Umasikini wetu ni wa kujichagulia. Je! Inaleta maana yoyote? Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu kuwa maskini? Hapana!

Status
Not open for further replies.

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Je! Inaleta maana yoyote kwamba Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu, na maji tosha; kuwa masikini zaidi ulimwenguni. Umasikini wetu ni ule wa kujichagulia, Afrika inapaswa kutafakari tena mfumo wake wa uchumi na metriki za kupima mafanikio.

Wengi wenu bado hamjanipata, kwani mnawezadhani kuwa ninawauliza: “kwanini mataifa haya wasiuze rasiliamali vao kwa faida kubwa?”

Hiyo sio lengo langu:


Fikiria: Hauwezi kula kompyuta, huwezi kunywa begi la thamani, huwezi kuzalisha machine kwa fikra na mipango peke yake. Kimsingi, vitu hivyo vyote havina thamani bila vifaa vya msingi: Ardhi, maji, watu (Kazi).

Haya ndio mahitaji ya kimsingi ambayo ndio chanzo cha utajiri wote duniani, na tunayo tele.

Sasa Kwanini sie ndio maskini zaidi?

Kwa maoni yangu, ukoloni na vipaumbele vya kiuchumi vilivyopotoka ndo sababu.

Sisi Waafrika tumechagua kufafanua mafanikio ya kiuchumi kwa masharti ya magharibi bila sababu nzuri: vitu kama: Skyscrapers, viwanja vya ndege, barabara, na kompyuta n.k., zinafafanua mtazamo wetu wa utajiri.

Hatuwezi kuzalisha chochote kati ya hivi kwa kujitegemea, hivyo tunadai msaada wa magharibi. Haishangazi pale kampuni za kigeni zinapodai pesa za kigeni, zikidai zetu hazina thamani kulingana na zao.

Kulingana na wao; madini, Ardhi, na kazi-hatarishi (hard labour) ndio kitu pekee ambacho huanza kulingana na thamani ya matunda ya kazi zao; na sie tunakubali na kutoa.

Kukataa kunajibiwa kwa kuaibishwa kama maskini (waandishi wao wa habari: BBC Swahili), kutengwa (Zimbabwe, Cuba), na hata uvamizi (Libya), kwa hivyo hofu na maslahi ya wachache (wanasiasa) husukuma kukubalika kwa faida ndogo.

Ugavi na mahitaji (supply and demand) yadaiwa kuwa sababu ya kusukuma swala hili, sasa kwanini, ukizingatia kwamba ulimwengu hauwezi kujimudu bila malighafi ya Afrika; thamani ya malighafi za nchi zake zipo chini sana.

Hatujawahi kuhoji mfumo huu wa kuthamini na ivyo tumegeuza mataifa yetu kuwa mashamba ya magharibi na uwanja wa madini.



Pointi za ziada:
Mtu anaweza kuuliza: je, vitu hivyo ambavyo umevitaja ni utajiri wa kweli?
Kwani huwezi kumtibu mtoto wako na dhahabu, ivyo mtu anahitaji dawa kutoka magharibi na maarifa yake.

Hapana! huu kwakweli ni mtego wa mzunguko (circle):


Dawa kwa mfano; angalia magonjwa tunayotibu, idadi kubwa yao ililetwa kwetu na mfumo huo huo.

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na utumiaji wa sukari iliyosindikwa (fructose). Ikiwa Waafrika wangeshikilia lishe yao ya asili, wasingepata kisukari.

Cholera, Ebola, Typhoid, na milipuko mingine husababishwa na kuishi kwa watu katika nafasi finyu mijini. Msongamano wa watu mijini unasababishwa na watu kulazimishwa kuhama kwa idadi kubwa kwenda mijini kupata pesa kwa kuuza kazi.

Malazi duni na miundombinu husababisha wakaazi hawa wa jiji wasio na uzoefu na miji, kusambaza magonjwa ambayo wasingekuwa nayo vijijini.

Ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo, ugonjwa wa ini; zote husababishwa na ulaji wa bidhaa zenye sumu: Pombe, sigara, uchafuzi wa mazingira, na kemikali zingine ni chanzo kikubwa cha shida hizi.

Simu za rununu, Magari, na vifaa vingine vya mawasiliano mara nyingi ni muhimu kwa sababu ya mpangilio wa maisha watu wanalazimishwa kuingia kwenye mchakato wa kuuza kazi yao. Kijadi, Waafrika wamekaa karibu na mahitaji yao na hivyo kuondoa hitaji la zana za mawasiliano za masafa marefu

Wakati gharama na mazingira ya kazi yanatenganisha familia, simu huwa chaguo pekee kwa mawasiliano. Wakati mtu anaishi masaa 1-2 kutoka mahali pa kazi, magari ndiyo njia pekee ya kusonga mbele.

Vitu vyote vilivyotajwa hapo juu vinahitaji uwekezaji zaidi. Dawa kwa mfano lazima iambatane na shule za matibabu, hospitali, na aina zingine za miundombinu ili kuhudumia mahitaji. Na hizi mara nyingi zinahitaji msaada wa kigeni na sarafu ya kigeni. Hii inamaanisha uuzaji zaidi wa kazi, ardhi, na maliasili nyingine.


Njia ya Mbele
Huu ni mduara, mchezo ambao hatuwezi kushinda.

Afrika inapaswa kutafakari upya mfumo wake wa uchumi kwa kutanguliza watu wake. Kuunda mfumo ambao unalinganisha kimkakati na maslahi yake.

Kwanza, watu wetu wanahitaji chakula, maji, jamii, na makazi. Hatuhitaji kampuni za magharibi kutoa hiyo kama tunayo na wingi wa vitu hivyo vyote.

Jinsi tunavyowasilisha yote hayo yanapaswa kuwa uamuzi wa ndani kwani wanajua sana hali yao.

Kimsingi, tunapaswa kuondoa mtu wa kati na kuwapa watu na jamii mahitaji yao muhimu bila kuwalazimisha kuuza kazi zao kwenye biashara ambazo hazitekelezi malengo hayo.

Vipimo vyetu vya uchumi, badala ya kuzingatia takwimu holela kama Pato la Taifa, inapaswa kulenga dhiki ya kiuchumi kwa lengo la kuitokomeza.

Ndio, tunapaswa kufanya biashara, lakini kwa uangalifu mkubwa.

Uagizaji wa bidhaa au teknolojia zisizo lazima unapaswa kuepukwa. Kimsingi, chochote kinachounda utegemezi wa muda mrefu kinapaswa kupitishwa kimkakati na mpango wa jinsi ya kutoroka matumizi yake.
 
Ardhi, maji, watu (Kazi).
Kuna sehemu ya dunia isiyokuwa na vitu hivyo? Madini una technology ya kuyachimba na kuyatumia? Kilimo una nyenzo za kilimo? subsistence farming itakupeleka wapi katika "utajiri"?

Ni kukaa na walio na uwezo wa kufanya kilimo, kuchimba madini mka negotiate win- win terms ukafaidika na wao wakafaidika. OR AS NYERERE PUT IT ONCE, AU UVIACHE VYOTE UJENGE UWEZO TARATIBU HATA KWA MIAKA 100, THEN YOU EXPLOIT YOUR NATURAL RESOURCES. Lakini hii mitulinga mnayowafanyia wenye utajiri wa kufanya hayo, hamtafika popote!
 
Tanzania sio kisiwa. Ili kufanikiwa kiuchumi dunia ya leo, ni lazima tushindane na wenzetu kiuchumi na kufanikiwa zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya "Made in Tanzania" itambe Africa na duniani.

Lakini sasa hivi hata mafuta ya kula tu Made in Tanzania haitoshi eti hadi yaje kutoka China. Sukari, simenti za ujenzi nk. Mambo ni hivyo hivyo..

Mliambiwa Tanzania ya viwanda, ila investors wanakimbia mbioo, hakuna mtu anataka kuwekeza Tanzania sasa hivi. Serikali ina-control kila kitu, na imekuwa hivyo tokea uhuru. Sasa ni kwa nini tusilaumu mfumo wa serikali hii? Hao ndio wanaangusha wananchi wa Tz. Watake wasitake, huo ndio ukweli.
 
Je! Inaleta maana yoyote kwamba Bara lenye ardhi yenye rutuba, idadi kubwa ya vijana, madini adimu, na maji tosha; kuwa masikini zaidi ulimwenguni. Umasikini wetu ni ule wa kuchichagulia, Afrika inapaswa kutafakari tena mfumo wake wa uchumi na metriki za kupima mafanikio...
Yawezekana tatizo ni hilo, tuna kila kitu, labda ingekuwa vice versa akili ingechaji...
 
Tanzania sio kisiwa. Ili kufanikiwa kiuchumi dunia ya leo, ni lazima tushindane na wenzetu kiuchumi na kufanikiwa zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya "Made in Tanzania" itambe Africa na duniani. Lakini sasa hivi hata mafuta ya kula tu Made in Tanzania haitoshi eti hadi yaje kutoka China. Sukari, simenti za ujenzi nk. Mambo ni hivyo hivyo.. Mliambiwa Tanzania ya viwanda, ila investors wanakimbia mbioo, hakuna mtu anataka kuwekeza Tanzania sasa hivi. Serikali ina-control kila kitu, na imekuwa hivyo tokea uhuru. Sasa ni kwa nini tusilaumu mfumo wa serikali hii? Hao ndio wanaangusha wananchi wa Tz. Watake wasitake, huo ndio ukweli.
Sasa hapo ndo tatizo:
Kwanini lazima awepe investor kutoka nje? Umeshawahi kusikia Marekani wanakuja Afrika kutafuta investors?

2. Tunashindana na wenzetu kwa lipi?

Pointi yangu ni kwamba: mfumo mzima wa kiuchumi umejengwa ili sisi waafirka tushindwe na tutegemee ulaya.

Jiulize hao investors wanakimbia nini, kama sio sera wasiozipenda. Na ni sera gani wanazitaka.
 
sasa hapo ndo tatizo:
kwanini lazima awepe investor kutoka nje? umeshawahi kusikia marekani wanakuja afrika kutafuta investors?....
WaTanzania wengi hawana hela ya kujenga viwanda vikubwa au kufanya miradi mikubwa. Na serikali ya Tz haitoi mikopo wala kusaidia mtaji. Lakini kuna investors wengi wenye hela, wangependa sana kuwekeza na Mtanzania mzawa. Ni win win situation.

Hebu soma hii link hapa. Ni waTz walipata partners, lakini serikali imewaangusha.
 
Kuna sehemu ya dunia isiyokuwa na vitu hivyo? Madini una technology ya kuyachimba na kuyatumia? Kilimo una nyenzo za kilimo? subsistence farming itakupeleka wapi katika "utajiri"?...
Hoja yako ina issue zifuatazo:
1. Kuna nchi nyingi hazi hivi vitu: Singapore ni moja kwa chap chap
2. Neno utajiri inabidi tuwa makini nalo sana: Kwani tunaweza tukahisi kitu ni utajili wakati ni uchafu (zingatia bidhaa za plastiki vs chakula)
3. Win-win terms ni vague sana (40% 50% 60%?)

Point yangu mie ni bara la Afrika kukomaa na kutimiza mahitaji ya msingi kabisa ya raia wake: na baada ya hapo kukuza uwezo wa kutimiza mahitaji haya kimkakati.

Mfano: Tujiepushe na mafuta as much as possible kwani kuingiza mafuta kunaitaji dollar, dollar inatuforce tifanye biashara zisizo na tija na wa tu wetu: zaidi ya hapo tunakuwa wepesi kusukumwa na marekani kwa kutumia mabavu (santions)

Solution: Tu invest kwenye public transportaton, na architecture inayopunguza safari ndefu: hii itapunguza need for cars inturn fuel
 
WaTanzania wengi hawana hela ya kujenga viwanda vikubwa au kufanya miradi mikubwa. Na serikali ya Tz haitoi mikopo wala kusaidia mtaji. Lakini kuna investors wengi wenye hela, wangependa sana kuwekeza na Mtanzania mzawa. Ni win win situation.
Hebu soma hii link hapa. Ni waTz walipata partners, lakini serikali imewaangusha.
Ok point nzuri:

Lakini: Viwanda vikubwa vya kazi gani:

Hapa inapaswa uwe makini kwani ukichunguza utagutukia kwamba: Tunatafuta solution kwa tatizo tuliotengeneza wenyewe

Viwanda kwa ajili ya kutengeneza bidhaa: Bidhaa kuuza nje kwa ajili ya foreign currency: foreign currency ya kununua medicine

Medicine ya kutibu cholera: Cholera inayotokana na slums: Slums zinazotokana na watu kuhamia mijini kufanya kazi kwenye viwanda.
 
ok point nzuri:

lakini : viwanda vikubwa vya kazi gani:..
Ni sawa na wewe kuoa mke, halafu ukamwambia tuishi maisha yasiyohitaji kutumia hela ya noti hata kidogo? Je, hayo maisha yatawezekana?

Una ndoto ambazo haziwezekani kwa dunia ya leo. Kila nchi inategemea nchi nyingine. Mfano hakuna viwanda vya mashine, enginez, nk Tanzania, kwa hio lazima tractors, irrigation equipment, etc tuvinunue kutoka nje (import).

Tatizo sisi hata hio ardhi tuliyo nayo, ndio nimesema hatuitumii ipasavyo, kulima vitu vizuri, vikatengeneza consumer products nzuri nchi Tanzania manake.. kuzalisha vitu vya quality ili viuzwe nchi za nje (export),. na hela yetu iwe na thamani, na tuitumie kuendeleza nchi yetu. Eti nchi ya viwanda...

Kwa hiyo jaribu kufikiria solutions ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.
 
hoja yako ina issue zifuatazo:
1. kuna nchi nyingi hazi hivi vitu: singapore ni moja kwa chap chap...
Kuingiza mafuta YES KUNAHITAJI DOLLARS. Hela ya Tshs hauwezi itumie nchi yeyote. Hata kenya tu HAWAITAKI. Kila kitu unachonunua nnje ya Tz, lazima utumie Forex. Na hio forex money, lazima uipate kwa kuifanyia kazi.

Kama umeenda kuuza bidhaa nje ya nchi (exports za viwanda, basi unalipwa forex huko huko directly). Na kama umeuza kitu ndani ya Tanzania, lazima ubadili Tshs iwe forex, ndio uende nchi ya nje kununua hicho kitu.

Na hao investors tunaowakimbiza teari wana masoko nchi za nje. MTz angefaidika sana, ila sasa tunarudi miaka ishirini na zaidi nyuma ila WANAKUAMBIA TUNASONGA MBELE
 
Ni sawa na ww kuoa mke, halafu ukamwambia tuishi maisha yasiyohitaji kutumia hela ya noti hata kidogo? Je, hayo maisha yatawezekana?

Una ndoto ambazo haziwezekani kwa dunia ya leo. Kila nchi inategemea nchi nyingine. Mfano hakuna viwanda vya mashine, enginez, nk Tanzania, kwa hio lazima tractors, irrigation equipment, etc tuvinunue kutoka nje (import). Tatizo sisi hata hio ardhi tuliyo nayo, ndio nimesema hatuitumii ipasavyo, kulima vitu vizuri, vikatengeneza consumer products nzuri nchi Tanzania manake.. kuzalisha vitu vya quality ili viuzwe nchi za nje (export),. na hela yetu iwe na thamani, na tuitumie kuendeleza nchi yetu. Eti nchi ya viwanda...

Kwa hio jaribu kufikiria solutions ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.
Sidhani kama point yangu ni kwamba tuishi bila kutumia money kama medium of exchage: na wala sisem napinga kuacha kutumia money kama medium of exchange.

mi point yangu inagusa swala la value: hapa nikiuliza kwanini nchi zanye vitu amabvyo fundamentally ni vya thamani zinathaminiwa kwa chini kabisa.

ila tuangalie mfano wako: nchi 1 inatoa vifaa (tractors), nchi 2 inatoa ardhi na watu.
kwanini nchi 1 inakuwa na thamani kuliko nchi 2
Kwanini nchi 2 inalazimika kushusha thamani ya bidhaa zake?

kuhusu matumizi mabaya ya ardhi (hii point ni nzuri na naunga mkono) na upo sahihi ndo maana nasema tunahitaji mfumo utakao fanya matumizi ya ardhi yanufaishe wananchi.

lakini mi sikubaliani na notion kwamba ardhi lazima itumike kuzalisha consumer goods for exchange: again hili ndo tatizo (matumizi mabaya ya ardhi) kwani for the most part tunalenga kupata foreign currency na kutumia hizo foreign currency kutungeneza even more dependency on foreign products.

NOTE: mi sipingi trade, ila nasema kuwe na strategic trade, na kabla ujaanza ku-trade, hakikisha kwanza umekidhi mahitaji ya watu wako ili usiwe desperate mda wa exchange.
 
Kuingiza mafuta YES KUNAHITAJI DOLLARS. Hela ya Tshs hauwezi itumie nchi yeyote. Hata kenya tu HAWAITAKI. Kila kitu unachonunua nnje ya Tz, lazima utumie Forex. Na hio forex money, lazima uipate kwa kuifanyia kazi. Kama umeenda kuuza bidhaa nje ya nchi (exports za viwanda, basi unalipwa forex huko huko directly). Na kama umeuza kitu ndani ya Tanzania, lazima ubadili Tshs iwe forex, ndio uende nchi ya nje kununua hicho kitu.

Na hao investors tunaowakimbiza teari wana masoko nchi za nje. MTz angefaidika sana, ila sasa tunarudi miaka ishirini na zaidi nyuma ila WANAKUAMBIA TUNASONGA MBELE
Doc, hapa umegusa point yangu vizuri: mimi do nauliza kwanini hela yetu aina thamani (najua jibu lake kiuchumi ndo maana nina challenge hii system ki-logic)
fikilia:
tuseme leo afrika nzima wakazuia kuuza mazao duniani, na wakaamua kuanza kulisha watu wao kwanza kwa kutafuta suluhisho ya challenges za ukulima. asilimia 100% ya vijana na resources ikatumika katika hiyo task.

nini kitatoke Africa? na why?

mda huo huo nini kitatokea duniani na why?

mtazamo wangu ni kwamba our raw materials (food, minerals, etc. ) have far more value that what they give us.
lakini kwa sababu ya desperation, curroption, na self interest: Africa tuna-exchange kwa really low value


mwishowe tunaviwanda vinavyomilikiwa na wageni, migodi ambayo hailipi kodi, na nchi ngeni zinatupa masharti ya kuishi

tunahitaji economic system (hii ni nje ya expertise yangu) inayomlenga mtanzania (mwafrika) na matakwa yake.
 
Sidhani kama point yangu ni kwamba tuishi bila kutumia money kama medium of exchage: na wala sisem napinga kuacha kutumia money kama medium of exchange...
Ili uchumi ukue, ni lazima kukuza GDP na GNP. Kuzikuza hizo, ni lazima nchi iwe inategemewa sana na nchi nyingine duniani. Umesema nchi #2 inaharibia nchi #1, HAPANA. Ni nchi #1 inashindwa kucheza mchezo vizuri wa kiuchumi, na mwisho wa siku inajiharibia yenyewe.

Lengo sio kutegemea Forex, lengo ni kufanya Tshs iwe ni forex ya kutegemewa na nchi nyingine. Na hapo ni jambo MOJA TU SOLUTION YAKE. Solution ni kuuza vitu vingi vya KiTz nchi za nje. Unapoviuza, manake nchi za nje wanavinunua kwa kutumia Tshs. Na hela yako INAPANDA THAMANI.

Ukishaelewa principles za economics, utaelewa ni kwanini mengi unayoyaandika hapa sio sahihi.
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Doc, hapa umegusa point yangu vizuri: mimi do nauliza kwanini hela yetu aina thamani (najua jibu lake kiuchumi ndo maana nina challenge hii system ki-logic)...
Hapana ndugu yangu. Value ni we ndio inatakiwa uietengeneze. Ukienda supermarkets za USA ukanunua korosho, ni ile ile INAYOTOKA MTWARA. Lakini imeandikwa made in vietnam au made in India. Ni korosho ya Grade A. Walinunua raw materials, wakaipeleka kwa viwanda nchini kwao. Wakaitengeneza, ikaenda kuuzwa USA, Europe etc. Tanzania hawaweki viwanda sababu ya SERA MBAYA. Afadhali wanunue tu raw materials waachane na sisi.

Ukienda supermarket Tz ukala korosho, lazima kila pakti utakuta ina Korosho mbili tatu MBOVU, ZIMEOZA NK.

Hio ndio made in Tanzania. Na hakuna mtu atanunua hio nchi zilizoendelea zenye fedha nyingi ambapo pakti ya korosho inauzwa $10 na kuendelea. Lakini Tz, pakti hio hio ni $1.

Hakuna anayetuharibia. Tunajiharibia wenyewe KUTOTAKA kutengeneza vitu vya quality. Na hapo ndio collaboration na investors ingesaidia. Exposure yao inasaidia sana katika utengenezaji wa quality products na pia SOKO ili zikauzwe nchi za nje.
 
Ili uchumi ukue, ni lazima kukuza GDP na GNP. Kuzikuza hizo, ni lazima nchi iwe inategemewa sana na nchi nyingine duniani. Umesema nchi #2 inaharibia nchi #1, HAPANA. Ni nchi #1 inashindwa kucheza mchezo vizuri wa kiuchumi, na mwisho wa siku inajiharibia yenyewe.

Lengo sio kutegemea Forex, lengo ni kufanya Tshs iwe ni forex ya kutegemewa na nchi nyingine. Na hapo ni jambo MOJA TU SOLUTION YAKE. Solution ni kuuza vitu vingi vya KiTz nchi za nje. Unapoviuza, manake nchi za nje wanavinunua kwa kutumia Tshs. Na hela yako INAPANDA THAMANI.

Ulishaelewa principles za economics, utaelewa ni kwanini mengi unayoyaandika hapa sio sahihi.
Ili uchumi ukue, ni lazima kukuza GDP na GNP. Kuzikuza hizo, ni lazima nchi iwe inategemewa sana na nchi nyingine duniani. Umesema nchi #2 inaharibia nchi #1, HAPANA. Ni nchi #1 inashindwa kucheza mchezo vizuri wa kiuchumi, na mwisho wa siku inajiharibia yenyewe.
Ndugu yangu: unaongea exactly ninacho kisema ila we unasukuma upande mwingine:

supply and demand:

Ndo maana nasema, kama nchi za Afrika zikipunguza demand on western goods tutapunguza desperation yetu (mfano; kupunguza mafuta kwa ku-invest in public transportation and kupunguza commute)

lakini western countries hawawezi kusema watapunguza ulaji, rare minerals, au labour kwani vyote ni muhimu kwa uchumi wao.

Tukijenga nchi zetu strategically, tunaweza punguza kwa asilimia kubwa western dependency inturn kutupa leverage kwenye meza ya exchange na kukudha thamani ya vitu vyetu bila industrilisation.

lakini tatizo tunaenda direction ya exponential depedency (magari kutoka nje= mafuta= foreign currency = labour= magari = etc. )

hii ndo point ya essay
 
Hapana ndugu yangu. Value ni we ndio inatakiwa uietengeneze. Ukienda supermarkets za USA ukanunua korosho, ni ile ile INAYOTOKA MTWARA. Lakini imeandikwa made in vietnam au made in India. Ni korosho ya Grade A. Walinunua raw materials,

Mi nabisha kwamba Quality ya bidhaa ndo kichocheo kikuu cha bei (ndio inaweza changia lakini inabidi uwe makini)

katika soko la ushindani Quality ya bidhaa inaweza kuchangia bei ya bidhaa: lakini kuna vitu vingi vinavyoweza influence":
1. upatikanaji ni kitu muhimu sana kuliko quality:

ushahidi:
angalia soko la mafuta la OPEC, baada ya baadhi ya nchi kuanza kuzalisha kupita kiasi bei ilishuka, na baada ya nchi fulani kuweka vizuizi bei ilipanda.

Pointi yangu ni nini: Afrika tukiamua kuweka control kwenye supply ya raw materials, haitajalisha nani anaweza kuchambua korosho, bei itakuwa chini ya usimamizi watu na ivyo kunyanyua value
 
Mi nabisha kwamba Quality ya bidhaa ndo kichocheo kikuu cha bei (ndio inaweza changia lakini inabidi uwe makini)...
Kuweka control ya supply ndio KOSA KUBWA SANA lilifanyika miaka miwili iliyopita suala la korosho. Wanunuzi wa nchi za nje walikimbia wakaenda kuwekeza kwa mashamba ya west africa na wakanunua huko na za kwetu?? Tulitafuta soko hadi tukakiona.

Hauwezi PIGANA na principles za economics. Quantity ni muhimu, lakini quality ni muhimu sana pia, hasa kwa final consumer. Na final consumer, ndio ana-dictate price ya kila kitu along the supply chain.
 
Nyie shukruni Tu Kwa vile mna mishahara minono au mna Tu viwanda twenu twa bakery..... Mnaona wenzenu wanaotaabika kama wanatania....
Mambo sio rahsi kama unavyofkria
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom