UMAR Ibn Al-Khattab na Paul (SAUL wa Tarso): Mashujaa wa imani mbili Kinzani...

But the Lord said to him, “Go, for he is a chosen vessel of Mine to bear My name before Gentiles, Kings and the children of Israel. I will show him how many things he must suffer for My name’s sake.”
acts 9:15
alipewa na Yesu waliewapa mitume wengine.
Na huyu anania alikuwa ni nani.mpaka akamshika paulo akaona tena?
 
Jamaa alimuua kwa sababu zake binafsi.
Kwa sababu Umar alikuwa mtu wa haki, Huyu mtumwa aliyekuwa muhunzi wa vyuma alienda kumshtaki bosi wake aliyekuwa anamtumikia apunguze kumnyonya maana jamaa alijipatia pesa nyingi kupitia yeye.
Umar akamwambia awe Mvumilivu.
Jamaa Hilo jibu hakulipenda, akakasirika sana na kumchukia Umar. akatengeneza jambia kisiri, na akanunua Sumu ambayo alihakikisha inaua akaliloweka kwenye sumu jambia na akamvizia Umar akiwa kwenye sala.
Akamtoboatoboa vibaya sana. Waliokuja kusaidia aliua makumi kadhaa kumbuka kile kisu kikikugusa tu unakufa maana kina sumu. walimzidi ujanja akajiua.

Inaonekana ilikuwa ni Issue personal mkuu.
hii ni kulingana na vyanzo mbalimbali...

Alitengeneza jambia akaua kwa kisu mbona statement zinajicontradict,halafu kama kutengeneza hilo jambia ilikuwa ni siri ilikujaje kujulikana wakati alifanya siri? Je aliitoa hiyo siri mwenyewe?,je alijiua siku hiyohiyo aliyomuua huyo nabii,je kama ni siku hiyohiyo alipata mda wa kutoa siri kabla hajajiua?
 
Alitengeneza jambia akaua kwa kisu mbona statement zinajicontradict,halafu kama kutengeneza hilo jambia ilikuwa ni siri ilikujaje kujulikana wakati alifanya siri? Je aliitoa hiyo siri mwenyewe?,je alijiua siku hiyohiyo aliyomuua huyo nabii,je kama ni siku hiyohiyo alipata mda wa kutoa siri kabla hajajiua?
jamaa alikuwa Mfua vyuma, Jambia/Kisu ni kitu anachokitengeneza bila shida...
stori hizi zinasimuliwa na waliokuwepo enzi hizo. Pia yule alikuwa kiongozi mkubwa sioni sababu ya ile jamii kushindwa kutrace back tukio. Siri anaweza asitoe yeye, kipindi hicho vifo vya namna hiyo vingi tu. Hata Caliph wa mwisho Ali nae alichomwa na kisu cha sumu msikitini hivyo hivyo na maadui...
 
Mkuu unataka kusema watu siku hizi hawaendi kutambika kwa sababu ya ukristo na uislamu?
Ndio kwa kiasi kikubwa dini kama ukristo inakataza inakataza matambiko ni dhambi ya ushirikina. Una abudu miungu (Worshipping idols). Hata ktk uislam itakuwa inakatazwa.
 
Ndio kwa kiasi kikubwa dini kama ukristo inakataza inakataza matambiko ni dhambi ya ushirikina. Una abudu miungu (Worshipping idols). Hata ktk uislam itakuwa inakatazwa.
Hayo matambiko pamoja na hizi dini zote ni mambo ya imani,na ndiyo maana kuna wengine hawaamini hata hizo dini. Hivyo huwezi kulaumu dini bali ni uamuzi wa mtu kuamua kuamini dini na kuacha kufuata matambiko kama ambavyo kuna wasioamini dini wala matambiko.
 
ni kweli kuna utofauti,maana hata hz ni dini mbili ni tofauti
kuna tofauti[/QUOTE]
 
Umar ibnl-Khatwab (Allah amridhie) moja kati ya maswahaba wakali sana na wenye jazba katika maswahaba wa mtume(s.aw), pia wanamuita Al-faruk ndie aliyefarakanisha makafir katika kuufuta msafala wa mtume siku mtume na wafuasi wake walipohama kutoka makka kwenda madina. wakati makafir wanaufuatilia msafala kwa ajili ya kuwafanyia shari waislam, umar alisimama na kuwaambia "kama miongoni mwenu kuna anayetaka kumuacha mke wake awe mjane na wanawe wawe yatima basi na aendelee kutufuata" makafir walirudi nyuma kwa kuogopa vitisho vyake. Historia ya umar ni historia ya mazingatio sana kwa umma wa kiislam na watawala wake.
 
Je katika ulimwengu huu kuna utofauti gani kijamii,kiuchumi,kiimani na kwa ujumla kati ya kafiri na asiyekuwa kafiri?
Hapo kwenye imani tofauti imekuwa ni kubwa sana mkuu. Waislam wanaamini mungu mmoja, ALLAH na mtume wake aliyetumwa kwa walimwengu wote, mtume MUHAMMAD(S.W), waislam pia wanaamini ISSA au MESIAH ibn mariam ni nabii wa Allah na ni neno kutoka kwake na kukanusha vikali na kwa hoja zenye dalili ya kuwa SIO MUNGU na kuamini katika utatu ni kufuru iliyo ya wazi na kumzulia Allah uongo kuwa ana mtoto. Hii ni tofauti kwa wakristo ambao wao hayo matatu ya juu wanayaamini kinyume chake.
 
Paul aliifanya kazi ya kuineza injili akiwa mtu wa kawaida sana, asiye na ushawushi wa kiutawala wala kifedha, bali alijawa na imani na kuwafanya watu kumuamini kwa kuyafurahia matendo yake. Pia aliifanya hii kazi kwa tabu sana, akiteseka sana na hata baadaye kuuawa. Huyu mwingine alikuwa mtawala na hivyo alitumia mabavu na ushawishi wake kiutawala kuueneza uislamu. Pia hakupitia mateso yoyote katika kazi yake bali ndiye aliyetesa wengine wasiokuwa wa dini yake
 
Back
Top Bottom