Umasikini na utamaduni ni changamoto katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
16 days 2.jpg

Moja kati ya maadui wakubwa wa taifa letu na nchi ya Tanzania ni umasikini, umasikini ambao umekuwa ni tatizo Katika familia nyingi za mijini na vijijini, umasikini ambao unatokana na matatizo mbalimbali ambayo yanahitaji kutatuliwa kwa Pamoja ili kuondokana na hali hiyo.

Watu wengi waliopo Katika hali ya umasikini ndio waathirika wakubwa wa matatizo ya Ukatili wa Kijinsia na unyanyasaji,kuna wakati mtu anakubali kufanyiwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia siyo kwa kapenda, hapana, ila ni kwa sababu hana Jinsi ya kufanya na hivyo anaona kama akitendewa kitendo cha Ukatili wa Kijinsia na unyanyasaji inaweza kuwa sababu ya kupunguza umasikini na shida zake.

Asilimia kubwa ya wanaofanyiwa Unyanyasaji wa kingono ni wale ambao wanaamua kutumia njia hiyo kama njia mbadala ya kupunguza hali yao ya umasikini na wanaofanya vitendo vya Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia kwa watu masikini, wanafanya hivyo wakijua kabisa kuwa wanaemfanyia Ukatili huo hana sehemu ya kukimbilia kwa sababu ya shida zake na binadamu shida zikimzidi sana anaamini kuwa kaumbiwa shida, hili nalo tatizo.

Wale wanaofanyiwa Ukatili wa kimwili, kama ni masikini anajikuta akiishia kuvumilia tu Ukatili huo kwa sababu hata akichukua uamuzi wa kwenda kushtaki atakuwa kajiharibia ama anaamini kuwa kushtaki kwake kufanyiwa vitendo vya Ukatili kutamnyima fursa Fulani Katika Maisha yake.

Umasikini unachangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza kwa vitendo vya Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia hii ni kwa sababu sauti ya masikini haisikiki vyema Katika Jamii, sauti ya masikini ni kama kivuli tu, pakipitishwa mwanga wa fedha sauti hiyo inafifia.

Jamii sasa inahitaji uwezeshaji kielimu na kiuchumi ili kukabiliana na matatizo ya Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia, lakini ni nani wa kuweza kuiwezesha Jamii kuondokana na umasikini ili kuutokomeza Ukatili wa Kijinsia, kila mmoja atakuwa na jibu lake.

Lakini tuangalie , Mapambano dhidi ya Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia, yanahitaji fedha, lakini siyo fedha tu, pia yanahitaji utayari wa Jamii Katika kukataa vitendo hivi vya Ukatili.
Utamaduni wetu, ukichanganywa na umasikini, unachangia kuwepo kwa matatizo ya Ukatili na unyanysaji wa Kijinsia,

Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vitaendea vikibadilika kila siku , yote ni kwa sababu binadamu ni kiumbe kinachoamini Katika kutungiwa sheria ili azivunje na siyo ili azitelekeze
Utamaduni siyo dini , eti tuamini kuwa hauwezi kubadilika,utamaduni ni maamuzi ya watu wachache waliokaaa kulingana na mtazamo na zama zao, na wakaamua kuwa jambo Fulani lifanyike vipi.

Maamuzi yao na mtazamo wao, siyo lazima uendane na zama na nyakati zetu, kama Katika nyakati zetu tutaona kuwa kitendo hiki hakifai, basi ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa Tunaweza kuondoa aina hiyo na utamaduni na kubakiwa na tamaduni nyingine.

Kuikataa tamadunia Fulani, haitutoi Katika utanzania wetu, wala haituvui vazi la utu wetu, kama utamaduni utakuwa ni sehemu ya kutuumiza au kuumiza wengine, basi tuutumbilie mbali utamaduni huo.

Kama utamaduni wetu utakuwa ni sehemu ya kuwaumiza Wanawake, wasichana , Watoto na vijana, basi utamaduni huo hauhitajiki na waliouleta utamaduni huo hawakuwa na malengo mazuri na Jamii yao.

Kuna wakati huwa najiuliza, Yule mtu alieamua kuwa Mwanamke akifiwa na mume wake anyanganywe mali yake, alikuwa na akili kweli au alikuwa na tamaa ya kurithi mali, unaweza kujiuliza Mwanaume gani wa leo, alielelewa Katika family iliyoamini utamaduni mbovu na Katika family isiyomjua Mungu.

Ifike wakati, Katika Mapambano haya tusiogope kuzilaumu tamaduni zetu, na tuziache kuzikata tamaduni hizo zinazotutesa ama kutesa wengine.

Mwanamke wa kweli hawezi kukukubali kufanyiwa Ukatili wa Kijinsia kama sehemu ya kuifikia fursa Fulani, huo ni uvivu wa akili na umasikini wa mawazo.

Idd Ninga
Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
View attachment 2025339

Goood analysis though kuna baadhi ya watu wanaachwa nyuma
 
Back
Top Bottom