Umasikini Tanzania tuwalaumu Waarabu au sisi wenyewe?

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
WANANET
Pamoja umasikini wetu unasababishwa na vigezo vingi lakini mimi naona WAARABU ni moja ya kigezo kikuu cha umasikini,sijui waliacha nini?

Ukiangalia sehemu ambazo Tanzania waarabu walikaa kwa wingi ni masikini kulinganisha na sehemu zingine
ukiangalia mikoa Kigoma,Lindi,mtwara,tabora,zanzibar,tanga- hii mikoa imekaliwa na waarabu na badala ya kwenda mbele hua inarudi nyuma.Na ukija kwenye vijiji pia wilaya waraabu walipobobea napo hali ni hiyo hiyo BAGAMOYO-KAOLE,IGUNGA,BUKENE-tabora, KAYENZE -mwanza,OLD SHINYANGA.
Mifano mingine unaweza wewe mwenyewe kua shuhuda fikria tu sehemu walipo kua waarabu wengi harafu ulinganishe na kwingine.

Na ukiangalia Tanzania wenda ndio nchi afrika chini ya jangwa la sahara iliyokaliwa na waarabu wengi kutoka omani na hivyo kuifanya nchi masikini.

Mimi nashauri turudi ktk historia tuone ni nini waarabu walitenda? Maana uzoefu onaonyesha kila wanapopita wanacha umasikini na badala ya kwenda mbele sehemu hiyo hua inarudi nyuma.
 
Last edited by a moderator:
Mkamap,
Mkuu naona sasa umeishiwa au ndio sponsership ya wacheza kandanda imedata sasa unatafuta mchawi!
Hivi ni mikoa gani iliyokua tajiri?...na twambie wana utajiri gani.
 
Mkamap,
Mkuu naona sasa umeishiwa au ndio sponsership ya wacheza kandanda imedata sasa unatafuta mchawi!
Hivi ni mikoa gani iliyokua tajiri?...na twambie wana utajiri gani.

Mikoa hiyo iko chini ukilinganisha na mikoa mingine na ukiingalia utaona kuna waarabu wengi walipita hapo.
Yani maendeleo yake ni mwendo wa kinyonga ama inarudi nyuma kabisa.

Wewe tafuta tu kakijiji kengine kalikokaliwa na waarabu hua kanarudi nyuma nyuma mpaka kanaachwa hoi.

Hizo mikoa ama sehemu zilipaswa kuendelea zaidi ,maana zinasababu ya kuendelea na badala yake zinarudi nyuma TANGA,BAGAMOYO,LINDI,KIGOMA,ZANZIBAR ni miji mikongwe ,kama Nchi kongwe Misiri na Palestina.
Misiri ilipaswa kua imepiga hatua ya ajabu kwenda mbele maana wao wamestaarabika karne ya 72 zilizopita na ndio maana ndunia yote tupo karne ya 21 lakini misri ipo karne ya 72.
 
Nimekuuliza ni mikoa gani hiyo yenye maendeleo?.. iseme vipi inakuwa ngumu au niseme Kilimanjaro!...haya nambie maendeleo ya mkoa huo maana sijui ni kipimo gani umetumia kuyaona hayo maendeleo ktk kipimo chako..Nina hakika kabisa Kilimanjaro haina maendeleo ya aina yoyote unayotaka wewe kuliko mkoa wa Mwanza kwa sababu kulikuwa nama kuna waarabu wengi Mwanza kuliko Kayenze...
 
Mwanza kuna maendeleo na waarabu hawakua kwa wingi mjini wapo hako kamjii kazamani lakini maendeleo ndiyo hivyo tena.

Arusha huwezi linganisha na bagamoyo ama tanga
Moshi huwezi linganisha na miji maarufu kama bagamoyo na pangani. Huko lindi na mtwara kwenye masoko yao huwezi linganisha na Mbeya ama Bukoba

kuna sehemu tabora walipokua wamejazana LUBUBU,IDALA,BUKENE,URAMBO nenda uone

Nenda SINGINDA MANYONI ukaifananishe na KAHAMA ama GEITA.

Mwanza sehem za GUNDU ,KISESA waarabu wamepita pita.

KAGERA-buziyombo, bwanga na kwingine.

Kigoma kwenda sumbawanga ujiji ,mpanda na kwingine.

Umeshafika BAGAMOYO ?? hasa Kaole sehemu walipokua makao makuu yao??

Sijafika mbeya ,iringa ,na kwa wazee wa rizombe lakini nafikiri majibu yatakua yanafanana fana sana sehemu walipopita waarabu .Nitajaribu kuwaulizia wa kongo nione kama na wao sehemu ya mashariki mwa kongo upande wanaoongea kiswahili na wamanyema kama kuna maendeleo sawia upande wa walingara.
Huku Kisangani miji maarufu yakina TIP TIP ilitakiwa nayo iwe juu huko DRC lakini wapi bwana sehemu alipopita mwaarabu du shaka tupu.
 
Mkamap,
Mkuu naona sasa umeishiwa au ndio sponsership ya wacheza kandanda imedata sasa unatafuta mchawi!
Hivi ni mikoa gani iliyokua tajiri?...na twambie wana utajiri gani.

Thank you Mkandara! Theory nyingine jamani!!!!
 
mkamap,
Mkuu hata sikuelewi kabisa.. nenda Brazil sehemu kama Sao Paulo au Rio huwezi kulinganisha na na miji yoyote Marekani ukiaacha NY na pengine Chicago lakini huwezi kunambia kuna maendeleo huko kuliko Marekani. ndio maana nauliza unatumia kipimo gani?..Nenda Maputo sidhani kama kuna mji wowote ktk Afrika unaweza kulinganisha nao ukiondoa South Afrika lakini sidhani kama Msumbiji imeendelea sana kuliko sehemu nyinginezo...sehemu hizi zimejengeka kuliko hata kwa mkoloni mwenyewe Portugal. Ndio maana nauliza unatumia kipimo gani cha maendeleo?..
Waarabu imekuwa Nongwa mbona leo Dubai, Saudi, Qatar na hata Oman zipo juu ya nchi kibao za Ulaya? Je unachojaribu kusema hapa ni kitu gani haswa maanake hata mtoto aliyelelewa na kukulia Dar anaweza kusema ana maendeleo kuliko mtoto wa Moshi ukitazama mavazi na jinsi wanavyojiweka.. lakini je hayo ndio maendeleo au?.. sasa nambie hao Word Vision na NGO zote za kutoa misaada kwa watoto maskini zimejaa sehemu gani? maanake hawa jamaa hufuata sehemu zenye dhiki zaidi...na kama Umaskini ni moja ya kipimo cha maendeleo basi hatuna haja ya kuendelea wakati kipimo kipo!
 
Mkandara
wewe usihusishe emotional zingine ;
Hapa naongelea waarabu kama waarabu na sivinginevyo ninachojaribu kusema hapa waarabu ktk utawala wao walikua komba komba hata ukoko hawabakizi na wala hakujishughurisha mfano na ujenzi wa shule,miundo mbinu na vitu kama hivyo.
Miundo mbinu yetu mingi imejengwa na wakoloni wakizungu ,vyuo mashule,zahanati wakoloni wa kizungu navyo wamechangia sana.

Lakini hawa waarabu kazi yao ilikua ni kuuza tu watu wala hawakujishughurisha sana nakutusaidia ktk mazingira hayo.

Umasikini unapimwa na miundo mbinu, vyuo, shule za kutosha yani elimu.

Nitajie sehemu gani palipo na miundo mbinu mibovu Usiposema KIGOMA,MTWARA,LINDI,TABORA basi utakua mnafiki, Na tanga inasaidiwa tu kwa kua ni uelekeo wa Moshi,Arusha ,mwanza na Kenya.

Ukiambiwa ni sehemu gani kulipo na shule chache na usipotaja hiyo mikoa basi nitashangaa.

wala sina haja ya kukuelezea unajua ila basi tu.

Hata hizo shule sijui shauri tanga,tanga tech na zinginezo hapo tanga ukizifuzatilia kwa makini utakuta ni middle school za mission ,sina uhakika sana

Tabora napo fuatilia tu TABORA boys, MIRAMBO zote zilikua mission school.

Ninachosema hapa unielewe WAARABU hawakufanya kitu chochote cha maendeleo na ndio maana sehemu walipokaa kuna lag behind maana walipaacha patupu.Na umasikini wetu moja ya sababu kuu ni waarabu walivyoondoka waliacha patupu zaidi ya kutuibia na kutuzaririsha.
 
Mkama p naona umeishia na hoja, lete hoja zenye sense. This is a total nonsense

hiyo ni hoja mkuu ,Unajua hata daktari hawezi kukutibu bila kumpa historia ya ugonjwa.Ni ngumu kwenda kwa daktari na ukamwambia unaumwa bila kumpa historia maana atashindwa aanzie wapi.

Inabidi kabla ya kutibu tatizo la umasikini wetu uijue barabara historia ya umasikini ili upate kuruka viunzi.

Najua wengi tutasema umasikini ni ufisadi wa viongozi ,na kuingia mikataba isiyo ya kimstakbali ni kweli hii ni moja ya sabau lakini sio sababu kuu.

Mwl Nyerere mimi naamini hakua mfisadi japo alikua na mapungufu yake na amekaa 24 years kama Rais lakini umasikini uko pale pale, wameenda mpaka JK naye akakili hajui tatizo letu la umasikini ni nini?
Hivyo mimi nimeskuti na kuona ni waarabu ,wewe unadhani nini ukiachilia ufisadi wa baadhi ya viongozi??
 
Mkandara

Hiyo hoja yako ya mji sio sahihi kabisa na mashirika ya misaada sio kabisa,wenye mashirika nao wanapenda kuishi sehemu iliyo na miundo mbinu fresh.

Hata kama hujafika sehemu hizo kujionea miundo mbinu ,kipimo ambacho kipo karibia na usahihi wa masikini na utajiri wa maeneo ni.

Elimu hua inaendana kabisa na utajiri ama umasikini na palipo na umasikini elimu mara nyingi hua duni na palipo na uhaueni elimu kidogo hua ahueni.

sasa basi fuatilia matokeo ya jumla ya mikoa hizo kwa shule za misingi na secondary ,na hicho nikipomo tosha.
 
Mkamap,
Unaposema miundombinu unamaanisha vitu gani?..
maanake nijuavyo ni hizi NGO zinazochimba visima, sehemu wanazoweka kambi zao huwa hazina maji, umeme, shule wala Hospital na watatumia vigezo hivi kuomba fedha zaidi...Ni umaskini unaowapa nguvu ya NGO hizi kujijenga sehemu ambayo haina miundombinu hata Marekani huwezi kukuta NGO Manhatan kusaidia maskini ila utasikuta huko kusikokuwa na hizi miundombinu..
Halafu ktk maswala ya miji ebu rudia huko nyuma wewe umeandika vitu gani kama sio kuitaja miji..sasa umerukia maswala ya shule kuwa ni maendeleo hivi mkuu unataka kunambia kwamba Watawala wazungu walikuja jenga shule zipi?...Au unataka kusema wakristu dhidi ya waislaam na ndiko nilijua unataka sana kwenda. Nijuavyo mimi shule zile zimejengwa kwa mfuko wa dini kutusaidia maskini na sio kutuendelea na sio mzungu mkoloni aliyetutawala sawa sawa kabisa na mwarabu wa Oman ambaye alikuja tawala tu.

Mkuu jivunie kilicho chako, ulichojenga wewe kuliko misaada inayokudhalilisha maanake hata huyo Mjarumani alituacha na reli tu, Muingereza ndio hakujenga kitu kabisa..labda unazungumzia maghorofa ndio maana nikaweka mifano ya miji!
Mkuu hii mada haina mpango kabisa na nimechangia tu kutaka kukuonyesha wazi kwamba pamoja na ufinyu wake ni muhimu tupeane darasa...
 
Mkuu hebu tueleze hoja yako ipo wapi? Umasikini munaletwa na kutawaliwa na Mwarabu au Mwarabu hakutengeneza sehemu alizozitawala?

Kama hoja yako kuwa umasikini unakuja kwa kutawaliwa na Waarabu, nafikiri tusingewalaumu Waarabu bali sisi wenyewe kwani Waarabu walikwishaondoka na kuwaachia Wazungu wakati tulipopata Uhuru mwaka 1961. Baada ya uhuru kulikuja Ujamaa nao pia ulishindwa kuleta maendeleo na ushahidi unaonyesha kuwa kule kulikokuwa hakuna harakati za Ujamaa ndio sehemu zinazoonyesha maendeleo.

Kati ya Sehemu ambayo ilitawaliwa na Mwarabu kwa muda mwingi na umetowa mfano ni Zanzibar. Naogopa kusema kuwa pengine huijui Zanzibar. anzibar hadi tunapata uhuru 1961ilikuwa mbele kimaendeleo kushinda sehemu nyingi za Afrika Mashariki. Kudorora kwa maendeleo ya Zanziba kunaltwa na mfumo wa Ukandamizaji wa Muungano. Zanzibar iliendelea kiuchumi na kijamii sana sana kuliko sehemu nyingi za Tanzania. Si busara kueleza hali zilivyokuwa tofauti kati ya pande mbili hizi kwani pengine itasababisha kupelekana nje ya mada.

Ama kama hoja yako ni kueleza kuwa Waarabu hawakuzitengeneza sehemu walizozitawala nakubaliana nwe kwani hiyo ndio utamaduni wao. Kwao wao hata nchini mwao (wanabadilika sasa kutokana na hali ya kilimwengu) haweana tabia ya kujenga majengo makubwa makubwa. Utamaduni wao hawana haja ya kujenga sehemu nyengine kama za burudani kwa vile wao hukaa wenyewe kwa wenewe basi. Hivyo sioni sababu kwa nini tusiwe tumeshajijengea makazi mazuri iwapo makazi mazuri ni maendeleo.

Hata hizo sehemu zilzojengwa vizuri zilifanywa hivyo kwa faida ya Watawala na sio wananchi na ndio maana Waingereza waliijenga zaidi Kenya kwa kuzingatia kuwa ni sehemu nzuri kwa wao kuishi.
Kwa hivyo mtazamo wangu nahisi umasikini wetu tusiubebeshe kwa Waarabu kwa kuwachagua wao tu bali kama ukoloni ulikuwa kikwazo kwa maendeleo yetu bali tuwaseme kwa ujumla wao.
 
Mkamap ni mchokozi lakini ukiondoa Ngekewa, naona hoja yake mnaikwepa! Kwani maendeleo ni maghorofa? Au hali ya maisha ya wananchi wake? Ukiangalia nchi zinazoongoza katika hali bora za wananchi wake zote ni za Nordic, Canada, Uswis na viinchi kama Luxembourg na Liechtenstein. Kwa kigezo cha ubora wa maisha ya raia zake nchi za kiarabu ziko nyuma.Nchi za kiarabu zitaweza kuzipita nchi za ulaya kama Albania (ya kiislamu) na Romania (ya kikristu).

Hadi ilipopata uhuru Zanzibar haikuwa tajiri au na maendeleo kama Kenya. Lakini katika nchi zote hizi mbili maendeleo yalikuwa kwa tabaka la watawala, kwa Kenya wakoloni na Zanzibar waarabu na wahindi. Hapo kwetu kweli sehemu zinazokaliwa na waarabu au tuseme waislamu ziko nyumba kimaendeleo. Cha kujiuliza ni je wakoloni ambao walikuwa ni wakristu walifanya jitihada gani kupeleka maendeleo katika sehemu hizi? Au waliwatosa kwa sababu hawakuwa wamisheni?
 
Tanzania nzima kwa ujumla wake tu maskini. Kwamba sehemu moja iliendelezwa ama laa halina maana sana baada ya miaka zaidi ya 40 ya uhuru. Swali lakujiuliza sio waarabu au wazungu walifanya nini katika sehemu ipi kuwa maskini.

Swali ni nini sisi kama watanzania tumefanya kwa miaka 40 ya kuwa huru, katika kujiletea maendeleo? Iwe Tabora iko ilikuwa nyuma au Dar au Tanga swala ni je kwa miaka 40 iliyopita tumefanya nini kujikwamua?

Haya mambo yakuishi kwenye nyakati zilizopita hayatatufikisha kokote. Tuishi nyakati za sasa. Tuko huru taifa huru, je tunafanya nini kujiletea maandeleo? Sio sijui waarabu... huku ni kutapa tapa. maana kama nikurudi nyuma zaidi, basi kulikuwa na falme ambazo zilikuwa tajiri zaidi ya nyingine TZ. hapo utasema machifu wao walifanya nini?

Jamani tuamke tumpambane na haya ya sasa. Daktari haitaji kujua kama miaka 40 iliyopita uliumwa malaria, anataka kujua unafanya nini sasa hivi kujizuia na mbu?
 
WANANET
Pamoja umasikini wetu unasababishwa na vigezo vingi lakini mimi naona WAARABU ni moja ya kigezo kikuu cha umasikini,sijui waliacha nini?

Ukiangalia sehemu ambazo Tanzania waarabu walikaa kwa wingi ni masikini kulinganisha na sehemu zingine
ukiangalia mikoa Kigoma,Lindi,mtwara,tabora,zanzibar,tanga- hii mikoa imekaliwa na waarabu na badala ya kwenda mbele hua inarudi nyuma.Na ukija kwenye vijiji pia wilaya waraabu walipobobea napo hali ni hiyo hiyo BAGAMOYO-KAOLE,IGUNGA,BUKENE-tabora, KAYENZE -mwanza,OLD SHINYANGA.
Mifano mingine unaweza wewe mwenyewe kua shuhuda fikria tu sehemu walipo kua waarabu wengi harafu ulinganishe na kwingine.

Na ukiangalia Tanzania wenda ndio nchi afrika chini ya jangwa la sahara iliyokaliwa na waarabu wengi kutoka omani na hivyo kuifanya nchi masikini.

Mimi nashauri turudi ktk historia tuone ni nini waarabu walitenda? Maana uzoefu onaonyesha kila wanapopita wanacha umasikini na badala ya kwenda mbele sehemu hiyo hua inarudi nyuma.

Wacha kutafuta watu wa kulaumu wewe. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa!
 
Wacha kutafuta watu wa kulaumu wewe. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa!

Kwanza karibu JF....
Pili...HESHIMA HOJA NZITO....

Ni wazi hatuwezi kuijadili Afrika bila ya kujadili wahamiaji ambao walileta culture zao,Kututawala na kutupeleka UTUMWANI....

Sitaki kuanza kuingia kwenye mjadala huu...Ila sitokubali juwe na watu wene mawazo ya kifisadi na intimidation.

Toka nijiunge hapa jf nimejifunza mengi sana.

Kwa mfano wakati wa hoja za EPA na Ballali pamoja na nyinginezo...Nilipata UPINZANI zaidi ya huu wa Mkamap na tena karibia kila respected member hapa jf aliniona kama sina hoja na waliniponda kwa sana tu.

Lakini matokeo yake mmeyaona...Ballali HAKUNA na EPA ni kesi ya madai...Na mdeni HAFUNGWI.

Hivyo wewe unayesema unafanya research ya kisayansi...Ni bora urudi maabara na SIASA UWAACHIE WENYEWE.
 
Back
Top Bottom