Umejenga nyumba yako kwa muda mrefu kwanini uibomoe kwa muda mfupi?

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
19,011
11,942
Habari zenyu bana,

Watu wengine wanashangaza sana, unakuta limtu limehangaika Kwa
muda mrefu kuijenga nyumba yake kwa hali na mali,mwisho wa siku linakuja kukubali ibomoke kirahisi rahisi tu wendawazimu huu.

Mtu ulikuwa hohehahe wa kutupwa kama ganda la muwa liloisha utamu,wakati huo hakuna mtu aliyekuthamini hata mmoja zaidi ya mwenza wako unayeishi naye, ukirudi home anakuliwaza na kukupeti peti bila hiyana wala masharti.

Na unapoondoka asubuhi kwenda kwenye mihangaiko anakuombea na kukutakia kheri kwa mwenyezi Mungu, nawe unaondoka kwa bashasha na kujipa moyo kwa jinsi unavyothaminiwa na ze wife japo mifuko imetoboka,

Mtoto nae anatabasamu na kukupungia mkono wa baraka ili baba ukafanikiwe huko uendako,ili jioni umletee japo zawadi ya kitumbua pindi utakaporejea nyumbani, kama mjuavyo baraka za watoto ni muhimu mno ndani ya nyumba.

Mnalisongesha hivyo hivyo kimagumashi yaani mnaishi bora maisha na si maisha bora,hamkati tamaa na ze wife mnapeana moyo wa matumaini ya mafanikio kwamba siku si nyingi mtafanikiwa kimaisha na kuzifanya shida mlizopata kuwa historian.

Kama mjuavyo Mara nyingi mtu mwenyewe kiu ya mafanikio huwa hachoki,ni kukomaa tu kwa kwenda mbele Mungu saidia mambo yanaanza kunyooka, kwa machungu mliokuwa nayo na ze wife mnapanga kuto hama kwenye tembe mpaka mmalize njenge yenu.

Kila kitu ni malengo na mahesabu mnakomaa mpaka mnamaliza njenge,mnahamia kama waswahili wanavyosema umoja ni nguvu
na kweli kwa umoja wenu mambo yanakuwa mswano,siku zinajongea maisha murua mnanunua na kitu cha miguu minne watoto wanasoma shule nzuri.

Unaanza kuoga vizuri unapendeza na kina Delilah nao wanaanza kukuona kama nawewe ni mtu,na wako faster sana akikunasa tu hutoki maana ni mabingwa sana wa kutumia mabomu aka kuroga,na wewe kwa urimbukeni sijui ushamba unajitumbukiza mmzima mzima.

Kama mjuavyo ukinasika kwa nguvu ya ziada kujinasua huwa ni ngumu sana,na siku hizi hata vibinti vidogo ni vichawi sana vingi vinaamini sana nguvu za giza, Mzee mzima unaanzisha uhusiano wa siri na Delilah,Delilah naye bila kuzubaa anafanyia mambo taratibu katabia kanaanza kuchage.

Ulikuwa unafika home saa 11 na unaanza kucheza na watoto na kuwahoji habari za shule na kufanya nao homework,sasa unachelewa unarudi mida mibovu, ze wife akihoji unakuja juu na vijineno vya kijinga eti umenioa au nimekuoa?Watoto nao hawapati muda wa kukaa na wewe na kuenjoy,matumizi home yanapungua kwa kasi bila maelezo.

Ze wife anabaki kushangaa na asijue la kufanya maana huguswi wala kuambiwa, akiomba tendo eti unamwambia huwezi kushirikiana nae kwanza ni mchafu ananuka,umesahau kwamba huyo unayemuona mchafu kwa sasa ndio mmefika nae hapo ulipo,ada za watoto hulipi mpaka wanafukuzwa shule,Delilah ambaye hana mchango wowote kwako na kipindi huna kitu alikuwa anakuona kama mwehu,eti Leo hii ndio anayekula good time kuliko mtafutaji, huu ni wendawazimu

Yaani unaacha familia inateketea kwa ajili ya kitobo? Ebu kuwa na uchungu japo kidogo hicho kitobo ukichacha kitageuka na kuwa adui yako mkubwa, ebu kuweni makini basi msikubali nyumba zenu zibomoke kirahisi namna hiyo, ukishapata pata mafanikio tu jua ya kwamba,una maadui kila kona jambazi anakuwinda ili akuibie, kina Delilah wanakuwinda ili wakunase,wanafiki wanatamani uporomoke uwe omba omba.Tumwombe Mungu atusaidie kuwaepusha wabaya wetu ili nyumba zetu zisibomoke kirahisi Amina.
 
sipendi maoni yanayomjenga mwnamke wakukaa nyumbani tu na kusubiri mume arudi! hivi kwa nini msiansike vitu vinavyoendana na wakati? ni kweli mifano uliyotoa ni hai kwa asilimia kubwa leo hii wanawake wako nyumbani tuu? hiyo inafaa miaka ya 80 japo nia yako ilikuwa njema
 
Mfano huo haujalenga wanawake wanaokaa nyumbani tu Bali ni kurekebisha Tabia za watu wa aina hiyo,Kwa sababu hayo mambo yanawatokea watu wa a in a zote,kwenye kazi na wasio na kazi
 
Pia na wadada sis tuwe na huruma unapoona unatembea na Mume wa mtu tambua walitoka mbali na mke wake heshima iwepo. Mchepuko wenye akili haupendi mtu alale nje na wala amsumbue mke wake maana kilio cha mwanamke yule na watoto wale kiko juu yake. Every man cheat but if he love he will never let me know.
 
Ni wachache sana kwenye huruma wengi wao wanaroho mbaya sana
 
Pia na wadada sis tuwe na huruma unapoona unatembea na Mume wa mtu tambua walitoka mbali na mke wake heshima iwepo. Mchepuko wenye akili haupendi mtu alale nje na wala amsumbue mke wake maana kilio cha mwanamke yule na watoto wale kiko juu yake. Every man cheat but if he love he will never let me know.
Eeh kumbe kuwa mchepuko ni akili? Aanze kukuonea huruma mumeo kwanza kabla ya mchepuko.

Wanawake tumejikatia tamaa jamani, eti if he loves me acheat bila me kujua, hivi kuna definition mpya ya love au mimi ni old school? Siku hizi what you don't know; cannot only kill you, but can also burry you alive.
 
Back
Top Bottom