Umaskini utafutika kwa kutumia sayansi badala ya usanii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaskini utafutika kwa kutumia sayansi badala ya usanii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jun 15, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  HISTORIA imethibitisha kuwa jamii, dola au mataifa yaliyofanikiwa kupata maendeleo haraka ni yaliyokuwa na viongozi ambao walithamini na kutumia kwa busara ’vipaji’ vya watu wachache miongoni mwa raia katika jamii hizo.


  Himaya za kale zilizokuwa maarufu kama Misri ya Mafarao, Mesopotamia ya Waajemi na China ya ”Mafedhuli” ni mifano ya maendeleo ya kihistoria. Himaya za kisasa zilizo juu kimaendeleo kama Ujerumani, Uingereza, Marekani, Japan, China, Ufaransa, Sweden, Malaysia ni mifano hai wa matumizi ya watu ’vichwa’.  Viongozi wa mataifa hayo wametumia sana akili za wanasayansi wachache wenye elimu bora kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda katika jamii. Kwanza waliochofanya ni kuthamini uwezo wa kiakili wa wanasayansi hao na kisha kuwatia moyo na kuwapa misaada ya hali na mali ili wazidishe juhudi kwa manufaa ya jamii.

   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Myahudi huyu ndiye aliyevumbua "virai" au fomula maarufu sana ya fizikia (E = MC2) iliyowezesha wahandisi kuunda vinu vya mitambo ya kufua nishati ya nyuklia kwa kuharibu maada (matter).

  Aidha ni kwa kutumia fomula ya Einstein na nishati ya nyuklia ndio wahandisi wameweza kuunda na hatimaye kurusha maroketi ya kasi na hata vyombo vya kubarizi katika anga za juu. Mfano hai ni chombo cha Marekani aina ya Apollo 11 kilichopeleka binadamu wa kwanza mwezini miaka 38 iliyopita (1969).

  Fomula ya Einstein ilitumiwa pia vibaya na wahandisi wa kijeshi kwa kutengeneza bomu la kwanza la atomiki lililotumiwa na Marekani kuteketeza kabisa miji ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan mwaka 1945 na kumaliza "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" (1939-45). Binafsi Eistein hakufurahia matumizi hayo ya kijeshi lakini hakuwa na uwezo wa kuyazuia.

  Kitu muhimu na cha msingi zaidi cha kukumbuka kuhusu mwanasayansi huyo ni tabia yake ya uadilifu na kujituma katika fani ya hisabati na sayansi ya fizikia. Kwa mfano kuna wakati viongozi wa Israel, taifa lake la asili, waliwahi kupendekeza na kumwomba Einsten awe rais wa heshima wa Israel, lakini akakataa wadhifa huo mkubwa kwa maelezo kwamba yeye ni gwiji wa hisabati na fizikia na sio siasa na uongozi.
   
Loading...