanyaji tu wa ushuru huo, ambapo makusanyo yote yatakabidhiwa REA.

  Kutokana na tangazo hilo, sasa katika ankara ya umeme mteja atapaswa kulipia asilimia 18 kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), malipo kwa EWURA asilimia 1 na Mfuko wa Umeme Vijijini (REA), asilimia 3.

  “Hii inatokana na upungufu wa nafasi katika fomu ya Ankara. Hata hivyo, kwa sasa tunatengeneza fomu mpya ambayo itaonyesha kila gharama peke yake. Tunategemea fomu hii itakuwa tayari kabla ya mwisho wa mwaka 2009,” ilisema sehemu ya tangazo hilo.


  Source: DarHotWire.com
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa mnatakaje?umeme wa bure?
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Imawezekana kabisa kama kusingekuwa na richmond, merememta, radar, ndege ya raisi na chai ya billioni tisa, umeme ungekuwa wa bure. Kutokuwa na priorities ndiko kunakopandisha umeme.
   
 4. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  suala hapa sio umeme wa bure... kila mwananchi anatakiwa kuachangia maendeleo ya umeme vijijini sio watumia waliopo sasa ambao ni wastani wa wateja 600,000. Tatizo la Tanzania wale wanaolipa kodi ndo huwa wanaendelea kukamliwa zaidi.... nadhani wangetafuta njia nyingine ya kupata hizo fedha za miradi yao...

  kwa maana hiyo katika kila shilingi mia utakao tumia kununulia umeme, shilingi 21 zitakuwa ni kodi mbalimbali weka na service charge kwa mwezi ambayo ni sh 3000, kwa mlalahoi kama mimi ili niwashe bulb yangu ya sebuleni na chumbani ni lazima niwe na buku 10 !!!!!

  mandeleo yaletwe na wote sio 600,000 tu!!!!!
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tutajuuuuuutaaaaa kuifahamu ccm!
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kupanda kwa bei kulitakiwa kuendane na huduma siyo bei inakuwa juu na umeme wenyewe ndo ule wa kukatika kila dakika.

  Ni vizuri serikali na TANESCO watafute vyanzo ambavyo wanawe zalisha umeme kwa bei nafuu zaidi kuliko kulalia zaidi kwenye kuwakamua wananchi ambao ukiangalia kwa undani unakuta vipato ni vidogo sana.

  Pia CCM wasiwakumbatie mafisadi maana ndo waliochangia hadi tumefika hapa.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tulishazoea wapandishe watakavyo hata wakitaka asilimia mia sisi tutalipa tu kwani kuna la kujitetea? hata kama sitaki nitapata huduma hiyo muhimu kwa nani?
  Wapandishe tu hamna noma tutalipa tu!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  watanzania wote wangekuwa kama wewe nchi ingeendelea kwa haraka,matatizo yetu ni kuwa kila mtu ni mjuaji na mbishi hata kwa mambo ya faida,kila mtu ni "much know"
   
 9. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mchukia Fisadi!

  Kwenye kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 3% sio ufisadi au kwa manufaa ya tanesco bali ni katika kutekeleza sera ya CCM ya MAISHA BORA kwa kila Mtanzania!! Huna wa kumlaumu haya ni matunda ya kura zenu za kishindo zilizomweka JMK mtoto wa CCM madrakani!

  Serikali ya CCM badala ya kubadili sheria ya kodi ili madini yachangie kwa kiwango cha maana katika kupeleka umeme vijijini wameona wawabebeshe ailimia 10% ya watanzania wanaopata huduma ya umeme kuwapelekea umeme Watanzania asilimia 90% wasiokuwa na umeme. Hii sio njia muafaka kwani watu wote waliohai wangepaswa kuchangia kama CCM imekosa mbinu!
  Kazi ya kufanya electrification ni kubwa hizi mbinu za kichovu za hawa wahuni wa CCM plus a few members of parliament calling themselves opposition.
  Kuna haja ya kutafakari na kuweka mpango mkubwa wa kufanya kazi hiyo.

  What comes from the 3% is a pea nut assume ni Tshs 740m/= per month itachukua karne ngapi kupeleka umeme vijijini!!

  Msichekelee this is national tragedy!!! Janga la kitaifa nyie CCM cant you use your grey matter!!!

  Toeni mawazo msilalamike tujenge hoja na msiseme ufisadi ina maana serikali is a big fisadi or what?
   
Loading...