Umejifunza nini kwa tukio la Lowassa tuliyeelezwa kwa miaka karibu 8 nyuma kuja kuwa mgombea urais?

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
16,207
7,570
Hivi ikiwa kama wewe ni mwananchi wa kawaida na mpiga kura, ni jambo gani umejifunza kutokana na uchaguzi huu kwa tukio la Lowassa ambaye tulikuwa tukimfahamu kama fisadi mkubwa sana kwa muda mrefu tu lakini mwishoni kajakuishia kuwa mgombea urais?

Mimi binafsi nimejifunza kuwa wakati wananchi tuna hamu ya mabadiliko wenzetu pia wao wana hamu ya madaraka,hivyo pengine hawa wengine niwajuwao kama mafisadi leo yawezakuwa ni tofauti na nijuavyo.
 
Ni kati ya wagombea urais walioonesha udhaifu mkubwa katika kujieleza ( kwa muda mfupi) kuwah kutokea hapa nchini
 
nilivyojifunza ;angekuwa mfanyabiashara angefanikiwa sana kuliko Bakharesa kwa sababu ana uthubutu,haogopi kupata hasara.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Nimejifunza mambo matatu makubwa.

Mosi,WaTanzania wengi wameichoka CCM wanataka mabadiliko ingawa mfumo uliopo kuanzia tume ya uchaguzi na vyombo vya dola bado havijawa tayari kwa mabadiliko.

Mbili,Mgombea uRais wa UKAWA alikuwa dhaifu sana hasa eneo la kujieleza badala yake wapiga debe Sumaye,Kingunge,Mgeja na Msindai ndio waliochukua nafasi kubwa ya kuomba wapiga kura ridhaa ya kuingia Ikulu huku mhusika mkuu akishindwa kutawala jukwaa.

Tatu,UKAWA hawakuwa wamejiandaa vya kutosha kukabiliana na hila,ghilba na fitna za CCM na serekali yake.
 
You can say that again.....
UKAWA hata kuwapa chakula mawakala tu walishindwa
sasa wataweza wapi kuishinda CCM?
 
Nimejifunza kuwa ukimsingizia mtu bado ukwelui unabaki pale pale. Wanahci wameonekana kumpenda sana tu huku wakitaka kuwatoa mafisadi wa kweli.
 
Nimejifunza umuhimu wa kusikiliza ushauri wa mkewako...Mama Regina aliona mbali na akamshauri sana EL asihamie Chadema..lakini mkuu akatia shingo ngumu na mwishoe mkewake akaona hana jinsi bali kufuata maamuzi ya mume...ila matokeoyake wote tunayafahamu
 
nimejifunza huwezi kuingia ikulu kwa kuhonga mapesa lowasa alijitahidi kuhonga wajumbe wa nec,wenyeviti wa cc ,mkutano mkuu na hata kwenye kamati kuu alikuwa na watu wake pia nje ya system alihonga waandishi wa habari,viongozi wa dini,waendesha bodaboda,wanasiasa kama mbowe,wanavyuo hao ni kwa uchache na bado akashindwa kwenda ikului
 
Upinzani hawako serious kabisa na kushika dola. . . . .Hilo ndio somo nililodhihirishiwa kwa matendo yao
 
Mimi nimejifunza watanzania wameichoka sana CCM hadi yeyote yule akija kuwaambia tuitoe CCM wanamkubali

Walio wachache, tulio wengi tunaamini mabadiliko huanzia ndani mwako na ndiyo maana tukaanza kuwapangua akina Lowassa.
 
Lowasa hawezi kuongea na anaumwa,lakini wakawa wanafich(nilichojifunza)
 
Hivi ikiwa kama wewe ni mwananchi wa kawaida na mpiga kura, ni jambo gani umejifunza kutokana na uchaguzi huu kwa tukio la Lowassa ambaye tulikuwa tukimfahamu kama fisadi mkubwa sana kwa muda mrefu tu lakini mwishoni kajakuishia kuwa mgombea urais?

Mimi binafsi nimejifunza kuwa wakati wananchi tuna hamu ya mabadiliko wenzetu pia wao wana hamu ya madaraka,hivyo pengine hawa wengine niwajuwao kama mafisadi leo yawezakuwa ni tofauti na nijuavyo.

Mimi Nimejifunza Kuwa Binadamu Kwenda HAJA KUBWA Mara Kwa Mara Siyo DALILI Kama Labda Una Afya Sana au Umeshiba Mno Pengine Kutokana Na Utajiri Wako. Ni Hayo Tu Mkuu Kwa Upande Wangu Na Ngoja Niwapishe Na Wengine Waendelee Na Za Kwao!
 
Walio wachache, tulio wengi tunaamini mabadiliko huanzia ndani mwako na ndiyo maana tukaanza kuwapangua akina Lowassa.
Mabadiliko si lazima yaanzie ndani tu, hata from external inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko.
 
Mi nimejifunza kua Mbowe ni mwanadamu pekee Duniani, mwenye uwezo wa kusamehe na kusafisha dhambi.
Afu nimejifunza kua siku shetani akienda mbinguni, atakua Malaika kama zamani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom