Umekosea namba... Sawa! Sasa kwanini unalazimisha mapenzi na mtu usiyemjua?

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
19,732
10,057
Habari zenu wana jukwaa!?

Refer to the heading above!

Binafsi nachukizwa sana na watu hawa wanaojifanya kukosea namba halafu mwisho wa siku mtu anakutaka kimapenzi, tena si kwa staha, unakuta wengine ni by force!

Sielewi inakuaje mpaka haka katabia kanawatokea mpaka watoto wa kike! Yani binti analalamika kwenye simu mpaka huruma!

Sasa tatizo hapa ni kwamba, mtu sikujui na wewe hunijui, inakuwaje u-fall in love kiasi kwamba kama vile ulinifahamu kwa muda mrefu?

By the way, niwapongezeni ninyi ambao mmefanikisha kuwa na wapenzi kwa njia ya kukosea namba!
 
Mie bwana kuna jitu hivyo hivyo. Likawa limeniganda mpaka basi. Kama miaka 5 iliyopita nikiwa chuo. Mpaka nilikosa raha. Nikajua ni michezo ya chuo, kila nikijaribu kuchunguza wapi.

Siku ya siku akanitumia namba, nikapiga ile namba kumbe ya mchumba wake na alikuwa anamsubiri wapate dinner. Nikamwambia yote kwa uchungu.

Kumbe bwana walikuwa wafunge ndoa the following week...... bi dada akavunja uchumba.

That man swore angenitoa msukule.
Simjui but he really stressed me.
 
Duh!ukweli mtupu!huwezi amini hizi tabia hata kwa wadada zipo,kuna dada mmoja alikosea namba,baada ya hapo tukawa tunawasiliana,mara akaniuliza najishughulisha na nini,nikamjibu nafanyia benk,unaambiwa ananifanyia followup hadi kero,mara ananiandikia "usiku mwema bby",mara "una mchumba"n.k,sielewi hajishitukii hata distance coz yeye yupo Dar,alafu mimi nipo mkoani,yaani ni msumbufu huyu dada hadi kero,nashangaa hanijui simjui,lakini amefall as if ananijua.....
 
dah, pole sana dada!!

mpaka kufikia hatua hiyo, hakika ungeripoti abuse tu polisi wamshughlikie!
 
Duh!ukweli mtupu!huwezi amini hizi tabia hata kwa wadada zipo,kuna dada mmoja alikosea namba,baada ya hapo tukawa tunawasiliana,mara akaniuliza najishughulisha na nini,nikamjibu nafanyia benk,unaambiwa ananifanyia followup hadi kero,mara ananiandikia "usiku mwema bby",mara "una mchumba"n.k,sielewi hajishitukii hata distance coz yeye yupo Dar,alafu mimi nipo mkoani,yaani ni msumbufu huyu dada hadi kero,nashangaa hanijui simjui,lakini amefall as if ananijua.....

mabinti nao wako serious kweli!

mi pamoja na kuwa enzi hizo jobless sina chochote, lakini nililazimishwa kupenda,

mpaka nikatunza simcard kwa muda ili nimkatishe tamaa!!

yani hata usipojibu simu zake na sms kwa mwezi mzima, bado tu ana wewe!!
 
Wenzenu wanajaribu bahati zao mjue....

Mbona watu wanacheza kamari kwa kutumia pesa nyingi sana??

Ila kiboko yao huwa ni babu....anaishia kuwaunganisha na bibi awape ushauri nasaha...lol!!

Babu DC!!
 
hata mimi kuna mdada alikoseaga namba....yaani kwa ule ustaarabu wangu tu aliponibeep nikampigia nikamfahamisha kuwa amekosea namba...baada ya dk kadhaa akanibeep tena...nikaongea naye..si alitaka kunijua kidogo...mara eti akaanza kutuma msg za mapenzi...from no where at all... kama JINI vilee
 
Duh!ukweli mtupu!huwezi amini hizi tabia hata kwa wadada zipo,kuna dada mmoja alikosea namba,baada ya hapo tukawa tunawasiliana,mara akaniuliza najishughulisha na nini,nikamjibu nafanyia benk,unaambiwa ananifanyia followup hadi kero,mara ananiandikia "usiku mwema bby",mara "una mchumba"n.k,sielewi hajishitukii hata distance coz yeye yupo Dar,alafu mimi nipo mkoani,yaani ni msumbufu huyu dada hadi kero,nashangaa hanijui simjui,lakini amefall as if ananijua.....
hahaha,ishakua fasheni,sasa hivi tu tu kuna demu ametoka kuniambia usiku mwema,ameniganda leo mwezi sasa.kwanza yuko mbali then simjui kisha sauti lainiii.kha...!!
 
Wenzenu wanajaribu bahati zao mjue....

Mbona watu wanacheza kamari kwa kutumia pesa nyingi sana??

Ila kiboko yao huwa ni babu....anaishia kuwaunganisha na bibi awape ushauri nasaha...lol!!

Babu DC!!
mkuu sijapashika vizuri hapo..

suala la kujaribu bahati si angalau kwa mtu unaemjua?
 
hata mimi kuna mdada alikoseaga namba....yaani kwa ule ustaarabu wangu tu aliponibeep nikampigia nikamfahamisha kuwa amekosea namba...baada ya dk kadhaa akanibeep tena...nikaongea naye..si alitaka kunijua kidogo...mara eti akaanza kutuma msg za mapenzi...from no where at all... kama JINI vilee

hofu yangu ndio hiyo mkuu!

mambo ya kufanya mapenzi na popobawa, mmh!
 
hahaha,ishakua fasheni,sasa hivi tu tu kuna demu ametoka kuniambia usiku mwema,ameniganda leo mwezi sasa.kwanza yuko mbali then simjui kisha sauti lainiii.kha...!!

hahahaaa!! hiyo factor ndiyo huchangia wengi kutokataliwa!!

tatizo nyingine hazina reflection na maumbo yao!
 
Kuna jamaangu alipata mke kupitia hiyo hiyo wrong no. mtoto bomba na wanaenda mwaka wa 4 saiv kwenye ndoa yao, dah! yani ananfanya na mim nitamani kujaribu wrong no..
 
hahahaaa!! pole sana!

unataka kulalia mlango wazi bahati ya mwenzio?
 
Nna mshikaji wangu naye alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akamwambia wrong no kutokana na maelezo aliyokuwa anampa. Baadaye demu akapiga tena kutaka kufahamiana na jamaa wakaongea vizuri tu kumbe demu alikuwa mtoto wa mama sita enzi hizo sie tuko chuo. Sasa hivi wanafanya mipango ya harusi na demu alibadili na dini kabisa ili awe kama jamaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom