Umeicheki IRIS? Hizi ni facts 10 usizozijua kuhusu series hiyo

Kiukweli IRIS 1&2 ni 'konyoo',,, ni moja series bora kuwahi kuziona

Maudhui kwa ujumla ya ile series ni kuonesha namna gani South Korea na North haziwezi kuja kuwa kitu kimoja kwasababu kila mara viongozi wa hayo mataifa wakijaribu kukaa meza moja kutafuta muafaka inashindikana kutokana na kikundi hatari cha IRIS chenye nguvu na ushawishi ndani na nje ya nchi zao kinavyohujumu mipango na mikakati yao

Kikundi hiki cha IRIS ambacho kimeundwa na watu wenye pesa kimejaa watu waliobobea kwneye ujasusi, mapigano nk kinawapa upinzani mkubwa sana idara za usalama wa Taifa wa mataifa haya mawili

Hio sio series ya kukosa hata kidogo
 
Dah nmeichek vipande kadhaa tu nikijua nitapata nzima muda wwte ila sijafanikiwa, naweza kupata wapi hii seriese pamoja na zingine za kikorea???
 
Kuna ile scene wanavamia mall magaidi naona magaidi wa Kenya walicopy walipovamia Westgate mall.Ni series moja Matata sana
 
huyu mwamba alikuwa ananifurahisha,ila jinsi alivyokamatwa mpaka nikashangaa,yale yale ya adui kufia nyuma ya nyumba.
images.jpg
 
Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa kdrama hii drama sijawahi kuiangalia. Sababu kuu iliyofanya nisiangalie ni haya masimulizi ya watu yanayoelezea iliishaje. Mimi nikishaambiwa tu kuwa drama inaishaje huwa hamu ya kuangalia inaisha kabisa....ya nini nipoteze muda na mb zangu wakati najua kabisa mwisho wake? Labda nikute inarushwa kwenye kituo cha televisheni
 
Jumong ilipelejea kuangalia hizi series za kikorea, tokea hapo nimeangalia series na drama nyingi sana za kikorea mpaka zingine nimezisahau.

1. City Hunter
2. Iris 1&2
3. Athena
4. Six dragon fry
5. Dong Yi
Love story in Harvard
 
Mara ya kwanza kucheki Korea series ilikuwa Athena,sikudhani kama kutakuwa na series kali kama hiyo.

Ila huo mzigo wa Iris ni ilikuwa ni shida nyingine,kuanzia sterling hadi adui wana balaa.Mzee baba Baek San,Kim Sun Hwa,Jin Sa Woo,Choi Seung Hee na yule Dr kichaa wa kule NSS bado kule North Korea na Security Service yao na yule boss wao,mtaalam wa machare kama yote vile.

Love story kali,action kali,matumizi ya akili makubwa mno. Huwezi kupredict kinachofuata.

Nilikuwaga naangalia na sister angu home,kuna kipindi alikuwa analia sana jinsi Kim Hyun Jan alivyokuwa anateseka na maisha yake ya kusalitiwa.

Sema wazee mapenzi ni matamu sana na yana nguvu mno. Ila vipi TISS wetu sijui wapo kama vile kwenye recruitment hadi kufanya kazi. Na IRIS wa nchi yetu sijui ni wakina nani.

Kwa nini na sisi tusiandike movie kali kama ile moja tu.Kila siku tuna deal na mapenzi tu. At least vipepeo weusi The Bold alitupa utamu kunoga.

IRIS itabaki kuwa IRIS tu,ila Athena na yenyewe ni shida nyingine wazee.
Inji hii bhana inakataza kufanya maigizo yoyote yawe ya luninga au sauti yanayoendana na majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. Kufanya ivo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya usalama wa Taifa nimesahau ni sheria namba ngapi na ya mwaka gani. Kuangalia bongo muvi heri waninyonge. Licha ya vikwazo vya technolojia wanayotuma watu wa hongo muvi lakin bado sheria za nchi zinawabana sana hata kufanya ubunifu walau kulingana na mazingira yaliopo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom