Umeipata hiyo? Sumbawanga jamani ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeipata hiyo? Sumbawanga jamani !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkyandwale, Feb 14, 2011.

 1. nkyandwale

  nkyandwale Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Vyombo vya habari vimeripoti kwa nyakati tofauti juu ya wanafunzi kuanguka na kuzimiya katika baadhi ya shule za hapa nchini Tanzania, kwasababu ya kuweweseka na kuanguka kutokana na imani za kudaiwa kuwa Wanafunzi hawo wana mashetani, matukiyo hayo yakihusishwa na mtazamo wa kishirikina na uchawi.

  Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule x katika Manispaa ya Sumbawanga, kabla ya pumziko dogo la saa nne Jumatatu ya leo Asubuhi, aliwaambiya wanafunzi anaokaa nawo katika dawati moja, kuwa analala kidogo, na endapo hataamka mpaka kengele ya pumziko wamvue sweta na kumfunga kiunoni.

  Mwanafunzi huyo wa kike akalala, saa ya pumziko ilipowadiya wale wanafunzi wenzake walishangazwa kumwona mwenzawo amelegeya na akiwa katika hali ya kuzumiya jambo ambalo liliwatiya hofu, hivyo walimbeba na kumpeleka ofisiya Walimu akisindikizwa na kundi la wana darasa.

  Baada ya robo saa, mwanafunzi aliyezimia, alizinduka na kusema kuwa alikuwa anashuhudiya mashindano ya mpira wa miguu kati ya wanaume na wanawake timu za mtaani kwao na
  amerudishwa kwa ndege ili aendelee na masomo.

  upo?
   
Loading...