Umeme bado ni tatizo Zanzibar maisha yapanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme bado ni tatizo Zanzibar maisha yapanda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Dec 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  HUDUMA muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu zimeonekana kupanda ghafla baada ya kukosekana kwa umeme visiwani Zanzibar . Moja ya huduma muhimu ni kule kupanda kwa mafuta Kutokana na tatizo hilo linalowafanya wakazi wa visiwani humo kushindwa kumudu gharama za matumizi hayo ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku..

  Tangu kukatika kwa umeme, kumebainiwa kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa wakazi na kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wanaotumia umeme kwani wengi wao wamefunga biashara zao kutokana na tatizo hilo.

  Biashara zilizoathirika na tatizo hilo la umeme ni pamoja na saluni za kiume na kike, vibanda vinavyotoa huduma mbalimbali vikiwamo vya vinywaji baridi, wauzaji wa samaki, baa, kumbi za starehe, nyumba za kulala wageni huku biashara ya teksi na daladala, zikionekana kusuasua na kuwa ngumu kutokana na ukosefu wa mafuta .

  Hivyo mji huo umekumbwa na tatizo la miungurumo ya jenereta kila kona ambapo inakuwa kero kwa wagendi waiingiao visiwani humo.

  Pia tatizo hilo limeonekana kusimamisha baadhi ya ajira kwa vijana visiwani humo.

  Katika taarifa zilizozifikia nifahamishe ilidaiwa kuwa baadhi ya wakazi na maharusi hujenda Dar es Salaam kwa ajili ya matengenezo ya nywele kwa kuwa saloni nyingi visiwani kufungwa kutokana na aujosefu wa umeme.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3777918&&Cat=1
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mgawo wa umeme unavyotafuna uchumi Tanzania

  SEPTEMBA mwaka huu, Shirika la Umeme nchini (TANESCO) lilitangaza kuanza kwa mgawo wa umeme nchini kote.

  Mwandishi MARIAM MKUMBARU Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma, anayesomea Shahada ya Kwanza ya Uhusiano wa Kimataifa, anaeleza athari za mgawo huo, kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.

  Moja ya mambo yanayowakera Watanzania wengi hapa nchini, si jingine zaidi ya hili la mgawo wa umeme.

  Ni majuzi tu tumetoka kumaliza mgawo huo, kwa baadhi ya maeneo ya hapa nchini na mengi bado yanaendelea kupata mgawo wa umeme, ambao kusema kweli unaathiri uchumi.

  Viwanda na maeneo mengine ya uzalishaji ndivyo vilivyoathirika zaidi kutokana na mgawo huo.

  Uchumi wa nchi unaporomoka sana, kutokana na ukosefu wa nguvu ya umeme wa uhakika. Kama tungeyatumia vizuri madini ya urani, ambayo yapo hapa nchini, basi mgawo wa umeme ungekuwa hadithi katika nchi hii.

  Tangu kuanza kwa mgawo huo, wafanyabiashara mbalimbali wameshaathirika sana na kusababisha kupungua kwa uzalishaji viwandani, pamoja na kusababisha kushuka kwa pato la taifa.

  Kumbuka nishati ya umeme nchini inachangia asilimia 35 ya pato la Taifa (GDP).

  Mara nyingi tumekuwa tukiambiwa kuwa sababu za kuwepo kwa mgawo huo ni kupungua kwa maji kwenye vituo vya kuzalisha umeme vya Kihansi, unaozalisha megawati 60 na Pangani 50, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mitambo mingine iliyoharibika ni ule wa Songas ulioko Ubungo, Dar es Salaam unaozalisha megawati 20 wa Hale unaozalisha megawati 8.

  Kuharibika kwa mitambo hiyo kulibakizia Shirika la Tanesco, umeme wa megawati 100, kwa nchi nzima, kutoka megawati 500 hadi 600 zilizokuwa zikizalishwa.

  Hakuna shaka kuwa mgawo wa umeme umesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa viwango vya uzalishaji katika makampuni makubwa hapa nchini, hasa yale yenye mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi, kupunguzwa kazi kwa watumishi wa viwandani, gharama kubwa kutumika wakati wa kuwasha mitambo na kukithiri kwa bidhaa za kigeni katika soko la ndani na pamoja na zile bidhaa feki.

  Akielezea hali hiyo, Ofisa Mipango wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Mdee alisema kuwa viwanda vinavyolipa kodi kubwa hapa nchini kwa thamani ya shilingi ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambayo inalipa kiasi cha shilingi bilioni 12 kwa mwezi, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) shilingi bilioni 10, Kampuni ya Sigara Tanzania Sh bilioni 7.

  Kampuni nyingine zinazochangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa ni Tanzania Portland Cement, Steel Masters Ltd, Tanzania Distillers Ltd, Tanzania and China Friendship Textile Co.Ltd, Tanga Cement Company Ltd, Tanzania Printers Ltd na Tanzania Tea Packers Ltd.

  Kwa mujibu wa Mdee, asilimia 10 ya mapato ya Serikali, yalipungua kutoka katika viwanda mbalimbali vya uzalishaji hapa nchini, ambapo ni zaidi ya shilingi bilioni 15, kwa mwezi, ambazo ni sawa na asilimia 35 ya kodi katika uchumi wa Taifa.

  Mkurugenzi wa Sera na Ushauri wa Shirikisho la Viwanda nchini, CTI, Hussein Kamote alisema mgao wa umeme unaikosesha nchi zaidi ya shilingi bilioni 1.7 kwa mwezi kutokana na kukosekana kwa tija na ufanisi wa umeme viwandani.

  Alisema kuwa, sekta nyingine nazo zinaingia hasara ya asilimia 10 sawa na shilingi bilioni 42,466.8, kwa mwezi kutokana na mgao wa umeme.

  Mfano mzuri wa athari za mgawo wa umeme ziko katika kiwanda cha Gold Star, kilichopo Temeke, Dar es Salaam, ambacho kinatumia mafuta ya dizeli lita 600, kwa siku sawa na shilingi 800,000, ili kuweza kuwasha mitambo mbalimbali ya kuzalisha rangi na makopo kiwandani hapo.

  Kusema kweli, kiwanda hicho kimeathirika vibaya, katika kupanga mikakati ya kiwanda hicho kutokana na mgawo huo, ambapo ilipanga kuongeza uzalishaji, kwa ajili ya kupeleka bidhaa hizo katika Soko la Shirikisho la Afrika Mashariki, ambalo limezinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete.

  Kiwanda hicho kilikuwa kimepanga kuzalisha tani 50, kwa siku, kwa ajili ya wateja wa hapa nchini, lakini wanatarajia kuongeza tani 20 ya rangi ili soko hilo la Afrika Mashariki na kufunga transfoma la umeme kiwandani, hapo ambalo wamelinunua kwa shilingi bilioni 16, ambapo litasaidia kuongeza umeme katika kiwanda hicho na kuleta ufanisi wa hali ya juu, lakini wameshindwa kutekeleza mipango hiyo kutokana na mgawo wa umeme.

  Umeme wa mgawo pia umesababisha ucheleweshaji wa bidhaa mbalimbali za wateja, badala ya kupata kwa siku moja inafikia siku tatu hadi nne kitu, ambacho kinachangia kuvunjika kwa mikataba baina ya mwenye kiwanda na mteja na kusababisha kupoteza wateja.

  Aidha, Kiwanda cha Gold Star, hali hiyo imesababisha kupata hasara ya kukarabati mitambo ya kiwanda hicho, kwa mara tatu kwa wiki, ukarabati huo unatokana na kuzima kwa mitambo kiwandani hapo, ili kupisha ukarabati wa hali hiyo pia utaongeza kwa bajeti, ambayo haikupangwa kiwandani hapo.

  Naye, Meneja Miradi wa kiwanda cha Steel Masters Ltd, Laurence Manyama alisema uzalishaji katika kiwanda hicho cha chuma na bati umepungua sana kutokana na mgawo huo, jambo ambalo limechangia kurudisha nyuma maendeleo ya kiwanda.

  Alisema mpango mkakati (Strategic Plan), wao umeathirika kwa kushuka kwa uzalishaji kwenye kiwanda hicho, kwa sababu walikuwa na mikakati ya kuongeza uzalishaji, ili kuingiza bidhaa zao katika Soko la Afrika Mashariki, ambalo limefunguliwa hivi karibu.

  Alisema kuwa, mgawo huo umesababisha wapunguze wafanyakazi 30 na wengine 50 wamekwenda likizo bila malipo, ambapo hayakuwepo kwenye mipango yao, jambo ambalo limeathiri bajeti ya kununua malighafi za kuzalisha chuma na bati kwa sababu fedha zilizotumika hazikuwemo kwenye bajeti ya kuwalipa wafanyakazi waliopunguzwa na waliokwenda likizo.

  Aidha kupunguza huduma za jamii kwa Watanzania, mbalimbali kwenye sehemu nyingi kama shule, hospitali, maabara, walemavu, wajane, wagonjwa wa moyo na ujenzi wa nyumba za walimu na vifaa mbalimbali vya michezo kutoka shilingi milioni 500 hadi Sh milioni 800.

  http://www.habarileo.co.tz/makala/?n=4869
   
 3. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...aaaah! ZANZIBAR kwisha habari Kudadek!
   
Loading...