Umasikini na utajiri, akili na mazingira

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
Karne nyingi barani Ulaya kabla ya kuzaliwa Kristo palipata kuwepo watu wenye akili kubwa waliowaza mbali pengine waliendeleza mawazo na falsafa zilizopata kuwepo hata kugundua vitu kama Simu, Magari,ndege hata nishati ya Umeme.

Tulipata kuwashuhudia watu maarufu duniani waliofanya gunduzi mbalimbali kama akina Michael Faraday, Albert Einstein, Aristotle, Alexander Bell, Isac Newton, Macnon na Wanafalsafa mbalimbali wakubwa.

Tulipofanya utafiti tuliambiwa lishe inamsaidia sana mtoto kuwa na akili kubwa yenye kuwaza mbali hata kufanya ugunduzi hapo baadae lakini tafiti inapingwa na tafiti,Sasa miaka hii ambayo kwa ulaya na Amerika chakula kimeboreshwa sana kiubora hatuoni watu wenye akili kubwa kama zamani.

Kwa sasa Wajapan ndio wanaoongoza kuwa na akili kubwa mno na hii ni sababu ya kula sana vyakula vya asili wakiepuka sana vyakula vya kupandikiza kwa kutumia kemikali.

Kama suala la chakula pekee ndilo linalofanya mtu anakuwa na akili kubwa basi Mkoa wa Morogoro ungeongoza kuwa na akili kubwa ukifuatiwa na Mkoa wa Mwanza,Ruvuma na Iringa.Mikoa hii ndio yenye vyakula haswa nao wangekuwa wengi vyuoni ila sivyo ilivyo mpaka sasa.

-Akili na vinasaba vyetu.

Mojawawapo ya sifa za moja kwa moja za kuwa na akili kubwa ni kurithi kutoka kwa wazazi.

Kuna kizazi (jamii) ambayo vinasaba vya akili ya kuwaza mbali vinatawala katika kufikiri na kuwaza kwao wakati vinasaba vingine akili kubwa ya kufikiri na kuwaza mbali imezidiwa na tabia nyingine za mwanadamu.

Bado nampa sifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kufanya mchanganyiko wa makabila mbalimbali ili kuweza kupata jamii bora yenye akili itayoishi pamoja bila kutengana.

Maeneo yote ya Taifa la Tanzania yalifanyiwa upgrading kati ya jamii moja na jamii nyingine, Kutokana na jamii ya Kaskazini mwa Tanzania kupelekwa kusini mwa Tanzania na jamii ya Magharibi ya Tanzania kupelekwa Mashariki.

Mchanganyiko huo ulionuia kuondoa ukabila ukaleta faida kwa upande wa kibaiolojia pakafanyika crossbreeding kwa maana ya mtu wa kusini kumuoa mtu wa Kaskazini na uzao wao ukaleta jamii moja yenye uwezo mkubwa wa akili ya kuwaza mbali kwa maana ya IQ.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa mambo yote ya kurithi ni ya asili na hivyo hubadlishwa kwa njia hizo hizo.

-Akili kubwa inavyohusishwa na dini,kabila na Ukanda.

Mtu mwenye akili kubwa anaweza kuwepo katika dini na kabila lolote lile kiasili ila anaweza kutojulikana kwa sababu ya mazingira yanayomzunguka na jamii anayoishi nayo.

Suala la Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa kuwa wengi katika nyanja za elimu linatokana na suala la kihistoria la Wamishenari wa dini ya kikristo kufika katika maeneo hayo na kuanzisha shule za kueneza utamaduni wa kizungu kumfanya mtu awaze kama wao.

-Kufaulu darasani hususani kwenye elimu hii ya kukaririshana iliyoletwa na Wamishenari wa kizungu haina uhusiano wowote na akili kubwa.

Sisi watu wa Pwani au Mimi Mbena, Mluguru wa Matombo, Morogoro kwa ujumla hatufanyi vizuri darasani,Wamishenari walichelewa kufika kueneza elimu ya kukaririshwa darasani kwa kuwa kipindi hicho maeneo yote ya Pwani,Morogoro na Tanga yalishikiliwa na Waarab,

Sasa sahau zile porojo za watu za kuhusisha madrasa na kutokuwa na akili ya kukaririshwa darasani kwani ni Waislamu wachache sana wanaoenda madrasa na ukikutana na mtoto wa madrasa anayependa shule lazima awaburuze darasani katika elimu ya kukaririshwa na Wamishenari,

Ikiwa mtu anameza Msahafu je atashindwa nini kumeza History book au kumeza fomula za kemia,fizikia na hisabati,Hivyo basi sababu kubwa sio makabila fulani hayana akili bali ni historia na mazingira ndiyo yenye kusababisha akili kubwa.

-Tanzania nzima tunafanya mtihani mmoja wa darasa la saba,form four na form six.

Kwa darasa la saba alama za kufaulu kwenda sekondari ni tofauti mikoa na mikoa hii inajirudia kwenye dhana ile ile ya sehemu zilizowahi kuanza na Wamishenari katika elimu ya kukaririshwa darasani na zile sehemu zilizochelewa kufikika na Wamishenari,

Sasa alama za ufaulu zinakuwa tofauti sehemu na sehemu ili kuendana na hali ya kuwahi na kuchelewa kwa Wamishenari, kwa kufanya hivi kunasaidia Watanzania wote kupata fursa sawa za kuendelea kielimu.

Tungetumia alama sawa, shule zote za sekondari nchini, zingejaa watu wa baadhi ya makabila tuu, au baadhi ya maeneo, wakiwemo Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa ambao waliwahi kufikiwa na Wamishenari na kuwahi kufundishwa elumu ya kukariri darasani,

Hivyo basi kuna makabila na maeneo, wasingegusa kabisa secondary kutokana na ile hali na hamasa ndogo miongoni mwao iliyotokana na kuchelewa kuja kwa Wamishenari walioeneza elimu ya kukaririshwa darasani.

-Makabila Tajiri na Makabila Masikini.

Kuna makabila tajiri kwa Ufugaji,Kilimo na Madini,lakini pia kuna makabila yaliyonyuma kimaendeleo na yaliyoendelea (Primitive Tribes na Advanced Tribes)
Tanzania japo tuna makabila 120, makabila haya hayalingani, kuna makabila makubwa, na kuna makabila madogo (the biggest tribe or the giant and the smallest) kati ya hayo makabila 120 ya Tanzania, kabila kubwa ni Wasukuma na kabila dogo ni Hadzabe.

Uwezo wa akili za makabila haya unatofautiana, hivyo kuna advanced tribes, developed tribes na primitive tribes, hawa developed tribes wana akili zaidi za dasani kuliko the primitive tribes, lakini when it comes to intelligence, kuna primitive tribes wako more intelligent kuliko developed tribes, mfano the Masai are the best in alternative medicine, na ndio wana the best birth control, hawazaliwi vilema, wala zeruzeru!.

Baadhi ya advanced tribes hadi kuzungumza kwa kilugha wanachomekea kimombo kidogo, mfano " mugambire inafu", "anigambire fulishi infront of my wife", wengine.

Hawa developed tribes unakuta hadi vijijini wana nyumba bora, maji ya bomba na umeme, wakati wengine bado wanaishi kwenye tembe!. Jee akili zitafanana?.

Viwango Tofauti vya Ufaulu, Wengine Wana Akili, Wengine Vilaza!'
Tulipopata uhuru, nchi zote zinazotawaliwa na Uingereza, tulifanya mtihani mmoja tuu wa Cambridge, ulitungwa London, hivyo ni watu wa baadhi tuu ya makabila waliweza kufauli kuingia sekondari.

Tukadhania ni kwa sababu mitihani inatungwa London, hivyo tukaachana na mitihani ya London, tukaanzisha NECTA, tukatunga mitihani yetu, bado tukakuta ni baadhi tuu ya makabila wanafanya vizuri, hivyo tukiendelea hivi kuna makabila shule wataushia kuisikia tuu.

Ndipo Nyerere akaamua kubadili viwango vya ufaulu, ili kila Mtanzania asome na elimu ilikuwa bure.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuwasomesha kwa nguvu watoto 4 wa kabila la Wahadzabe, wote walifeli darasa la saba, lakini akalazimisha waende sekondari kwa lazima. Wakasomea pale Pugu, na wote wanne walipata Divisheni Zero!.

Tuulizane kidogo,hivi umewahi kusikia Mwanafunzi bora kitaifa katoka Zanzibar? Au Zanzibar hakuna Div I, Div II, wala Div III , Wao ni Div IV na Div Zero Tuu?!

Kama ni hivyo jibu ni lile lile kuchelea kwa Wamishenari au kutofika kabisa kwa Wamishenari kueneza elimu ya darasani ya kukariri. Waarabu wao waliwekeza sana kwenye kupanda minazi ambayo inaisha miaka 50 hadi 100 na kuzaa kila mwaka,hii ilisababisha umwinyi.

-Umasikini wa Kanda na Mikoa,Historia ya Tanzania na influence ya wakoloni.

Mikoa ya Bukoba, Kilimanjaro, Mbeya ni mikoa iliiyobahatika kupata shule za kwanza baada ya wazungu kuleta elimu.

Zanzibar na Tanga ilimezwa na utamaduni wa kiarabu kabla ya uzungu.

Utamaduni wa waarabu kwa wakati ule ulikuwa ni biashara na biashara zao nyingi ilikuwa utumwa na kilimo cha minazi. Minazi ikitunzwa vizuri hukaa kwa miaka 50-100. Hivyo ili fanya wazee wapumzike.

Kwa nini nimetaja Bukoba,Kilimanjaro na Mbeya kwa sababu kuna idadi kubwa sana ya Wananchi walio wasomi tangu enzi hizo kwasababu taasisi hizo za elimu, dini na afya zilianzishwa katika mikoa hiyo, mfano Kilimanjaro, Mbeya, Kagera na hata Arusha pia kuna taasisi nyingi za elimu za wakoloni.

Mikoa ya Pwani iliyochelewa kufikika na Wamishenari (kasoro wagogo tu) ndiyo inayoonekana kuwa na uelewa mdogo kama Mtwara, Lindi, Kondoa(kwa warangi), Wanyaturu,Tanga,Dar es Salaam,Morogoro,Zanzibar.

-Akili kubwa ni tofauti na akili unayofundishwa darasani.

Naamini kama mfumo wa kupata ajira Tanzania ungejumuisha aptitude test kwa maana ya kupima kiwango cha akili ya kuwaza mbali katika ubongo basi wengi wangekosa ajira,

Naamini scores za watu wengi zisingefikia kiwango cha IQ kubwa kwa kuwa elimu iliyokichwani ni ya kukariri na kuwa Mwanasheria kama ndugu yangu Richard.

Hivyo basi kuna uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha IQ ya mtu nikimaanisha akili, na umasikini tulionao Watanzania . Maeneo yenye umasikini uliopitiliza, IQ za wengi ziko chini yaani low IQ au akili ndogo.

Umasikini na kufeli, Mkoa tajiri wanafaulu sana, Mikoa masikini wanafeli sana,Sasa angalia level ya umasikini ukanda wa Pwani, ukijumuisha na Zanzibar, mikoa ya Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara, au makabila yenye umasikini uliopitiliza kama Wagogo, Warangi, Wanyaturu, Wabarbaig, Wasandawe, Wataturu, Wahadzabe, Wazaramo, Wandengereko etc,

Sasa linganisha na mikoa yanye neema ya kufikiwa haraka kwa Wamishenari ambao walijenga shule nyingi kwa ajili ya kueneza elimu ya darasani na utamaduni wao.

Mikoa ya Kilimanjaro, Bukoba, Mbeya, Iringa, Mwanza, angalia akili za kukariri zilivyochangamka na kuenenda kama wenye IQ kubwa mfano Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa etc,

Bila kusahau kabila kubwa Tanzania, Wasukuma, watu wanaokula vizuri, wanakuwa na IQ kubwa kwa maana ya akili kubwa, Makabila ya mlo mmoja, wanakuwa na low IQ kwa maana ya akili ndogo.

Nimalizie kwa kusema mtu mwenye IQ kubwa kwa maana ya akili kubwa ya kuwaza mbali, anaweza kuwepo katika kabila lolote lile kiasili iwe limewahi kufikiwa na Wamishenari au limechelewa,iwe kwenye kabila la Waluguru au Wachaga tatizo linakuja kwenye kutambulika na kujulikana kwasababu ya mazingira yanayomzunguka na jamii anayoishi nayo.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Una proof yoyote wazaramo wana umasikini uliopitiliza?

Alafu IQ ni nini na inatumia vigezo gani?
 
'mfano the Masai are the best in alternative medicine, na ndio wana the best birth control, hawazaliwi vilema, wala zeruzeru!.'

Ni alternative medecine ipi iyo?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom