Umasikini wa wengi ni chanzo cha utajiri wa wachache

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Kwa sasa kuna michezo ya kubashiri na bahati nasibu mbalimbali, tunacheza kwa kuwa tunataka shortcut ya mafanikio na bado inakuwa shida ni wachache wanapata pesa hizo.

Tufanye hesabu ndogo kwenye hizi habari za bahati nasibu,

Kuna michezo ambayo kiwango chake cha kucheza ni tsh 500,

Tanzania ina watu takribani milion 55, kati ya hao tuseme milioni 1 wamecheza, haya tufanye hesabu.

1000,000 * 500 = 500,000,000 Maana yake kama watanzania milioni moja wamecheza kwa shilingi miatano kila mmoja wanakuwa wameipa kampuni Tsh 500 milioni, katika millioni miatano toa millioni kumi za kumpa mshindi nyingine zinaingia kwenye kampuni, kisha angalia tena jinsi umasikini unavyowakamata wanaohitaji kupata mafanikio ya shortcut.

Nikizungumzia betting, the odds ni illusion

Kwenye bettings za kubashiri michezo, odds huwa zinawekwa kumnufaisha mwenye kampuni, the odds are always with company, yaani wao wenyewe wamejiwekea uwezekano mkubwa wa kuchukua hela ya mtu kuliko anayeweka mkeka kuchukua hela yao. Inconsistence decisions and bad bets, irrationality ni moja ya topic iliolezea odds/probability vizuri

Masuala yote ya michezo ya kubashiri na bahati nasibu huwa yanapata umaarufu mkubwa kwa kuwa ni washindi peke yao hutangazwa huwezi kupewa idadi kamili ya washiriki. Wapo wengi wanaocheza michezo hiyo mitandaoni kwa siri, matokeo yao huwa siri yao.

Kabla hatujaenda kwenye uraibu wa shughuli hizi ambazo tunadhani zinatupatia kipato ni muhimu kuona ya kuwa pesa tunazochangia kampuni husika ni nyingi kuliko pesa tunayoingiza.

Mafanikio kiuchumi huja kwa mipango na mikakati, uchumi unatambua uwepo wa bahati lakini kimsingi hatari ya mapato kutokana na michezo ya kubashiri ni kubwa kuliko mipango mingine ya kibiashara.

Na pia uwezekano mtu wa kufanikiwa kimaisha kwa kupitia michezo ya kubashiri ni mdogo sana kiasi ambacho watu wengi huishia kubaki na matumaini ya kufanikiwa na kubaki kwenye michezo ya Kamari ambayo huwafanya wapoteze hata vingine ambavyo wamevitafuta awali.

Ni michezo ya kutumaini mafanikio kupitia njia rahisi ndio inayozidi kuwafanya matajiri wazidi kuwa matajiri na masikini wazidi kuwa masikini.

Na pia,

Sitapinga Imani za watu lakini angalia umasikini unavyodumaza fikra kiasi cha kuwaza shortcut, kitu ambacho kinafanya masikini wawape utajiri wengine. Imani tulizo nazo juu ya mafinikia ndio kisima cha matumaini.

Kwa kuanza tuangalie Imani, za dini na uganga, angalia idadi ya watu wanaonunua vitu mbalimbali ili kupata nafuu ya maisha yao wanavyojikuta wanampa unafuu mchungaji au mwenye dini yake, sababu inayofanya viongozi kuwa na maisha bora tofauti na waumini. Babu wa Loliondo alikuwa anachukua shilingi mia tano tu kama ujira wake, kupitia hiyo maisha yake yamebadilika kabisa.

Hapo tusiweke maneno kuhusu uganga, kwa kuwa wapo waganga waliofanikiwa kirahisi kwa kushika matumaini ya watu wanaotaka kufanikiwa. Fikiria wengi wanaotapeliwa kwa kutaka utajiri kupitia jina la freemason kitu ambao wengi hupigwa hela kwa kuwa taarifa wanazozijua kuhusu freemason ni tatizo kwao na wao wanabaki kuhitaji mafanikio na sio vinginevyo. Wengi wao ni masikini tu, wanaotaka unafuu wa maisha yao, katika kutafuta unafuu wao njia zao huishia kuwatajirisha walio wachache na wao kuzidi kuwa masikini

Hapo naonyesha tu jinsi umasikini unavyokuwa chanzo cha utajiri wa walio wachache.

Maendeleo yakiangaliwa kwa kile tunaita social system, yaani muingiliano kati ya economic and non economic factors. Ambayo inaangalia attitude, ambayo inaweza kutafsiria kama Attitudes The states of mind or feelings of an individual, group, or society regarding issues such as material gain, hard work, saving for the future, and sharing wealth.

Signed: OEDIPUS
 
Well said mr

Nipo na jamaa kadhaa wenye hulka ya kutafuta unafuu kwa michezo pendwa ya kubadhiri .

Utasikia nimeweka 500 tu hiyo haina shida sana.

Tupige kazi vijana ni easy way.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri ni ubinafsi
Huwezi kuwa tajiri bila kuwakandamiza/kuwanyinya watu fulani , kadiri unavyowakandamizi ndivyo wewe unapata utajiri ili kutimiza ubinafsi wako na kuwatengeneza maskini wengi zaidi.
Kwahiyo ukitaka kuwa tajiri lazima ufikirie ni kitu gani ufanye kiwa addict watu ili upate namna ya kuwakandamiza.
watu wenye roho hio wasingekuwepo maskini pa wasingekuwepo ..bila tajiri hakuna maskini!
btw huu ni mtazamo tu mkuu
Nasimama kuwa sahihi ni umasikini unaofanya matajiri kuwa matajiri, na sio utajiri wao unaofanya masikini, soma hoja zangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri ni ubinafsi
Huwezi kuwa tajiri bila kuwakandamiza/kuwanyinya watu fulani , kadiri unavyowakandamizi ndivyo wewe unapata utajiri ili kutimiza ubinafsi wako na kuwatengeneza maskini wengi zaidi.
Kwahiyo ukitaka kuwa tajiri lazima ufikirie ni kitu gani ufanye kiwa addict watu ili upate namna ya kuwakandamiza.
watu wenye roho hio wasingekuwepo maskini pa wasingekuwepo ..bila tajiri hakuna maskini!
btw huu ni mtazamo tu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Akhsante wajinga bila nyinyi tusingekuwa matajiri.

Hiyo ni moja kati ya quote naipenda kuhusu utajiri,
Kuna wachache kati yetu ambao hutumia ujinga wa wengi na kupata utajiri na kuendelea kuwa matajiri kwa kuwa wengi ni wajinga na wanaamini Ignorance is Bliss

Sio lazima unyonywe ili mtu awe tajiri, wangapi wanalipa maelfu ili kupata burudani, iwe vichekesho au muziki, Is it that worth?
 
Akhsante wajinga bila nyinyi tusingekuwa matajiri.

Hiyo ni moja kati ya quote naipenda kuhusu utajiri,
Kuna wachache kati yetu ambao hutumia ujinga wa wengi na kupata utajiri na kuendelea kuwa matajiri kwa kuwa wengi ni wajinga na wanaamini Ignorance is Bliss

Sio lazima unyonywe ili mtu awe tajiri, wangapi wanalipa maelfu ili kupata burudani, iwe vichekesho au muziki, Is it that worth?
its worth kwakua ni furaha yao, na vile hafanyi mara kwa mara.. labda kama yeye kila siku halali bila hivyo ...ila kuna vile kama mtu haipiti siku hujanywa mo energy..
 
Kuliko mia tano hy kuivutia sigara na sigara ikaacha sumu mwilin bora kuipa kampun za kubahatisha inunue magari madereva wapate ajira serikali ipate kodi ijenge hospitar nk kupitia hiyhy jero zetu huoni kama faida au unawaza upande mmoja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom