Umelifahamu jina la Mama yako ukiwa na miaka mingapi?

jeipm

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
500
820
Waungwana mada inajieleza yenyewe

Kwangu Mimi nimelifahamu jina la Mama yangu nilipofanya matembezi kwa Bibi mzaa Mama ndipo nilipolijua jina la Mama

Wakati huo nilikuwa ndio nimemaliza darasa la saba na wakati huo nilikuwa na miaka 15

Je, wewe? Na unafikiria ni kwa nini?
 
Mimi na ndugu zangu huwahi kulijua, wakati tukianza kuongea. Maana mara nyingi baba alikuwa akimuita jina lake, hapo na sisi tunaunga kumuita.

Ilikuwa raha kumuona akiwakataza wadogo wangu wasimuite jina lake wamuite mama.
 
Waungwana mada inajieleza yenyewe

Kwangu Mimi nimelifahamu jina la Mama yangu nilipofanya matembezi kwa Bibi mzaa Mama ndipo nilipolijua jina la Mama

Wakati huo nilikuwa ndio nimemaliza darasa la saba na wakati huo nilikuwa na miaka 15

Je, wewe? Na unafikiria ni kwa nini?
Dah...ndiyo tatizo la shule za FM academia.. uzungu mwingiiiii ...sasa yale maswali ya std I ulikuwa unajibu vipi? Baba anaitwa........... Mama jina lake ni ......... 🤣 🤣🤣
 
Baada ya mimi kumaliza Sunday school na kuanza kusali jumuia ndio nikawa nasikia wanamuita😅
 
Dah...ndiyo tatizo la shule za FM academia.. uzungu mwingiiiii ...sasa yale maswali ya std I ulikuwa unajibu vipi? Baba anaitwa........... Mama jina lake ni .........
Hahahaha... Na haya yalikuwa ni maswali ya kuanzia chekechea mpaka darasa la kwanza
 
Jina la mama nimelijua secondary...
tena baada ya kuulizwa jina la baba nikataja kwa ukamilifu......
jina la mama nikashindwa.....
ikanibidi nirudi hme kuuliza kwa aibu
 
Nakumbuka mpwa wangu 4yrs alipanick baada ya kumsikia mama yake akimwita mama,mama yangu.yaani bibi yake.

Sasa sijui kichwani mwake alidhani mama yake hajazaliwaga na mtu???
 
Back
Top Bottom