Umaskini wa Tanzania na hoja za Ubeberu

salisalum

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
418
136
Kuna nadharia ya ubeberu inayotumika sana siku hizi kuelezea ama sababu za kutofanikiwa kwetu kiuchumi lakini pia sababu za kufanikiwa kwetu. Yaani mabeberu hao hao wanachangia na kutufanya tufanikiwe na hata kutumia vipimo vyao kuonyesha kama tumefanikiwa au la. Ningependa niite "The paradox of mabeberu".

Wakisema tumefanikiwa na kutupa mijihela tunashangilia sana, wakitukosoa au kusema hatujafanya vizuri katika hili au lile tunang'aka na kuanza hata kuwatukana huku tukiwaita mabeberu.

Tabia ya namna inatusaidije katika jitihada zetu za diplomasia ya kiuchumi?

Je, ni sahihi kila mtu kutoa matamko dhidi ya nchi nyingine kwa jambo linalohusu sera ya nchi au ni busara kuiachia taasisi mahsusi kutoa matamko dhidi nchi zingine?
 
Kiashiria kimoja kikubwa cha maendeleo ya kweli, ni pale viongozi wakubwa wa nchi watakapoanza kupata huduma za umma pamoja na wananchi wengi. Na isiwe kwa sababu ya kujionesha, bali kwa sababu ya ubora wa huduma hizo.
 
Back
Top Bottom