Umasikini waongezeka Marekani; zaidi ya raia milioni 146 wanaishi katika umasikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umasikini waongezeka Marekani; zaidi ya raia milioni 146 wanaishi katika umasikini

Discussion in 'International Forum' started by MpigaKura, Dec 16, 2011.

 1. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Takwimu mpya zilizotolewa nchini Marekani zinaonyesha kuwa, umasikini umeongezeka nchini humo ambapo zaidi ya raia milioni 146 wanaishi katika umasikini. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, karibu nusu ya Wamarekani wanakabiliwa na umasikini huku wengi wao wakishindwa kudhamini hata hawaiji na mahitaji yao ya lazima ya siku kama chakula.

  Ripoti hiyo iliyotolewa na Idara ya Takwimu ya Marekani inaonyesha kuwa, raia milioni 49 wanaishi chini ya mstari wa umasikini. Takwimu zinazidi kubainisha kwamba, ongezeko hilo la umasikini limetokana na kuweko kipato kidogo hali ambayo imewafanya wananchi hao kukabiliwa na njaa. Utafiti uliofanywa katika miji 29 ya Marekani unaonyesha kuongezeka maombi ya misaada ya dharura ya chakula.

  Hayo yanajiri katika hali ambayo, Wamarekani milioni 24 na laki nne wamepoteza kazi zao au hawana ajira kabisa. Ripoti hiyo ya Idara ya Takwimu ya Marekani inamalizia kwa kusema kuwa, umasikini, mshahara mdogo na kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo kodi ya nyumba nchini humo ni miongoni mwa sababu za kuongezeka umasikini na ugumu wa kudhamini mahitaji muhimu ya maisha yakiwemo ya chakula katika nchi hiyo.


  Over 146 Millions Live in Poverty in US


  'Based on a new supplemental measure by the Census Bureau more than ninety seven million Americans are considered to have low-income, defined as between 100 and 199 percent of the poverty level.

  Another 49.1 million Americans live below the poverty line, meaning 146.4 million Americans, or 48 percent are considered low-income or poor, Associated Press reported on Thursday.'

  Source:
  Over 146 Millions Live in Poverty in US - David Icke Website
   
Loading...