Umasikini ni nini?

Gigo

JF-Expert Member
Aug 6, 2006
456
46
Kama Mswahili-una Akili kiasi hiki.basi tuanze Kuona Mafanikio- tumechoka kusubiri-!
Lakini,Hatuwezi kuendelea kwa Kasi hiyo..Twendeni 'hatua kwa hatua'-Tutengeneze mambo ya msingi-Ulinzi na Usalama- Hapo-nikiwa nina maanisha Elimu yetu-Ufahamu wetu,Lugha yetu,Sisi na wenzetu!,Upendo wetu,Amani yetu,Hekima yetu,Furaha yetu,Ujuzi wetu,na kila kilicho chetu...

Chakwetu ni furaha yao,hao wasio wenzetu!!.........nao hao ni- Wakina nani?

Ona tunavyo Cheka- nahii ni kwasababu tuna fahamiana,Ona tunavyo Chukia hii ni kwasababu tuna heshimiana.

Maisha ni Magumu, lakini lazima iwe ni Changa moto kwetu-badala ya kua maisha ni shida, umasikini,taabu na mateso.
kabla sijaendelea Hivi Umasikini ni nini?
 
Ukitaka kujua umaskini ni nini, inabidi kwanza ujue kutokuwa maskini ni nini? Uwezo wa kumudu maisha ya chini kabisa (yaani kupata chakula kizuri, malazi mazuri, elimu, mavazi na usafiri mzuri na wa hakika), kuwa na uhakika wa kupata matibabu mazuri unapoumwa, uwe na uhakika wa kupata mapumziko na burudani baada ya kazi, uwe na uhakika wa maisha yako na kupata mahitaji hayo kwa walau miezi mitatu. Hapo unaweza kusema kuwa wewe sio maskini. Kama huwezi kupata hayo basi upo kwenye kundi la maskini kama mimi au unakaribia kwenye kundi la maskini.
Lakini kuna wengine wana-definition tofauti ya maendeleo, kwa na wanawake wengi, kunywa pombe na kula nyama mpaka utoke jasho, kuwa na gari la kisasa huku huna hata pa kulala, kuvaa nguo tofauti kila siku na cheni kubwa ya dhahabu, sasa inategemeana na uwezo wako wa kufikiri. Unaweza kuwa maskini na ukajiona si maskini kutokana na unavyofikiri na unaweza kuwa si maskini lakini ukajiona maskini kutokana na unavyofikiri.
 
Nikitaka kuulezea umaskini vema nitaelezea pesa ni nini kwanza. Pesa ni ubunifu wowote unaosimamiwa na kujiamini kwako. Unapokuwa na wazo zuri la kibiashara au la maendeleo na unapokuwa na confidence ya kulitekeleza kama inavyotakiwa then wewe una pesa. Wewe ni tajiri. Kinyume cha hapo wewe ni maskini.
 
Wewe Mswahili..Hufikirii Kwamba-Unaweza Ukawa na fedha Kiasi furani lakini bado ukawa masikini!!...Kuna tofauti gani kati ya Tajiri wa mtaa wetu na mtaa wa jirani?
 
Nakubaliana na wazo kuwa 'umaskini wa mtu unatokana na kiwango anachoweza kufikiri juu ya mahitaji yake na kuyatimiza'. Mtu anaweza kuwa na hela nyingi lakini akajikuta ni maskini ukilinganisha na mahitaji yake, hali kadhalika mtu anaweza kuwa hana fedha, lakini akawa tajiri kulingana na mahitaji aliyonayo kwa wakati huo. Kumbe umnaskini ni 'subjective'siyo 'objective'. Ndiyo maana tajiri wa kijijini kwetu au mtaani kwetu, ni maskini wa kijiji au mtaa mwingine kwa tafsiri na muonekano wake!
 
Mimi ntaelezea jinsi nnavofahamu umaskini.

Umaskini ni ule kwamba huna mahala pazuri pa kuishi (nyumba) nzuri yenye umeme,maji na choo kitumiacho maji, mlo wa mara tatu-asubuhi ,mchana na jioni.

Pia umaskini ni pale ambapo baada ya kutumia pesa ya ujira ulioipata kihalali kwa kulipia labda umeme,maji, na manunuzi ya chakula, unakuwa huna uwezo wa kununua vitu muhimu kama mavazi na masuala yote yahusianayo na utanashati na urembo na mengine ambayo kwa shingo upande tunasema ni anasa.

Pia umaskini ni pale ambapo sasa ndio unashindwa hata kumsomesha mtoto shule kwa kumlipia ada tangu aanze shule ya awali mpaka aingie chuo kikuu na awe na uhakika wa ajira.

Mwisho umaskini ni pale unaposhindwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kijamii na kujiona umetengwa kama kushiriki katika jambo forums na kukosa habari muhimu zinazoendelea mahala unapoishi kama ni Buzwagi na nje ya Buzwagi mpaka Dar-es-Salaam na nje ya mipaka ya nchi yako na kuona habari za kimataifa na kujifunza na kuwa na upeo na uelewa wa masuala mbalimbali yawe ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Baada ya kuelezea umaskini ni budi kuangalia chanzo chake.

Ukiachailia mbali sababu kama za kiasili za hali ya hewa na mazingira au labda za kijiografia ambapo hapa pana vitu kama ardhi, madini, na mali asilia zingine, umaskini unasababishwa na watu waliochaguliwa katika jamii na kupewa thamana ya kuongoza.

Kwa sababu ukiangalia jiographia na nikitoa mfano wan nchi yetu Tanzania,sehemu kubwa ya ardhi ni yenye rutuba kubwa tu na maji huwa yapo ukiondoa vipindi vichache vya ukame ukifananisha na Darful ambako hakuna uhakika mvua itanyesha lini.

Kwa hiyo hapa serikali imeshindwa kuondoa umaskini kwa kukosa mipango madhubuti ya kumuendeleza mkulima wa mazao ya biashara kama kahawa, chai na pamba na kushindwa kumsaidia kutokana na sababu ingine ya kuwepo kwa mfumo wa kibepari ambao ndio hupanga bei.Hivo basi, serikali inashindwa kupanga njia zingine mbadala za kumnyanyua mwananchi na kumwacha aendelee kuwa maskini wa kutupwa kimapato, kifikra na kimaono

Kwa hiyo basi hapa umaskini wa mtanzania mkulima umekuja kwamba hapati malipo ya mazao yake kwa bei halali na huishia kupata pesa ya kuganga njaa kama chakula kidogo na kwenda kutoa sadaka kanisani na kushindwa kupeleka watoto shule na mambo mengine kama kuamua kwenda kwenye klabu cha pomoni kuondoa mawazo.

Chanzo kingine cha umaskini ni maradhi mbalimbali kama ukimwi, vita na uhalifu. Hili la vita ndio linachangia kwa kiasi kikubwa kuleta umaskini.

Katika taarifa yake leo shirika la misaada la Oxfam limeeleza katika taarifa yake leo inaoitwa "Africa Missing Billions", kwamba tokea mwaka 1990 jumla ya paundi bilioni 150 zilipelekwa barani humo kama msaada na hazionekani zimesaidia nini na waafrika zaidi ya milioni tano wamekufa.

Ukimwi unachangia kumaliza idadi ya watu ambao ndio wanategemewa kufanya kazi na kuleta tija na hivo kuacha nyuma idadi ya watoto,au wazazi na mzigo wa watoto kwa hio ile "productive force" ya nchi inakuwa inapungua na matokeo uzalishaji viwandani unapungua na umaskini kuongezeka. Pia uhalifu unaweza kuchangia umaskini kwa kuangalia tukio la Ditopile la kumuua yule kijana dereva. Yule kijana alikuwa anawakilisha idadi ya watu maskini ambao wameamua kuwa njia ya udereva angalau inawasaidia wao kupata chochote na kuwasaidia kidogo familia, ndugu, jamaa na marafiki. Lakini kwa kumnyang'ny'a haki ya kuishi mtu kwanza ndugu Dito amekiuka agizo la katiba kwamba mtu kila mtanzania anahaki ya kuishi.

Vyanzo vingine vifuatavyo ndio babu kubwa katika kushindilia umaskini popote pale duniani.

Kukosekana kwa utawala wa sheria kunafanya umaskini ushamiri karika jamii yoyote ile. Kwenye utawala wa sheria inaaaminika kwamba hakuna mtu alie juu ya sheria na watu wote wanawajibika kuheshimu utawala wa sheria.

Kwa mfano wananchi wa Buzwagi wana haki kikatiba na kisheria kuifikisha mahakamani serikali au mbunge wao kwa kushindwa kuetetea maslahi yao kama wamilikiwa mgodi wa Buzwagi pamoja na serikali.

Katika sehemu ya tatu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano kuna kifungu kinachoelezea Wajibu Wa Jamii ,kipengere cha 27 kinasema- Kulinda Mali Ya Umma.

Kwa hio hapa wananchi wa ama Buzwagi au sehemu ingine nchini Tanzania au nje ya Tanzania wote wana wajibu wa kulinda mali ya umma mojawapo ikiwemo migodi ya madini.

Kukosekana kwa demokrasia ni chanzo kingine cha umaskini. Katika nchi inaondeshwa kidemokrasia utawala wa sheria unakuwepo pale watu wanapokuwa na haki ya kujua serikali yao walioichagua na kuipa dhamana ya kuongoza kama kweli inafanza hivo. Ukiangalia katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano kifungu kinachoelezea Serikali na watu sheria ya 1984 Namba 16, ibara ya sehemu ya nane inasema kwamba: nanukuu,

8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.-

mwisho wa kunukuu


Kwa hio hapa kama kuna namna yoyote ile ya kwenda kinyume na maagizo ya katiba yetu hii basi umaskini ni wa milele.
Wananchi wametaka kujua kuhusu suala la Buzwagi na ni hatua zipi zitachukuliwa kuhusu watuhumiwa, hivo kinachotegemewa ni polisi kuachiwa wafanya kazi yao ya kuchunguza tuhuma hizo na hatimae sheria ichukue mkondo wake badala ya kujaribu kuziba midomo wale wanaohoji uhalali wa kutia saini mikataba ambayo imejaa kila dalili za rushwa.

Chanzo kingine ni rushwa ambayo kwa nchi kama Tanzania bado tuna safari ndefu na wanaokamatwa ni visamaki vidogo tu na ilhali wachezaji mashuhuri wanajulikana.

Vyanzo vingine ambavo nafikiri nisiongelee sana kwa maana kwamba wasomaji na wana JF wengine wanaelewa ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha elimu ambapo mfano unaonekana sasa kwamba viongozi na watu wengine wenye fwedha wanaamua kupeleka watoto wao nje kwenye elimu bora katika nchi kama India, Uingereza,USA na South Africa.

Chanzo kingine cha mwisho ni miundo mbinu. Kama hakutakuwa na (carpet) barabara za kuwezesha wananchi kusafiri na kufanya biashara bila mikwara ya mashimo na majambazi humo njiani. Kwa mfano wananchi wa mikoa ya kaskazini magharibi wanaweza kusafiri kwenda Dodoma kwa kutumia masaa machache kama kutakuwepo na lami ya nguvu. Lakini nilipokuwa naangalia blog ya Mjengwa na kuona barabara za kwenda mikoani zilivo na taabu, hapo nasema watanzania tuna kazi kwelikweli.

Jamani nimejitahidi kwa maelezo yangu haya mareefu lakini nimeongelea umaskini, sasa namna ya kuondoa huo umaskini ndio tuendeleze mjadala.

Naomba kutoa hoja.
 
Nakubaliana na wazo kuwa 'umaskini wa mtu unatokana na kiwango anachoweza kufikiri juu ya mahitaji yake na kuyatimiza'. Mtu anaweza kuwa na hela nyingi lakini akajikuta ni maskini ukilinganisha na mahitaji yake, hali kadhalika mtu anaweza kuwa hana fedha, lakini akawa tajiri kulingana na mahitaji aliyonayo kwa wakati huo. Kumbe umnaskini ni 'subjective'siyo 'objective'. Ndiyo maana tajiri wa kijijini kwetu au mtaani kwetu, ni maskini wa kijiji au mtaa mwingine kwa tafsiri na muonekano wake!

Wewe Mswahili Hili Neno Subjective Lina maana gani?

Kupambana na umasikini sio ni kama kupambana na mila na Utamaduni wetu? Nauliza swali!!
 
"Poverty is a condition in which a person or community is deprived of, or lacks the essentials for a minimum standard of well-being and life. ..."
sourse, wikipedia.org

Umasikini ni hali ambayo binadamu anashindwa kupambana na mazingira[Ukosefu wa chakula,huduma ya matatibabu...] ni vigumu kuupima umasikini kwa fedha.

Chanzo kikubwa cha umasiki ni pale uchumi unapolala na mgawanyiko wa kazi unapokoma[division of labour]

Jamii ya kale
Kulingana na historia jamii hii ilikuwa na mgawanyiko mkubwa wa kazi, walikuwepo wakulima,wafua chuma,waganga wa jadi,wafugaji, viongozi nk. makundi yote haya yalitegemeana na walibadilishana bidhaa kwa kadri ya mahitaji.
mfano, ili kupata matibabu ulitakiwa kutoa kiasi fulani cha mavuno yako kwa mganga ili upate matibabu, mfua chuma alibadilishana zana za chuma na mfugaji akatoa ng'ombe, katika kipindi hiki japo walikuwa hawana fedha lakini umasikini ulikuwa ni kiwango cha chini sana.

In order to understand poverty on reservations, you must first understand the people. In order to understand the people, you must understand the Culture

...This land belongs to us, for the Great Spirit gave it to us when He put us here. We were free to come and go, and to live in our own way. But white men, who belong to another land, have come upon us, and are forcing us to live according to their ideas. This is an injustice; we have never dreamed of making white men live as we live.

Sitting Bull, September 1881
 
Ona Mswahili Unavyo yajua yote haya!!Lakini Mbona magonjwa Huya husishi na umasikini?
 
Kazi Kweli kweli....UMASIKINI NI UJINGA!! Full stop
 
inasemekana kwamba hakuna mmasai hata mmoja aliyewahi kufa kwa blood pressure, kisukari au mishutuko. hii inatokana na ukweli kwamba mmasai alale nje, ndani yote sawa. ale chakula kibichi kilichopikwa yote sawa.
milikutana na mswidish mmoja kijijini kwetu akawaangalia watoto yatima na kusema kuwa pamoja na shida zao, still they looked happier than his fellows in sweden.
kikubwa umaskini ni kutokujiamini na kuridhika na hali halisi ya maisha na mambo na badala yake ukatamani na kujiona mkosaji.
umasikini ni lack of happiness and freedom
 
Just picked this up from the web, John scazi's, being poor

September 03, 2005

Being Poor

Being poor is knowing exactly how much everything costs.
Being poor is getting angry at your kids for asking for all the crap they see on TV.
Being poor is having to keep buying $800 cars because they're what you can afford, and then having the cars break down on you, because there's not an $800 car in America that's worth a damn.
Being poor is hoping the toothache goes away.
Being poor is knowing your kid goes to friends' houses but never has friends over to yours.
Being poor is going to the restroom before you get in the school lunch line so your friends will be ahead of you and won't hear you say "I get free lunch" when you get to the cashier.
Being poor is living next to the freeway.
Being poor is coming back to the car with your children in the back seat, clutching that box of Raisin Bran you just bought and trying to think of a way to make the kids understand that the box has to last.
Being poor is wondering if your well-off sibling is lying when he says he doesn't mind when you ask for help.
Being poor is off-brand toys.
Being poor is a heater in only one room of the house.
Being poor is knowing you can't leave $5 on the coffee table when your friends are around.
Being poor is hoping your kids don't have a growth spurt.
Being poor is stealing meat from the store, frying it up before your mom gets home and then telling her she doesn't have make dinner tonight because you're not hungry anyway.
Being poor is Goodwill underwear.
Being poor is not enough space for everyone who lives with you.
Being poor is feeling the glued soles tear off your supermarket shoes when you run around the playground.
Being poor is your kid's school being the one with the 15-year-old textbooks and no air conditioning.
Being poor is thinking $8 an hour is a really good deal.
Being poor is relying on people who don't give a damn about you.
Being poor is an overnight shift under florescent lights.
Being poor is finding the letter your mom wrote to your dad, begging him for the child support.
Being poor is a bathtub you have to empty into the toilet.
Being poor is stopping the car to take a lamp from a stranger's trash.
Being poor is making lunch for your kid when a cockroach skitters over the bread, and you looking over to see if your kid saw.
Being poor is believing a GED actually makes a goddamned difference.
Being poor is people angry at you just for walking around in the mall.
Being poor is not taking the job because you can't find someone you trust to watch your kids.
Being poor is the police busting into the apartment right next to yours.
Being poor is not talking to that girl because she'll probably just laugh at your clothes.
Being poor is hoping you'll be invited for dinner.
Being poor is a sidewalk with lots of brown glass on it.
Being poor is people thinking they know something about you by the way you talk.
Being poor is needing that 35-cent raise.
Being poor is your kid's teacher assuming you don't have any books in your home.
Being poor is six dollars short on the utility bill and no way to close the gap.
Being poor is crying when you drop the mac and cheese on the floor.
Being poor is knowing you work as hard as anyone, anywhere.
Being poor is people surprised to discover you're not actually stupid.
Being poor is people surprised to discover you're not actually lazy.
Being poor is a six-hour wait in an emergency room with a sick child asleep on your lap.
Being poor is never buying anything someone else hasn't bought first.
Being poor is picking the 10 cent ramen instead of the 12 cent ramen because that's two extra packages for every dollar.
Being poor is having to live with choices you didn't know you made when you were 14 years old.
Being poor is getting tired of people wanting you to be grateful.
Being poor is knowing you're being judged.
Being poor is a box of crayons and a $1 coloring book from a community center Santa.
Being poor is checking the coin return slot of every soda machine you go by.
Being poor is deciding that it's all right to base a relationship on shelter.
Being poor is knowing you really shouldn't spend that buck on a Lotto ticket.
Being poor is hoping the register lady will spot you the dime.
Being poor is feeling helpless when your child makes the same mistakes you did, and won't listen to you beg them against doing so.
Being poor is a cough that doesn't go away.
Being poor is making sure you don't spill on the couch, just in case you have to give it back before the lease is up.
Being poor is a $200 paycheck advance from a company that takes $250 when the paycheck comes in.
Being poor is four years of night classes for an Associates of Art degree.
Being poor is a lumpy futon bed.
Being poor is knowing where the shelter is.
Being poor is people who have never been poor wondering why you choose to be so.
Being poor is knowing how hard it is to stop being poor.
Being poor is seeing how few options you have.
Being poor is running in place.
Being poor is people wondering why you didn't leave.



Posted by john at September 3, 2005 12:14 AM
 
inasemekana kwamba hakuna mmasai hata mmoja aliyewahi kufa kwa blood pressure, kisukari au mishutuko. hii inatokana na ukweli kwamba mmasai alale nje, ndani yote sawa. ale chakula kibichi kilichopikwa yote sawa.
milikutana na mswidish mmoja kijijini kwetu akawaangalia watoto yatima na kusema kuwa pamoja na shida zao, still they looked happier than his fellows in sweden.
kikubwa umaskini ni kutokujiamini na kuridhika na hali halisi ya maisha na mambo na badala yake ukatamani na kujiona mkosaji.
umasikini ni lack of happiness and freedom

Hii Kali...tena nzuri...lakini hebu ngoja..
 
Kupata Suluhisho Lenye Kudumu la Umaskini
IJAPOKUWA kuna ripoti mbaya kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni kuhusu umaskini, kuna wale ambao wana matumaini kwamba jambo fulani linaweza kufanywa. Kwa mfano, kulingana na kichwa kimoja katika gazeti la Manila Bulletin, Benki ya Maendeleo ya Asia ilisema kwamba “Asia inaweza kumaliza umaskini katika muda wa miaka 25.” Benki hiyo ilipendekeza ukuzi wa uchumi kuwa njia moja ya kuwatoa watu kutoka katika dimbwi la umaskini.

Mashirika mengine na serikali zimetoa mapendekezo na miradi mingi ya kujaribu kutatua tatizo hilo. Baadhi ya mapendekezo hayo ni: mipango ya bima ya jamii, elimu bora, kufuta madeni ambayo nchi zilizositawi zinazidai nchi zinazositawi, kuondoa vizuizi vilivyowekwa ili mataifa yenye idadi kubwa ya watu maskini yaweze kuuza bidhaa zao katika nchi za nje, na kujenga nyumba za gharama ya chini kwa ajili ya maskini.

Katika mwaka wa 2000, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliweka miradi inayopaswa kutimizwa kufikia mwaka wa 2015. Miradi hiyo ilitia ndani kukomeshwa kwa umaskini mkubwa na njaa, na vilevile tofauti kubwa ya mapato katika mataifa. Hata miradi hiyo iwe mizuri kadiri gani, wengi wanatilia shaka kwamba itatimizwa katika ulimwengu huu usio na umoja.
 
Back
Top Bottom