Umaskin na kupenda kwangu kumenifanya nikubaliane nae kwa kila alisemalo!!

Faiza nimepima kwa ajili ya maandalizi ya safari kama mwezi sasa na namshuru mungu nipo salama!!

Hongera kwa kuwa umepima na afya yako iko safi!!

Unaonaje ukienda "likizo ya mapenzi" mpaka utakapo pata fedha za kumpa huyu unaamini kuwa unapenda?
Ukitoka likizo hiyo nadhani utakuwa unaakili iliyotulia na kufanya maamuzi ya au uendelee naye huyo umpendaye au unatafuta mwingine. Kabla ya kufanya maamuzi hayo muombe Mungu akupe aliye wako.
 
Ushauri wanini tena umeeshaambiwa ukiwa napesa hatatangatanga. tafuta pesa. mapenzi yanagarama au subiri. LOVE IS A PROJECT DONT START IT WITHOUT CAPITAL.
 
Naomba mnisaidie japo ushauri!!
Nipo na girlfriend wangu huu ni mwaka wa tatu sasa tokea nasoma mpka hivi sasa naangaika kutafuta kazi, tatizo ni kwamba huyu mwenzangu nimegundua kuwa yupo na mtu mwengine na nilipomuuliza akajibu kuwa ni kweli lkn hakuna wanachofanya na anafanya yote hayo kwasababu mimi simpi chochote ktk mahitaji yake( si mapenzi) na kama nikimtimizia haoni sababu ya kuwa na hao wengine coz ananipenda( na naamini kweli ananipenda na anaonesha hilo)Sasa mwenzenu nipo kwenye mtihani mwanamke wangu namtaka ila roho nayo yaumia!!Naomben ushauri wenu ushauri wa maamuzi magumu!!!!

KUMBUKA

kama angekuwa anakupenda kweli asingethubutu kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako. sababu kubwa ni kuwa pesa sio msingi wa mapenzi.

hebu jiulize hivi endapo utapata kazi maisha yakawa mazuri halafu baada ya miaka mitano(5) hivi ukapoteza kazi na fedha ikapungua kwahiyo itamlazimu mke wako awe na mwanaume mwingine zaidi yako ili apate fedha, je utakubali hilo? tumia akili usisubiri wakati wote kushauriwa? ww jiulize mwanaume gani wa nje anayeweza kumpa mwanamke fedha bila ya kuwa na mahusiano naye kimapenzi?

pili, kwa kuwa huyo ni girlfriend mnafanya uasherati ambayo ni dhambi kubwa/kuu, mwache, tulia, kaa chini, mwombe Mungu atakupatia mwanamke mwenye upendo wa kweli na sio huyo uliye naye. huyo ukimwoa atakuua kwa presha sio mwaninifu wala hakupendi?

 
Du!Hata km ni kupenda huku kwako kumepitiliza,
Km utaendelea naye jiandae kufa mapema km sio kwa presha basi kwa dipreshen!
Huyo mdada kakudhalilisha sana,hebu amka utoke humo usingizin wanaume hawako ivo bana,
Achana naye bwana mwombe mungu atakupa atakayekuvumilia hata ukiwa km ulivo na kukupenda kwa dhati!
 
kijana hapo unachemsha kabisa, na huyo msichana wala hakupendi,kama anakupenda kwa dhati angecumilia kwa hali uliyokuwa nayo
 
Yaani anagawa uroda nje halafu unasema anakupenda?How?Wewe ni mtegemezi wa hisia,unajihisi mpungufu kama hutakua nae,achana na tabia hiyo wewe ni kamili bila hata kuwa nae,na pia hakupendi huyo!
 
Du!Hata km ni kupenda huku kwako kumepitiliza,
Km utaendelea naye jiandae kufa mapema km sio kwa presha basi kwa dipreshen!
Huyo mdada kakudhalilisha sana,hebu amka utoke humo usingizin wanaume hawako ivo bana,
Achana naye bwana mwombe mungu atakupa atakayekuvumilia hata ukiwa km ulivo na kukupenda kwa dhati!

Asante ndugu kwa kunipa moyo na nishachukua maamuzi ya kuachana nae!!
 
mtoa mada huyo akupendi kabisa coz kwanini atembee na mtu mwingine? mapenzi ayahangalii una nini ivyo yeye ni loveineed!
 
Da pole sana jaribu kuwa na subira na pia jifunze kujitegemea zaidi kuwa creative hata ka ni ndizi uza isiendeshwe na Tamaaa ,wengi ni maskini wa fedha ila tajiri wa afya .
 
Pata maombezi; pepo toka haraka sana mwachie kijana huyu, usimpe taabu tena, nasema pepo toka toka toka toka toka, uanze na kulegea halafu utoke kabisa; Amen.
 
unless una uhakika anao wanaume wengi ndio umuache,kama ni mmoja na anatoa mkwanja tulia hapo hapo

mwache tu akamuliwe mzee afterall mgodi ni wa kwake... cha kufanya, uwe unapitia pitia kwa huyo jamaa siku mojamoja na kuchukua 'fwedha' ya matumizi kwa kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi mfukoni
 
Dogo hakuna upendo hapo. Huyo ana mategemeo kwamba ipo siku utatoka ndiyo maana anakuweka reserve. Pia hizo ni dharau kubwa sana, eti anao wengine kwasababu huna kipato? Tumia elimu yako kufanya analysis, then make decision. Elimu siyo tu ikupe ajira, lkn pia ikusaidia ktk analysis ya mambo mengine ktk jamii.

Nb: Chain ya hiv haina excuse yoyote.
 
Back
Top Bottom