Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,105
- 2,499
Mimi niliipata jamiiforum kupitia kugoogle huko, sehemu ya kwanza kabisa kuingia ilikuwa ni jukwaa la Jamii Photos, hapo ndo ikawa mwanzo!
Acheni utani, JF imekuwa ya msaada sana kwangu.
Nakumbuka zilikuwa zimebaki siku chache sana nifunge ndoa. Bestman wangu akawa haeleweki. Nikiwasiliana naye kuhusu mipango ya kwenda kufanya manunuzi (tena kwa ghalama zangu) ananikwepa. Nilipomkumbusha siku ya kwenda rehearsal na kubaini hatuko ukurasa mmoja nikachanganyikiwa. Haraka sana nikamkumbuka mtu mmoja aliyewahi kuniomba mchango wa harusi kwa PM hapa JF. Huyu mtu japo nilimchangia, hatukuwa tumewahi kukutana na wala hatukuwa tunajuana. Roho ikanituma kuwasiliana naye. Jibu lilikuwa, USIPATE SHIDA. Hivyo ndivyo ilivyokuwa JF ikawa imenipa Bestman and Best-friend. Asante sana JF, Udumu Milele
Ninapoteza muda kujadiliana na ghost names hapa! Sijawahi onana na MjF hata mmoja...ngoja nisepe
Ninapoteza muda kujadiliana na ghost names hapa! Sijawahi onana na MjF hata mmoja...ngoja nisepe
Rev. kwa heshima na taadhima ningependa kuonana na wewe nipate upako..mambo yangu hayaendi kabisa!!
Ukiona hivyo uko sehemu ambayo haifikiki kirahisi.
Huenda mwenzetu uko Mars
Ninapoteza muda kujadiliana na ghost names hapa! Sijawahi onana na MjF hata mmoja...ngoja nisepe
Usisepe Rev bado mchango wako unahitajika
Hahahah kwanini usifikiri Loliondo ama Keta Keta?