Umeelewaje tangazo hili!

wanapaka rangi za gari, nyumba, za kucha n.k kwa wakati mmoja, ila hata mimi sijaelewa kitu gani kinapakwa hizo rangi zote
 
hilo tangazo limekosea, hauwezi kuelewa kwa maneno hayo ila walikuwa wanamaanisha:-

hapo walipo kuna ofisi ambayo wanajishughulisha kupanga rangi, katika eneo unalotaka, ila wamekosea hawajaeleza rangi gani ya nyumba au gari kwa sababu huwezi ukawa na biashara ya kupaka rangi za nyumba, magari, kucha, mwili, etc

ila kiswahili kazi kweli kweli jap ni lugha yetu
 
Ebwana hii ngumu kwa kweli,hasa ukimaanisha paka mnyama.
 
Umenikumbusha somo la Kiswahili. Hiyo ni Tungo Tata, ina majibu tofauti tofauti kutokana na mahitaji yako.
 
TUNAPAKA RANGI ZOTE
Hii sentensi inamaana nyingi
  1. wana Paka(wanyama) wa rangi zote ie blue, nyeusi, njano nk
  2. wanapaka rangi za aina zote.. ie ukitaka tupake blue. njano, nyeupe nk tunapaka
  3. wanapaka rangi sehem zozote ukitaka rangi ya kucha, rangi ya nyumba, rangi ya gari wanapaka
eeh mpaka kichwa kitauma kwa kufikiria...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom