Umaskini Wetu ni Matokeo ya Undumakuwili Wetu!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Watanzania kamwe hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili !!
Ndiyo! Huwezi kuutumikia mfumo wa demokrasi ya vyama vingi na wakati huo huo ukawa mwaminifu kwa mfumo wa chama kimoja!
Ni ama tushikamane na demokrasia kweli kweli au tuurejee na kuuboresha ujamaa na kujitegemea chini ya chama kimoja cha siasa, kiwe ni CCM au TANU ni sawa.
Vinginevyo tutakuwa viroja hasa pale tunapoushangaa mrejesho hasi wa undumakuwili wetu!

Hakuna asiyejua kuwa wenzetu wengi tuliolingana nao kiuchumi miaka ya sitini hasa wale wa mashariki ya mbali na Asia; kwa sasa uchumi wao ni gumzo duniani, pamoja na kwamba wengine hawana kabisa maliasili.
Wenzetu hawa wengi wao ama wameng'ang'ania kwenye ujamaa unaotukuza siasa za chama kimoja au walibadilika na kukumbatia ubepari unautukuza demokrasia ya vyama vingi.
Hawa jamaa hawakubaki kati kama sisi leo! bali wao waliamua kusuka ama kunyoa.
Waliamua kukataa ama kukubali.
Na leo hii wanaona matunda ya uamuzi wao, na kutuacha sisi tukiwa hatusomeki kisiasa wala kiuchumi huku tukivuna kile tulichokipanda!
Kwa mwelewa yeyote haiingii akilini kwa nchi kama Kenya kuwa na uchumi mkubwa kuliko Tanzania, na bado hili likaonekana ni jambo la kawaida kwa madereva wa siasa zetu!

Maskini Tanzania! Ni lini waheshimiwa wako wataukubali ukweli japo mchungu kuwa wamekuwa wakikupa matibabu yasiyoulenga ugonjwa wako?

Jamani kwani ugonjwa unalolisumbua taifa hili hatuujui?

Tukatae au tukubali shida yetu ni moja tu! Ambayo ni hii,

"Kwa makusudi yaliyoazimiwa kabisa katiba iliyopo imewapoka uwezo wananchi wa kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani, hata kama wakitaka kufanya hivyo.
Kwa mtu mwelewa hili ni jambo kubwa na muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yoyote ile".

Nitafafanua kidogo hapa,
Yaani chama kinachotawala wakati wowowte ule hakiwezi kikawajibika ipasavyo iwapo hakina hofu kuondolewa na wananchi pindi kitakaposhindwa kutimiza matakwa yao ilihali chama hicho hakina ujanjaujanja mwingine wa kukiokoa.

Hii ni kusema kwamba ifike mahali vyama vya siasa viwahofu mabosi wao wananchi, hapo ndipo tutakapoona maendeleo ya kweli yanayojipigia debe yenyewe.
Na waliopo madarakani wawepo kwa uwajibikaji wao tu na si vinginevyo.

Ndiyo maana Mimi nitakuwa mtu wa mwisho, kuamini kuwa; mfumo huu tulionao sasa unaweza kuleta mabadiliko hata kama viongozi wake wangelikuwa wale wa Ukawa, nasema tena, hili haliwezekani. Kujaribu kuubeza ukweli huu kwa sababu ya maslahi binafsi hakufanyi kutimia kwa ndoto zetu za shibe tunazoziota miaka nenda miaka rudi.

Laiti siku moja Mwenyezi Mungu angelitupatia kiongozi mzalendo kuliko Julius Nyerere, mnyenyekevu kuliko Rashid Kawawa!
MTU wa watu kwa ajili ya watu, ambaye yuko tayali kuweka misingi ya taifa hili hata kama ni kwa gharama ya kupoteza cheo chake kwa sababu ya maslahi ya wengi.
Yule aliye tayari kwenda nje ya maslahi ya chama chake kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa lake!

Huyu ndiye mtu yule taifa linayemsubiri kwa hamu ili aipitishe rasimu ya Jaji Warioba. Ile ambayo inamrudishia mwananchi wa kawaida meno ya kuiwajibisha serikali mpaka mbunge.

Naam ni huyu atakayetutoa katika undumakuwili unaotuchelewesha kimaendeleo atupeleke hadi katika msimamo thabiti wa kisera na kimaendeleo.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.
 
Machokoo, huu ni ukweli ambao kwa kujua kabisa hatupendi kuusikia ilhali unatuumiza.

Wanao faida na mfumo huu mbovu tulio nao sasa ni wachache sana tena kwa manufaa ya chama na mduara wa kifamilia.
 
Katiba mpya ipatatikane ambayo itawawajibisha viongozi na watu fulanifulani wenye maslahi yao.

Bila hivyo tutakuwa tunajidanganya.
 
Watanzania kamwe hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili !!
Ndiyo! Huwezi kuutumikia mfumo wa demokrasi ya vyama vingi na wakati huo huo ukawa mwaminifu kwa mfumo wa chama kimoja!
Ni ama tushikamane na demokrasia kweli kweli au tuurejee na kuuboresha ujamaa na kujitegemea chini ya chama kimoja cha siasa, kiwe ni CCM au TANU ni sawa.
Vinginevyo tutakuwa viroja hasa pale tunapoushangaa mrejesho hasi wa undumakuwili wetu!

Hakuna asiyejua kuwa wenzetu wengi tuliolingana nao kiuchumi miaka ya sitini hasa wale wa mashariki ya mbali na Asia; kwa sasa uchumi wao ni gumzo duniani, pamoja na kwamba wengine hawana kabisa maliasili.
Wenzetu hawa wengi wao ama wameng'ang'ania kwenye ujamaa unaotukuza siasa za chama kimoja au walibadilika na kukumbatia ubepari unautukuza demokrasia ya vyama vingi.
Hawa jamaa hawakubaki kati kama sisi leo! bali wao waliamua kusuka ama kunyoa.
Waliamua kukataa ama kukubali.
Na leo hii wanaona matunda ya uamuzi wao, na kutuacha sisi tukiwa hatusomeki kisiasa wala kiuchumi huku tukivuna kile tulichokipanda!
Kwa mwelewa yeyote haiingii akilini kwa nchi kama Kenya kuwa na uchumi mkubwa kuliko Tanzania, na bado hili likaonekana ni jambo la kawaida kwa madereva wa siasa zetu!

Maskini Tanzania! Ni lini waheshimiwa wako wataukubali ukweli japo mchungu kuwa wamekuwa wakikupa matibabu yasiyoulenga ugonjwa wako?

Jamani kwani ugonjwa unalolisumbua taifa hili hatuujui?

Tukatae au tukubali shida yetu ni moja tu! Ambayo ni hii,

"Kwa makusudi yaliyoazimiwa kabisa katiba iliyopo imewapoka uwezo wananchi wa kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani, hata kama wakitaka kufanya hivyo.
Kwa mtu mwelewa hili ni jambo kubwa na muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yoyote ile".

Nitafafanua kidogo hapa,
Yaani chama kinachotawala wakati wowowte ule hakiwezi kikawajibika ipasavyo iwapo hakina hofu kuondolewa na wananchi pindi kitakaposhindwa kutimiza matakwa yao ilihali chama hicho hakina ujanjaujanja mwingine wa kukiokoa.

Hii ni kusema kwamba ifike mahali vyama vya siasa viwahofu mabosi wao wananchi, hapo ndipo tutakapoona maendeleo ya kweli yanayojipigia debe yenyewe.
Na waliopo madarakani wawepo kwa uwajibikaji wao tu na si vinginevyo.

Ndiyo maana Mimi nitakuwa mtu wa mwisho, kuamini kuwa; mfumo huu tulionao sasa unaweza kuleta mabadiliko hata kama viongozi wake wangelikuwa wale wa Ukawa, nasema tena, hili haliwezekani. Kujaribu kuubeza ukweli huu kwa sababu ya maslahi binafsi hakufanyi kutimia kwa ndoto zetu za shibe tunazoziota miaka nenda miaka rudi.

Laiti siku moja Mwenyezi Mungu angelitupatia kiongozi mzalendo kuliko Julius Nyerere, mnyenyekevu kuliko Rashid Kawawa!
MTU wa watu kwa ajili ya watu, ambaye yuko tayali kuweka misingi ya taifa hili hata kama ni kwa gharama ya kupoteza cheo chake kwa sababu ya maslahi ya wengi.
Yule aliye tayari kwenda nje ya maslahi ya chama chake kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa lake!

Huyu ndiye mtu yule taifa linayemsubiri kwa hamu ili aipitishe rasimu ya Jaji Warioba. Ile ambayo inamrudishia mwananchi wa kawaida meno ya kuiwajibisha serikali mpaka mbunge.

Naam ni huyu atakayetutoa katika undumakuwili unaotuchelewesha kimaendeleo atupeleke hadi katika msimamo thabiti wa kisera na kimaendeleo.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.
nackia huyu rais wa sasa atafanya wote tuwe matajiri..............................wenye chama chao wamesema tusahau wote waliopita huyu wa sasa ndo mwsho wa matatizo...................................................................................................ameletwa na MUNGU
 
Back
Top Bottom