Umekwenda wapi ujasiri wa JK alioanza nao wa kuona haki inatendeka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umekwenda wapi ujasiri wa JK alioanza nao wa kuona haki inatendeka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 30, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwezi mmoja tu hivi baada tu ya kuingia madarakani, mapema 2006, kulitokea mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa Mahenge uliofanywa na polisi ambao walidai ni majambazi. Baada ya kusikiliza kilio cha wananchi kuhusu utata wa suala hilo - kwamba huenda waliouwawa hawakuwa majambazi, JK alichukua hatua kubwa ya kijasiri ya kuunda tume huru ya kulichunguza suala hilo -- Tume ya jaji Kipenka.

  Tume hiyi ilifanya kazi nzuri sana na wananchi waliridhika na matokeo/mapendekezo ya Tume, kikubwa ni kwamba wale hawakuwa majambazi. Akina Zombe na wenzake walitinga mahakamani na wa kulaumiwa baada ya pale haikuwa JK tena na Mhimili wake wa Utawala, bali ni Mahakama. JK alikuwa amejikosha.

  Sasa hivi kumetokea suala kama hilo -- hili la kupigwa kinyama kwa Dr Ulimboka na tayari polisi wamehusishwa. Haraka haraka polisi imeunda Tume yake -- ya mapolisi, na mara moja wanaharakati, wananchi mbali mbali wamepinga kwamba haitakuwa huru kwa sababu polisi ni mmoja wa watuhumiwa katika suala hilo.

  JK safari hii kakaa kimya, tulitarajia angeonyesha ujasiri kama ule wa 2006 na kuunda tume huru chini ya jaji wa Mahakama Kuu kulichunguza suala hili. Kwa nini anaogopa kufanya hivyo? Ujasiri wake umepotelea wapi?

  Bila shaka anatekeleza matakwa ya mafisadi waliomuingiza madarakani. Sipati jibu sahihi kuuelezea ukimya wake.

  Nawasilisha.
   
 2. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kwa hili la kupigwa kwa Dk.Ulimboka hawezi kuwa na ujasiri.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakubalina nawe 100%. Anajuwa kabisa kwamba serikali yake inahusika, na poengine yeye ndiye aliyewatuma kufanya hivyo.

  Lakini tumpe muda, labda ataunda tume huru.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu siyo jasiri 2006 alifanya vile kwa ajili ya kupenda misifa mwisho wake yakamtokea puani...watuhumiwa wote wakaachiwa huru kwa kuwa kesi ilipelelezwa kupumbafu ....hakuna kitu JK kawahi kufanya kwa umakini toka amekuwa rais wa nchi hii....na hakuna siku kawahi kuwa jasiri...na wala sio jasiri maana inafahamika kuwa yeye ni dhaifu
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hana ubavu kuunda tume huru katika sakata hili.
   
 6. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Polisi tayari wamehusishwa unafikiri yeye atasema nini wakati kazi ile polisi walifanya ilikutekeleza amri ya mkuu wao. Polisi niwatumwa tu katika sakata hili.
   
 7. mozes

  mozes Senior Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Baba Ritz kazdiwa sana anahemea mipira ICU.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sidhani kama JK ana moyo mbaya kiasi cha kuagiza mtu kuuawa ila watu wake wa chini wamefanya. unajua sasa hivi serikalini kila mtu anafanya analotaka. polisi wanaweza kua wamefanya hii kitu na bosi wao hajui
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Penye red. Na kama hajui, basi ndiyo aanze kuwatetea waovu?
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Therefore inathibitisha yeye ni dhaifu, kama vile yule mee wake.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mafisadi wamemwambie katu asirudie yote yale mema ya 2006. Sasa ni unyama tu kwa kwenda mbele!
   
 12. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  kuna hii falsafa ya uzee kwa maana ya umri kukutupa mkono, pengine yale maamuzi ya 2006 yalifanyika kwa vile alikuwa bado kijana ambaye damu ilimchemka kimapambano, sasa kazeeka, hawezi tena haya mambo ya kupambana na wahalifu wa haki za binadamu.
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Gesi ya soda hiyo sasa hivi katepeta watu wanamnywa kilainiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...........
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Aliingia madarakani kwa hila sana waliua,waliwaumiza sana watu wengi kupitia mtandao na magazeti Mungu hapendi inda ndio maana pamoja na kwamba wakristo kila jumapili kwenye liturgia tunamuombea kama kiongozi wetu mkuu kwa kutaja majina yake yote matatu lakini pepo lake la kishetani limekwama shingoni analo aachie ngazi nchi iwe salama
   
 15. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unanikumbusha kesi ya balozi wa itali aliyenunua jengo!
   
 16. m

  mamajack JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Zilikuwa nguvu za chai kumuonesha mkapa kwamba yeye yupo juu.
   
 17. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  LIWALO NA LIWE mnamsahau kwa nini ? Yeye ni kachero nammba moja ! Kwanza anatokea Sumbawanga kwa wachawi , na mwangalie alivyokaa kaa wauaji hao ni bahati huyu Dr Uli hajafa lakini bado wanawafanyia timing wengine
   
Loading...