- Thread starter
- #21
Mkamap,
Unaposema miundombinu unamaanisha vitu gani?..
maanake nijuavyo ni hizi NGO zinazochimba visima, sehemu wanazoweka kambi zao huwa hazina maji, umeme, shule wala Hospital na watatumia vigezo hivi kuomba fedha zaidi...Ni umaskini unaowapa nguvu ya NGO hizi kujijenga sehemu ambayo haina miundombinu hata Marekani huwezi kukuta NGO Manhatan kusaidia maskini ila utasikuta huko kusikokuwa na hizi miundombinu..
Halafu ktk maswala ya miji ebu rudia huko nyuma wewe umeandika vitu gani kama sio kuitaja miji..sasa umerukia maswala ya shule kuwa ni maendeleo hivi mkuu unataka kunambia kwamba Watawala wazungu walikuja jenga shule zipi?...Au unataka kusema wakristu dhidi ya waislaam na ndiko nilijua unataka sana kwenda. Nijuavyo mimi shule zile zimejengwa kwa mfuko wa dini kutusaidia maskini na sio kutuendelea na sio mzungu mkoloni aliyetutawala sawa sawa kabisa na mwarabu wa Oman ambaye alikuja tawala tu.
Mkuu jivunie kilicho chako, ulichojenga wewe kuliko misaada inayokudhalilisha maanake hata huyo Mjarumani alituacha na reli tu, Muingereza ndio hakujenga kitu kabisa..labda unazungumzia maghorofa ndio maana nikaweka mifano ya miji!
Mkuu hii mada haina mpango kabisa na nimechangia tu kutaka kukuonyesha wazi kwamba pamoja na ufinyu wake ni muhimu tupeane darasa...
Mkandara
kila maada ni pana maana kuna msemo unasema mwisho wako ama wangu ndio mwanzo wangu ama wako.
Mkandara lazima utambue uaarabu si UISLAMU na UISILAM si uarabu ,Hili ni tatizo kubwa ambalo waarabu wamepata kuwainginza baadhi ya waislamu wenye miono mifupi ili wapate suport za kimunkali.
Mwarabu anapokua anatofautiana na nchi husika anachota akili za watu kwa kusema ni vita dhidi ya UISLAMU.
Ndivyo hivyo BUSH alijitahidi kuteka akili za watu kwa kuhusisha watu fulani ni ma GAIDI.
Mkuu mimi hapa naongelea WAARABU kama WAARABU usijitahidi kujibu kwa hisia zako tofauti na kichwa cha thread,.
Nimesema ili kutibu gonjwa letu la umasikini lazima tujue historia ya umasikini na mimi nikaskuti nikaona sababu ni waarabu na inabidi tuanzie hapo kupata mwarobaini.Sababu ya ufisadi weka pembeni yani kama const na kukutaka wewe na wengine tutoe sababu zaidi.
Nashangaa kwa maneno yako eti nasifia wazungu na majengo sijui umeyatoa wapi??
Ama hoja pana kwako ni lazima niseme CHENGE fisadi ,CCM hoi itashindwa uchaguzi mdogo taarime??
Hoja hapa ni sehemu walipokalia waarabu kutoka OMAN ina lag behind ukilinganisha na sehemu zingine. kielimu, kimuondo mbinu ,kimuonekano nk,