Umeiskia hii ya wanaume watu wazima......

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,710
..... eti wanasema wanahitaji mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi..... hili mnalionaje wadau kwanini wanaume wengi wanapenda kuzaa watoto wengi.... mimi kwa kweli ni kijana bado sina mtoto bado nna ka elimu kadogo lakini namimi natamani sana mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi, mambo ya uzungu mi kwangu hayana nafasi hata kitogo " suala la mtoto mmoja tu au wawili tu, ntakuacha"....... ONYO: ILA UWEZO WA KUWALEA UWEPO
 
Hata mimi natamani kuwa na watoto kama nane hivi, just like my grandpa..
 
avatar179011_2.gif

JAMAA wewe zaa tu km mambo yenyewe ni kila mtoto atakuja na bahati yake haya weee
ndio km ilivyo katika picha ya avartar hapo juu mwanamume kuvaa sketi ya ngozi ya nguchiro mwaka mzima

  • Mtoto anataka malezi, na vyakula ili asipatwe na kwashiakor miezi 6 hadi 10 awe angalau na 10kg chakula yake sasa.
  • miaka 2.5 asome chekechea English Medium ada ya chini 350,000/= mpaka 800,000/ hapo usafiri wa kwenda na kurudi @ siku bado
  • Primary angalau ajue KKK sio mpaka anafika Sekondari (Kusoma, Kuhesabu na Kuandika) hajui
Huyo ni mtoto mmoja sasa kuna member anataka 8 bado Mama hajavaa
Kwanini wasikudunde wakikua au wawe wabeba Sembe km sio kukuibia?
Punguza idadi ya wototo, sio lazima kila shaft ikidai uzae nenda na Mpango wa Uzazi (mama ataelezewa Klinik)
 
Kwani wewe muha?

Sie waha tunatekeleza maagizo ya Mungu ya kuzaa ili tuijaze dunia ama nyie msiokuwa waha mnatekeleza zaidi ya shetani kwa kufanya zaidi vitendo vya kuuwa watoto kwa kisingizio cha kupanga uzazi na matokeo yake mnazaa mtoto ima mmoja au wawili.
 
..... eti wanasema wanahitaji mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi..... hili mnalionaje wadau kwanini wanaume wengi wanapenda kuzaa watoto wengi.... mimi kwa kweli ni kijana bado sina mtoto bado nna ka elimu kadogo lakini namimi natamani sana mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi, mambo ya uzungu mi kwangu hayana nafasi hata kitogo " suala la mtoto mmoja tu au wawili tu, ntakuacha"....... ONYO: ILA UWEZO WA KUWALEA UWEPO

Suala la watoto ni mipango ya MUNGU! ila itapendeza kama ukiwa na watoto hata mia mbili lakini unawalea vizuri na hawakosi wanachokitaka, muhimu ukiwa na mtazamo wa kuwa na familia kubwa kama uzaniavyo jikite zaidi maeneo ya vijijini, uwe na mashamba ya kutosha na uwe mkulima na mfugaji wa kisasa, watoto wako hawatalala njaa kamwe na kusoma watasoma na hapo utajiri utauona maana familia itakufanya ufanye kazi kwa bidii. kamwe usiwe na mawazo ya kukaa mijini utawatesa hao watoto na mama yao. nakutakia uzazi mwema ndugu.
 
Kila mtu anao uhuru wa kuamua idadi ya watoto aipendayo, hata ukitaka kuwa na watoto kumi ni wewe tu na jukumu la kuwalea. Binafsi sababu kubwa ya kuzaa ni ili watoto wangu warithi mali zangu na kuziendeleza pindi nikitangulia mbele za haki, idadi ya watoto itategemea na mali nilizonazo.
 
Jaribu kuutafakari huu msemo wa waswahili "kulea mimba si tabu..tabu kulea mwana"

Nadhani watu wengi wanapenda kuwa na watoto wengi lakini mazingira yetu na hali ya maisha ya sasa ni tofauti ndiyo maana ibabidi mtu azae watoto wachache...

Ukiangalia zamani maswala kama ya elimu..chakula..mavazi..hata kusaidiana ilikuwa rahisi kuliko sasa....

Kwa hiyo bwana ukitaka kuwa na watoto wengi ujipange haswa..
 
I thnk most men say wanataka watt wengi cz sio wabebaji mimba ,sio wazaa kwa uchungu au operation na sio waleaji wakubwa wa watoto physically,wange'experience hvo vtu tungeenda nao sawa,wengi ni watoaji wa monetary na emotional support na wengine ukipata hyo mimba utawasikia kwny bomba,kuwa na watt wengi kama uwezo wa kulea unao
 
Kuna jirani yangu ana watoto 8. Shule zikifunguliwa ni lazima agonge kuomba mkopo, ambao hata hivyo hajawahi kilipa yote.

Watoto wawili au wa 3 wanatosha sana.
 
nani alikwambia muha anapenda kuzaaa watoto wengi ? muulize mpare anayetaka kueneza majina ya ukoo , maana unakuta mpare anakwambia mimi nimemzaa mjomba , baba , shangazi n.k

Uvugizi nyokou zako..!
 
Hapana kwa kweli...bado sijasahau mziki wa labour...
Maji ya moto mwezi mzima.....
Sleepless nights.........
Unakuta kitoto kibishi kula..ukifika wakati wa kulisha unawaza mbinu mpya ya siku...
Hapo hajaanza shule....
Kumbuka enzi za bibi yako walikuwa wanaanza darasa la kwanza moja kwa moja tena na miaka tisa kwa ada ya shilingi 20 sijui...
Siku hizi wanaanza baby class na miaka miwili na nusu mpaka 3...ada yake....utaisoma namba.....
 
Back
Top Bottom