"Umefanana Nae", Song story kutoka kwa Belle 9 na kwa mwaka 2020

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
12,702
2,000
Story inaanza belle 9 katendwa na mpenzi wake aliyekuwa anampenda kiasi cha kutamani kufa pamoja nae,

Sasa wakati anaugulia maumivu ya kutendwa tena kutendwa kwenyewe katendwa kwa kusalitiwa na jamaa ambae hamfikii ata Robo kuanzia uzuri, capital na Nk. Lakini demu wake akamsaliti kwa kitu kidogo tu unakijua ni kitu gani hicho?

Basi bwana belle 9 akiwa katikati ya maumivu makubwa yasiyopona, mawazo ya kumbukumbu za demu wake aliyopita.

Ghafla akatokea mrembo, mtoto mzuri malkia ambae lengo lake lilikuwa ni moja tu Kumfuta machozi, kumsahaulisha shida na yale yote yaliyopita.

Mtoto alikuwa ni mkali aswaa, licha ya uzuri wake mtoto alitokea kumpenda belle 9 aswaa ile kiukweli ukweli na kuamua kuvunja ukimya kwa kumuelezea hisia zake vile moyo wake unavyofeel, hisia na kwa kiasi gani anatamani kuwa naye.

Tofauti na alivyodhani kwamba kwa kuwa kamkuta ndugu belle 9 yuko single na maumivu ya kusalitiwa basi itakuwa rahisi kwake kukubaliwa na kupewa nafasi.

Kinyume chake ikawa bwana belle 9 kumkataa na sababu ya kukataliwa kwake unajua ni nini licha ya uzuri wake, tabia njema na Nk.?"Ni kwa sababu tu Amefenana nae.

Unajua amefanana na yupi ni Ex wa Belle 9.

Hivyo belle 9 anaogopa kumpa moyo wake kwa sababu kila akimuona anakumbuka yale aliyofanyiwa na Ex wake.

Mzigo huo Umefanana nae kwangu ndio nyimbo bora kabisa ya mwaka uliopita 2020 ya story kutoka kwa belle 9, kuanzia uandishi, melody beat na nk ni konyo yaani ni balaaaa.
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,499
2,000
Wimbo mkali sana huu. Pale mwanzo zinaanza gitaa fulani kama rock vile. Belle anajua sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom