Umasikini wa Afrika kwa kiasi kikubwa unasababishwa na sisi raia na si Wanasiasa

RTI

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
2,423
7,124
Kama kichwa cha habari kinavyo sema kwakweli waafirika hasa vijana tuna takiwa kujitafakari tena kwa kina.

Kila siku tumekuwa na mtindo wa kuwalaumu wana siasa kwa umasikini wa nchi zetu ,lakini tatizo lipo kwetu hasa hasa kwenye fikira zetu. Ukitaka kuamini hilo fuatiria kampeini zinazo endelea utaligundua hilo. Anayetakiwa kulamiwa ni anaye lea tatizo na sio tatizo lenyewe.

Hebu fikiria mgombea anatoa ahadi ya kuifanya Tanzania kuwa kama Ulaya sijui Dubai ndani ya miaka 5 na watu wanashangilia na kuamini, lakini wana sahau ya kwamba hiyo Dubai ambayo leo tunayoitamani walikuwa masikini wenzetu miaka 70 lakini leo hii wametupita zaidi ya mara 200.

Hakika ni upumbavu uliovuka mipaka kuamini aliye shindwa kuifanya Tanzania kuwa kama Dubai ndani ya miaka 60 eti ataweza ndani ya miaka 5.

Amini usismini kuna watumishi wa uma watampa magufuri kula ambaye ajawaongezea mshahara miaka 5, alafu hao hao watashinda na kukesha makanisani kwa wachungaji ili wawaombee wapandishiwe mashahara makazini mwao.

Amini usiamini kuna wasomi ambao hawana ajira na watampa Magufuli kula, na haohao watashinda na kukesha kwa waganga ili wawape dawa ya kupata ajira, hii ni mifano michache inayo onesha dhahiri ya kwamba waafirika tuna matatizo ndani ya vichwa vyetu.
Tatizo sio kwa yule anaye ongea upumbavu bali tatizo ni nyinyi mnao amini upumbavu anao uongea.

Kabla hatujawalaumu wana siasa je sisi tuna fanya nini ili kuwafanya hao wana siasa kutimiza majuku yao? Moja wapo njia ya kuwafanya wana siasa kuwa na uwajibikaji ni kuwafanya watawale kwa hofu ya kuondolewa madarakani pale wasipo fanya mambo waliyo haidi.

Watanzania tufikirie kwa kina, kusema ukweli mfumo wetu wa utawala umeferi pakubwa sana kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo yanayo sitahili kutokana na rasilimali tulizo nazo.

Na ili kubadilisha mfumo wa utawala ni lazima kwanza CCM iondoke madarakani.

Ili tupate maendeleo inabidi mfumo uwe na nguvu kuliko anaye uongoza huo mfumo, ili siku akienda kinyume na huo mfumo basi umkatae.

Yaani mfumo ndio umuamuru rais afanye nini sio yeye aumuru mfumo ufanye nini.
 
Tena mtu anahubiri kubana matumizi na wakati huohuo anamsafara mkubwa na mrefu wa watu na magari.

Kweli mada inaonesha uhalisia
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Tena mtu anahubiri kubana matumizi na wakati huohuo anamsafara mkubwa na mrefu wa watu na magari.

Kweli mada inaonesha uhalisia
Yaani mkuu ili kupata maendeleo ni lazima tubadirike tuache kulea wana siasa wa hovyo hasa wa CCM la sivyo maendeleo tutayasikia mabara mengine.
 
Kunywa soda ulipo.
Asante mkuu inabidi tubadirike.

Eti mtu aliye shindwa kuchimba mitaro ya kupitishia maji kipindi cha mvua kwenye la Dar ndio huyo anaye waambia ataigeuza kuwa London na watu wanamuani.
 
Kweli aisee,

Ndio maana mimi huwa naamini maadui wa nchi hii ni ujinga na wanae wawili ambao ni umasikini na maradhi.

Maana uujinga unafanya watu waone serikali haina faida kwao,watu kwa ujinga wanaamini kuwa C ni mali yao.

Kwa ujinga watu wanaamini magufuli ni mzalendo eti kabadlisha mikataba ya madini ili hali aliipitosha yeye akiwa sehem ya baraza la mawaziri 1998.

Ni ujinga wetu ndio hutupoonza, Watanzania tubadilike
 
  • Thanks
Reactions: RTI
Back
Top Bottom