Uchaguzi 2020 Umeanguka umeanguka wee CCM, tokeni kwake enyi Watanzania

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
921
1,000
Miaka mitano ya CCM imejaa vilio kwa Watanzania kila Kona ya nchi, iwe ni kwa mwana CCM mwenyewe au hata asiye mwana CCM. Unamtumia muda mwingi kuhubiri flyover, SGR, ndege, Mabwawa ya umeme, meli. Nk

Jambo ambalo CCM wanapaswa kujua kuwa hayo mnayo ya hubiri mna wahubiria Wananchi wenye njaa. Unamhubiria mtu wa Kusini tena kule Nakapanya habari ya flyover imsaidie nini. Una mhubiria mtu wa Tarime kule Nyangoto habari ya ndege ili imsaidie nini.

CCM imekata pumzi au mgombea wao hajui ni wapi aseme hili na ni wapi aseme lile. Toka ameanza kampeni yeye ujenzi tu amesahau kuwa hao watu anaowazungumzia habari hizo ndio hao hao aliwabomolea nyumba zao tena bila hata ya fidia yoyote.

Katika hotuba zake hakuna hata mahali anapo zungumzia jinsi ya kuwainua Wananchi kiuchumi ambao kwa hakika ni yeye aliye uvuruga.

Ajira hakuna , biashara zimekufa, wananchi wamebaki kuhuzunika tu. Eti bila Aya muuza mchicha anunue kitambulisho cha biashara shilingi elfu ishirini? Kweli?

Mabaya ya CCM ni mengi watanzania wengi wamepoteza lakini serikali ya CCM iko kimya Wala hazungumzii kabisa utadhani hakuna yaliyo tokea ktk jamii.

Ni mtanzania gani mwenye akili ataendelea kuwavumilia watu wa namna hii. Ni mtanzania gani ataamka asubuhi na mapema kwenda kuwapa kura watu wa Aina hii.

Ni mtanzania gani anatamani kuyarudia maumivu makali aliyo yapitia kwa hii miaka mitano. ? Ni Bora kuipatia CCM mkono wa buriani iende na isirudi tena, kwani badala ya kuwa baraka kwa wananchi yenyewe imekuwa laana kwao.

Na ndio maana wito unatolewa CCM umeanguka watanzania tokeni kwake. Viongozi wake wamelewa mvinyo wa madaraka walio pewa kwa hii miaka mitano.
 

issa yurry

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
627
1,000
Kitu kimoja kiko wazi, CCM imeshaanguka. Swali kubwa Je watakubali kukabidhi mamlaka/nchi kwa watanzania?
Hawako tayari kukabidhi kwa kura lakini tukiamua kama Malawi walivo amua watakabidhi hamna jinsi watatua wangapi
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,415
2,000
Upinzani ulishajifia tangu 2015, kilichopo kwa Sasa ni futuhi.Miaka inayokuja wanatakiwa wapambane na CCM wakiwa wamejiunga na kuwa kitu kimoja. CCM haiwezi kuangushwa bila upinzani kuunganisha nguvu na hoja zenye mashiko.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
14,438
2,000
mcoloo,
Anaenda Busega kutangaza Ndege na Flyeover, huko watz hawana mpngo wa kupanda ndege wala hiyo flyover sio tu hawajawahi kuiona lakini pia hata picha tu kwenye akili zao haimo. Unanadi vipi sera kama hizi utegemee matarajio mazuri?? Mwisho wa siku watu wazima wanakidharau unabaki unakusanya watoto wa nursery
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,121
2,000
Magufuli ndiye mgombea pekee Tanzania aliyekosa Sera ukiangalia kwenye mikutano yake ni kunadi barabara Tu hata Yale yaliyomo Kwenye ilani yao hazungumzi...
Magu amekata moto kama betri mbovu
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
14,438
2,000
Upinzani ulishajifia tangu 2015, kilichopo kwa Sasa ni futuhi.Miaka inayokuja wanatakiwa wapambane na CCM wakiwa wamejiunga na kuwa kitu kimoja. CCM haiwezi kuangushwa bila upinzani kuunganisha nguvu na hoja zenye mashiko.
Matumaini hewa. Kamuulize Magufuli ametumia 2.4Trilion ku organize resources zote ili tu Chadema ianguke lakini mpaka sasa anahenya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom