Umaskini wetu unasababishwa na wale tunaowaona wakombozi wetu eti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaskini wetu unasababishwa na wale tunaowaona wakombozi wetu eti!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dijovisonjn, Mar 13, 2012.

 1. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tanzania sio maskini ila watanzania ni maskini! Watanzania ni maskini 100% kwa sababu ni wavivu wa kuwaza, watanzania wengi tumewapa viongozi wetu jukumu la kuwaza kwa niaba yetu, tunayaamini mawazo/fikraza viongozi wetu kuliko tunavyoziamini fikra zetu wenyewe!
  Hebu angalia mawazo yetu ya kila siku yalivyo jaman kila siku wale wa CCM wanawaza madongo ya kuwapiga CHADEMA na CHADEMA wao wapo bize kuonesha uozo wa CCM huku CUF wao wakijitahidi kutuonesha kuwa wao sio CCM B hakuna hata mmoja anayekuja na wazo la kumkomboa mtanzania jaman.
  Natambua kuwa lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dolana kile kilicho na dola kuendeleakuishikilia!
  Lakin je hiyo dola na umaskini huu jaman si kila siku itakuwa ni maandamano na migomo?
  "....... nitatengeneza nafasi za ajira 100,000 ....." aliyeniahidi hizi nafasi za ajira alinidanganya ni muongo, kwa sababu ya uongo wake na uvivuwangu wa kufikiri alinifanya nisiangaishe ubongo wangu kwani nlimwamini sana mwisho wake hizo ajira sijaziona na umaskini wangu ukaongezeka, Mungu wangu huyu mtu sio mwema kwangu na laiti ningejua uongo wake toka mwanzo nisingekuwa maskini hivi!
  " ...... CCM ni waongo mwaka 2005 waliwaahidi kutengeneza ajira 100,000 ajira zilizoongezeka ni zile za kuokota makopo ya maji, kuuza maji na kusukuma mikokoteni....." wote waliotoa kauli hii woteni wanafiki, waliitoa ili kujenga chuki baina yangu na yule aliyeniahidi kunipa ajira 100,000 lakini hawakunipa njia sahihi za kujikomboa na umaskini badala yake waliniongezea chuki tu, wote hawa wanafiki tu hata hawafai!
  Jaman kwa hali hii kweli tunaweza kuendelea?
  Wazo langu:- kama vile serikali ilivyoanzisha Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) napendekeza pia ianzishe Bodi ya mikopo kwa vijana.
  Bodi hii ya mikopo kwa vijana ishugulike na kuwawezesha vijana kama HESLB inavyowawezesha wanafunzi.
  Mfano hii Bodi ya mikopo kwa vijana kwa kuanzia itoe mikopo kwa wale vijana wote wa kimaskini wenye degree lakini hawana ajira. Kivipi? Kwa mfanokiwango cha juu 100% cha mkopo kikiwa bilioni 1 kwa mtummoja basi itengwe sekta maalumu mfano kilimo na kusema kwamba ili mtu apate 100% kwanza anatakiwa awekeze kwenye kilimo, pia awekeze kwenye mikoa fulani iliyo nyuma kimaendeleo na pia mradi wake uwe na uwezo wa kuajiri si chini ya vijana 25. Na hizo pesa zitolewe kwa awamu nne kama HESLB wanavyotoa napesa za awamu inayofuata zisitolewe kama awamu ya nyuma haijakamilika na kukaguliwa.
  Usimamizi sahihi na wa kizalendo ndo utahitajika hapa ili watoto wa vigogo wasifaidike na hii bodi.
  Ndungu zangu hili ni wazo langu, nimejaribu kulielezea kwa kifupi sana lakini nikipewa nafasi ya kulielezea kwa urefu naweza, lengo langu ni kutaka kukushawishi wewe kijana mwenzangu uliyepo chuo kikuukama mimi au uliyemaliza na ukakosa ajira uache kuwatengemea hao unaodhani ni wakombozi wako kwa sababu ndio wanaokuongezea umaskini hebu jaribu kufikiria namna ya kuwaza kujikomboa na kuishauri serikali namna ya kukuinua.
   
 2. Queen Kyusa

  Queen Kyusa JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona hakuna wachangiaji?
   
 3. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni kwa sababu hii haijakaa kiccm, kichadema wala kicuf
   
Loading...