Umaskini wa Tanzania ni wa kuchagua na sio bahati mbaya....soma hapa!!


N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Messages
2,602
Likes
10
Points
0
N

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2013
2,602 10 0
Nianze kwa kusema kuwa, hakuna nchi iliyoendelea bila kilimo. Kutokana na kilimo tunapata mazao mengi kama ngozi, maziwa, mazao ya biashara, mazao ya chakula nk. Tanzania umaskini wake ni wakujitakia/kuchagua,kwa kuwa haiwezekani nchi kuwa na kila aina ya rasilimali wakiwemo watu, madini, mabonde yenye rutuba, mbuga za wanyama, milima, mito, maziwa, gesi, nk lakini bado najiuliza tatizo ni nini?

Nimekuja kugundua kuwa ni mfumo wa uvunaji wa rasilimali zetu kuwa mbovu, pia mfumo wa utawala. Katika mfumo wa uvunaji,hapa tunaona kuwa tunachokivuna hatufanyi ongezeko la thamani (value addition), kwani ukifanya value addition kwa mfano ya gesi utapata gesi yenyewe, mafuta mepesi, petrol, mafuta ya taa, dizeli, grisi, lami na plastic materials. Lakini katika haya yote viongozi/wananchi hawajali.

Tungekuwa tunafanya hata hatua mbili za processing tungekuwa juu kiuchumi. Na hapa tunahitaji wawekezaji kwa ajili ya processing industry sio vinginevyo. Kikubwa zaidi serikali iwe na miundo mbinu kama barabara nk. Haiwezekani ndizi Bukoba zinaoza wakati kuna maeneo zinahitajika kwa wingi. Tatizo linakuja ni miundo mbinu tu. Kwa upande wa mfumo wa utawala,serikali imekuwa ikisaini mikataba ya siri, kuuza ardhi kwa wawekezaji kwa lengo la kupata misaada.

Viongozi wa Serikali kupitia mikataba na uwekezaji imekuwa ni sehemu ya kupora utajiri wa asili. Tunaharibu future ya taifa letu kwa kitu cha 400milion kwa mfano, wakati anayesaini huo mkataba (outsiders) wanapata 1000times. Nchi inaweza kuwa na kila kitu,na inaweza kuharibu kila kitu, hii ni kutokana na mfumo wa utawala na mindset ya watawala. Kama mindset ya viongozi ni kuiba hakika huwezi kuendelea kamwe. Na tatizo huwezi kulitatua kama ni sehemu ya tatizo.

Kwa hiyo ili tuondikane na umaskini ni lazima tutengeneze future yetu kwa kujali rasilmali zetu.
 

Forum statistics

Threads 1,273,820
Members 490,485
Posts 30,493,029