Umasikini ni laana, masikini ni kiumbe hatari, masikini ni mtaji wa watawala masikini

Ngoja nikutafutie zile nyuzi zako za flexible nikuletee humu maana siku hizi umeadimika mkuu....kwa hiyo ninapokupata ndio hapo ñakukabàdhi yale ya mwaka 2012
 
Asilimia 98 ya matajiri hutajirika kwa njia ambazo zifuatazo:
1. Kukwepa kulipa kodi
2. Kulipa mishahara midogo kwa wafanyakazi
3. Magendo
4. Kutoa roho za watu

Kwa maana hiyo basi, ndio maana yule jamaa kutoka Nazareth akasema ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu.

Ni asilimia chache sana za umaskini zinasababishwa na mtu mwenyewe, ila kwa asilimia kubwa umasikini ni tatizo la kimfumo ambalo vizazi na vizazi hujikuta wametumbukia.

Matajiri, na vibaraka wa matajiri hua wanataka kuwaaminisha watu kua umasikini ni laana wakati wao ndio chanzo kikubwa cha tatizo la umasikini.

Ila kiukweli kabisa Mungu amefanya agano na masikini, hata yule jamaa wa nNazareth aliwaambia baadhi ya matajiri wauze mali zao zote wawape masikini, maana yake ni kwamba wanamiliki mali ambazo sio haki yao!!!!

Hivi majuzi tu dunia imetoka kusikia kua asilimia moja ya watu fulani wa dunia wanamiliK karibu ya nusu ya utajiri wa dunia.

Hata shetani ameweka mitihani yake kwenye utajiri wa mali, iweje msemaje tajiri ana mafungamano na Mungu??
Kwa uelewa wetu ni kwamba, labda mungu mnayemmaanisha hapa ni shetani, shetani ambaye amefanya agano lake juu ya utajiri wa mali
Kwa maana hiyo basi,
Yeriko nyerere na wapambe wengine wote mnaopiga kelele juu ya hawa matajiri mnatekeleza ajenda ya shetani kama sio kumuabudu shetani.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tabia ya watu maskini hupenda kuona matajiri kufilisiwa na ongezea maskini ni watu wavivu sna kazi yao ni majungu na kujadili wenzao.
 
Hapa Mm Sijaelewa Ki2 Hapa Huyo Mnayosema Ni Maskin Amekuwa Maskini Kwakunyonywa Na Mafisadi Wanaokumbatiwa Na Serikali,inakuwaje Tna Awe Na Laana?
 
Sipendi Tabia Ya Kuwafilisi Matajiri Kwajili Ya Maskini,kila Mtu Afanye Kwa Jitahada Zake Bila Kumyonya Mwenzake
 
Wakati sisi matajiri tunatoa misaada , masikini wanakazana kulogana ! Kwa mujibu wa maandiko matakatifu Umasikini ni dhambi mbaya sana .
 
Kuna tajiri mmoja amehodhi akili za maskini waTZ na anazidi kuwaaminisha kuwa umasikini wao umeletwa na matajiri, halafu maskini hao kwa ujinga wao wanashangilia kweli wakiskia tajiri fulani kashushwa. Wamefikia hatua ya kufurahia hata pale wafanyakazi wa umma kunyimwa nyongeza za mishahara kwao ni furaha kwa sababu watalingana. Hayo ndo mawazo ya maskini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unachokifanya ni sawa na mtu anayerusha jiwe kwa woga, halafu anajificha kusikiliza nini kitatokea.
Sidhani kama kunamtu atakuja tilia maanani threads zako, kesho hatujui utasimamia wapi.
 
Hugo anaeiba godoro masaki n.a. anae iba godoro tandale yupo atapika polisi yipi atauwawa fikiria uwezo kiuchumi wa wakati wa maeneo hayo na nani anatenda ipasavyo
 
Kwanamna yoyote, masikini ni kiumbe mwenye roho mbaya sana duniani, masikini ndie hunena baraka kwa tajiri, lakini laana zake kwa tajiri ni mauti kwake tu.

Masikini wengi weusi hasa wa Tanzania wanaamini umasikini wao umesabanishwa na matajiri, furaha yao kuu nikuona tajiri anafilisiwa au kufilisika.

Kifalasafa masikini hana nafasi mbele ya ufalme wa Mungu, kwa kila lepe, Mungu huwachukia masikini, na hawa masikini ndio wachawi wa dunia hii.

Ni laana kubwa mtu kujisifu kwa umasiki wake au kuuishi na kuutumia umasikini wa watu kumiliki na kutawala.. Mungu hana maagano na masikini abadani hasilani.

Wanenwao wengi ni masikini wa akili na roho zao, hawa ni fimbo ya matajiri na kuni za masikini totoro watamanio Bakheresa awe kama wao sio wao wawe kama Bakheresa.

Laana kubwa ni kuwashusha matajiri wawe masikini ukitaraji uwanja wa masikini utakuwa barabara, katu masikini hawana ngazi za kuwapandisha wawe matajiri. Utajiri sio usomi, utajiri sio madaraka, Hakuna msomi aliyesoma mpaka elimu ya juu kabisa kule nera na akaufikia utajiri....Utajiri ni karama, ni mapaji yake maanani, sawa na huyu mfupi, yule mrefu

Hakuna masikini aliyewahi kutajirika kwa kumchukia tajiri... Kubwa zaidi huambulia mauti. Masikini ndie kiumbe mwenye dhambi zaid hapa duniani. Masikini hana dhamana, haaminiki popote na yoyote. Kumwamini masikini nikutotambua nguvu ya tumbo.

Kinyonge hakitaiona pepo!!!!

Na Yericko Nyerere

View attachment 564505
Ngonjera zako ni tamu ila awamu hii zitafaa tu kuwa TANZIA kwa matajiri fisadi dhidi ya jamii maskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tajiri mmoja amehodhi akili za maskini waTZ na anazidi kuwaaminisha kuwa umasikini wao umeletwa na matajiri, halafu maskini hao kwa ujinga wao wanashangilia kweli wakiskia tajiri fulani kashushwa. Wamefikia hatua ya kufurahia hata pale wafanyakazi wa umma kunyimwa nyongeza za mishahara kwao ni furaha kwa sababu watalingana. Hayo ndo mawazo ya maskini

Sent using Jamii Forums mobile app
Naaam naaam
 
Kwa hiyo ndo kutwambia mnayajutia mahubiri yenu ya kuwaita baadhi ya matajiri ambao baadhi yenu wamekuwa viongozi wakuu wa chama chenu mafisadi?

Pointi ni moja tu, consistency katika sera zenu na mahubiri yenu ni muhimu sana. Watanzania wameamua kuishi na mtu mkweli, anayeishi uhalisia wake. [HASHTAG]#Unafiki[/HASHTAG] katika siasa mwisho basi.
 
Back
Top Bottom