UMAR Ibn Al-Khattab na Paul (SAUL wa Tarso): Mashujaa wa imani mbili Kinzani...

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
2,000
Habarini za jioni wanaintellijensia na watu wa kufikiri katika nyuzi 360 kwa kila jambo.

Kama kuna kosa kubwa tunafanya ni kushika imani bila kujua japo historia kiduchu ya tulikotoka.
Dunia ya Imani imegawanyika katika makundi mawili makubwa yasiyoingiliana yaani Waislamu na Wakristo.

Paul (SAUL wa Tarso):

Historia inaonyesha Komandoo wa imani ya kikristo na mpambanaji aliyepitia kila aina ya changamoto ni PAULO aliyeitwa Sauli. Hakuna kuanzia matendo ya Mitume hadi Ufunuo hadi kesho aliyeonyesha viwango vya Paul.
Muda mwingi utamkuta kwenye boti akisafiri huku na kule, asia,ulaya,afrika kaskazini, mashariki ya kati kueneza injiri kwa ushawishi mkubwa usio na mfano.
Hakuna kama paul katika Ukristo.
Alikuwa msomi aliyetukuka linapokuja suala la elimu dunia, Hakuwa mtu wa majivuno.
Huyu kwa kazi aliyoifanya, na maandiko aliyoandika sio tu wapinzani wa ukristo yamewachanganya bali hadi wakristo wenyewe wakijikuta ktka makundi makundi kiasi cha mtu aliyekuwa mwanafunzi wa yesu PETRO kuwataadhalisha wasomaji wa maandiko yake kuwa kuna watu wasio na uelewa huyachanganya na kujichanyanya.

Mwisho wa paul, Baada ya kazi kubwa ya kusambaza Ukristo maeneo yote yenye ushawishi enzi hizo. Anakamatwa na kukatwa kichwa kama ng'ombe machinjioni. Tofauti na Ng'ombe,Mbuzi,Kitimoto au tunaowaona wakichinjwa na ISIS kwenye habari alionekana mtu mwenye furaha, kama vile Bwanaharusi anakwenda kumpokea bibi harusi.
Kifo kwake hakikuwa Tishio tena bali ni zawadi kwa kazi kubwa aliyoifanya mpiganaji huyu tayari kwa Kusubiri Taji na Medali siku ile ya Hukumu.

Haya ndio maneno yake ya Mwisho mwisho akimuandikia barua kijana shupavu Timotheo katika Usiku ule ambao wanahistoria wanasema asubuhi yake alipokea zawadi ya Kifo kwa kukatwa kichwa na shoka...
2timotheo 4:5-7
Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

UMAR Ibn Al-Khattab mtume alimuita Farouq(Distinguisher of truth and Falsehood )

Baada ya kifo cha Mtume Momammed SAW, Hakuna mtume mwingine aliyetakiwa kuwepo isipokuwa ukawepo mpango mkubwa wa muda mrefu wa kuwa na kingozi wa kidini atakayesimamia mambo ya imani na kuwa kiongozi wa dola la kiislam maarufu kama Islamic Calphate. Kiongozi wa Dora hii alijulikana kama Caliph. Katika historia Kumewahi kuwepo macaliph wanne tu tangu mtume kufariki na baada ya hapo imani iliendelea kuwepo bila ya umoja wa enzi hizo.

1:Abu Bakr.
2:Umar ibn al-Khattab.
3:Uthman ibn Affan.
4:Ali ibn Abi Talib.

Hapa tunamzungumzia Caliph wa pili kuwahi kuwepo duniani maarufu kwa jina la Umar. ZTV na nadhan Azam media wanavipidi wanaonyesha juu ya jemedali huyu na kiongozi shupavu ambae wanazuoni wanafananyisha kazi aliyoifanya katika uislam inaweza kufananishwa na PAULO kwa kazi aliyoifanya kwenye Ukristo miaka zaidi ta 500 kabla yake. Alipokea Uislam mwaka 616ACE kama SAUL Umar alikuwa katika harakati ya Kutafuta kumuua Mohammad kabla ya kukutana na watu wake wa karibu ambao tayari walikuwa wameshakuwa waislam. alishawishiwa na maneno ya quran na akajikuta nia yake ovu akiijutia na Kusilimu...

-Alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa katika mazungumzo (Public speaking), alikuwa na uwezo mkubwa sana wa ushawishi na usuluhishi,Wanahistoria wanamtaja kama mtu wa 52 kwa umaarufu duniani tangu mwanzo wa history...

Alikuwa mtu hodari kwa kusambaza Uslam. Ukiona leo waislam wamesambaa karibu dunia nzima huwezi kuwatenga na kazi ya huyu jamaa aliyejiita commander of the faithful” (amīr al-muʾminīn). Ndiye aliyebadili taswira ya Uislam kutoka kwa waarabu tu na kusambaa dunia nzima.Leo kuna waislam wachina,wahindi,wazungu,weusi n.k
Anaheshimika duniani kote kwa kutawala kwa kufuata haki. Alianzisha mifumo thabiti ya kidini na kiutawala.
Tofauti na wengi wanavyodhani, Siku walipoiteka Jerusalem, kulikuwemo na wayahudi na wakristo. Umar aliingia jijini hapo siku kadhaa baadae kwa staili ya aina yake ya kujinyenyekeza. Yaani aliingia akiwa amembeba mfayakazi wake kwenye punda huku yeye akivuta kamba ya punda yule. Kwa kiongozi kama yule watu hawakutegemea. Alipofika alitoa fundisho ambalo kwangu ni naliona kama ni la muhimu sana. Aliwaagiza waislamu wote wasimlazimishe mtu yoyote kuwa muislamu kwa lazima. bali waishi maisha mema ya mfano ili wakristo na mayahudi wawe waislamu kwa mvuto wa maisha ya waislamu wanaozunguka. aliagiza kuwe na haki sawa kwenye ardhi kwa watu wote. Aliwatoza kodi ya chini wakazi wa Jerusalem kuliko hata wakoloni waliokuwepo hapo.
Hiztoria za kuyahudi zinasema Umar japo yerusalem yote ilikuwa chini yake lakini aliwaruhusu wayahudi na wakristo kuendelea na ibada zao.

HIVI NI BAADHI YA VITU ALIVYOFANYA VYA KUKUMBUKWA
1: Historia zinasema ndiye aliyetoa wazo(kuna wananzuoni wengine wanasema yeye aliweka sheria tu lakini utaratibu ulikuwepo) la kutenganisha kwa wanawake na wanaume katika ibada ili kusiwe na matamanio na watu wajielekeze kwenye ibada tu.

2: Ni Umar aliyeifuta kabisa kazi nzuri aliyoifanya Paul middle east na maeneo ya karibu kwa kusambaza uislam kote huko.

3:wanahistoria wanasema wakati wa mwanzo waislamu walikuwa wanaabudu kwa siri, Umar ndiye aliyetoa wazo wafanye mambo yao wazi, na kuwatishia wote ambao wangewaingilia katika kusali kitu kilichosababisha mtume kuuita "AL-Farouq".

4:Umar ndie aliyeanzisha Kalenda ya Kiislam mwaka 639AD inayotumika hadi leo,

5:Kipindi cha njaa kubwa kuwa ubunifu mkubwa na akili nyingi akiwa kiongozi wa dola la kiislam aliokoa maisha ya mamillioni na watu.

6:Alikataa kuwakata mikono wezi, kwa sababu aliamini mtu aliiba kutokana na yeye kushindwa kutoa ajira kwa jamii.Kwenye utawala wake alikuwa na maono katika dola yake mtu asilale usiku akiwa hajashiba...
KIFO
kama inavyotokea mara nyingi Mashujaa wengi hufa vifo vya kawaida. Siku moja akiwa anasoma sala ya asubuhi alivamiwa na mtumwa wa kiajemi na kumchoma kisu/Jambia mara sita tumboni (vyanzo vingine vinasema mgongoni) na kumuacha damu zikibubujika ardhini na hapo ndio ukawa mwisho wa shujaa huyu katikati ya utawala. Umar sio mtu wa kawaida kwa maana ya uongozi
kuna mengi alifanya hapa wataalam zaidi wanaweza kuchambua.

karibuni,
mashehe,wachungaji, wananzuoni na maulamaa tujadili watu mashuhuri hawa katika imani hizi kinzani bila jazba, ugomvi,fitna na maneno ya kejeli.
naweza kuwa sijaweka mzigo wote ila yaliyobaki yanabaki kama changamoto na mianya kwa wachangiaji.
 
Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,479
2,000
Habarini za jioni wanaintellijensia na watu wa kufikiri katika nyuzi 360 kwa kila jambo.

Kama kuna kosa kubwa tunafanya ni kushika imani bila kujua japo historia kiduchu ya tulikotoka.
Dunia ya Imani imegawanyika katika makundi mawili makubwa yasiyoingiliana yaani Waislamu na Wakristo.

Paul (SAUL wa Tarso):

Historia inaonyesha Komandoo wa imani ya kikristo na mpambanaji aliyepitia kila aina ya changamoto ni PAULO aliyeitwa Sauli. Hakuna kuanzia matendo ya Mitume hadi Ufunuo hadi kesho aliyeonyesha viwango vya Paul.
Muda mwingi utamkuta kwenye boti akisafiri huku na kule, asia,ulaya,afrika kaskazini, mashariki ya kati kueneza injiri kwa ushawishi mkubwa usio na mfano.
Hakuna kama paul katika Ukristo.
Alikuwa msomi aliyetukuka linapokuja suala la elimu dunia, Hakuwa mtu wa majivuno.
Huyu kwa kazi aliyoifanya, na maandiko aliyoandika sio tu wapinzani wa ukristo yamewachanganya bali hadi wakristo wenyewe wakijikuta ktka makundi makundi kiasi cha mtu aliyekuwa mwanafunzi wa yesu PETRO kuwataadhalisha wasomaji wa maandiko yake kuwa kuna watu wasio na uelewa huyachanganya na kujichanyanya.

Mwisho wa paul, Baada ya kazi kubwa ya kusambaza Ukristo maeneo yote yenye ushawishi enzi hizo. Anakamatwa na kukatwa kichwa kama ng'ombe machinjioni. Tofauti na Ng'ombe,Mbuzi,Kitimoto au tunaowaona wakichinjwa na ISIS kwenye habari alionekana mtu mwenye furaha, kama vile Bwanaharusi anakwenda kumpokea bibi harusi.
Kifo kwake hakikuwa Tishio tena bali ni zawadi kwa kazi kubwa aliyoifanya mpiganaji huyu tayari kwa Kusubiri Taji na Medali siku ile ya Hukumu.

Haya ndio maneno yake ya Mwisho mwisho akimuandikia barua kijana shupavu Timotheo katika Usiku ule ambao wanahistoria wanasema asubuhi yake alipokea zawadi ya Kifo kwa kukatwa kichwa na shoka...
2timotheo 2:5-7
Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

UMAR Ibn Al-Khattab

Baada ya kifo cha Mtume Momammed SAW, Hakuna mtume mwingine aliyetakiwa kuwepo isipokuwa ukawepo mpango mkubwa wa muda mrefu wa kuwa na kingozi wa kidini atakayesimamia mambo ya imani na kuwa kiongozi wa dola la kiislam maarufu kama Islamic Calphate. Kiongozi wa Dora hii alijulikana kama Caliph. Katika historia Kumewahi kuwepo macaliph wanne tu tangu mtume kufariki na baada ya hapo imani iliendelea kuwepo bila ya umoja wa enzi hizo.

1:Abu Bakr.
2:Umar ibn al-Khattab.
3:Uthman ibn Affan.
4:Ali ibn Abi Talib.

Hapa tunamzungumzia Caliph wa pili kuwahi kuwepo duniani maarufu kwa jina la Umar. ZTV na nadhan Azam media wanavipidi wanaonyesha juu ya jemedali huyu na kiongozi shupavu ambae wanazuoni wanafananyisha kazi aliyoifanya katika uislam inaweza kufananishwa na PAULO kwa kazi aliyoifanya kwenye Ukristo miaka zaidi ta 500 kabla yake. Alipokea Uislam mwaka 616ACE kama SAUL Umar alikuwa katika harakati ya Kutafuta kumuua Mohammad kabla ya kukutana na watu wake wa karibu ambao tayari walikuwa wameshakuwa waislam. alishawishiwa na maneno ya quran na akajikuta nia yake ovu akiijutia na usilimu...

Alikuwa mtu hodari kwa kusambaza Uslam. Ukiona leo waislam wamesambaa karibu dunia nzima huwezi kuwatenga na kazi ya huyu jamaa aliyejiita commander of the faithful” (amīr al-muʾminīn). Ndiye aliyebadili taswira ya Uislam kutoka kwa waarabu tu na kusambaa dunia nzima.Leo kuna waislam wachina,wahindi,wazungu,weusi n.k
Anaheshimika duniani kote kwa kutawala kwa kufuata haki. Alianzisha mifumo thabiti ya kidini na kiutawala.
Tofauti na wengi wanavyodhani, Siku walipoiteka Jerusalem, kulikuwemo na wayahudi na wakristo. Umar aliingia jijini hapo siku kadhaa baadae kwa staili ya aina yake ya kujinyenyekeza. Yaani aliingia akiwa amembeba mfayakazi wake kwenye punda huku yeye akivuta kamba ya punda yule. Kwa kiongozi kama yule watu hawakutegemea. Alipofika alitoa fundisho ambalo kwangu ni naliona kama ni la muhimu sana. Aliwaagiza waislamu wote wasimlazimishe mtu yoyote kuwa muislamu kwa lazima. bali waishi maisha mema ya mfano ili wakristo na mayahudi wawe waislamu kwa mvuto wa maisha ya waislamu wanaozunguka. aliagiza kuwe na haki sawa kwenye ardhi kwa watu wote. Aliwatoza kodi ya chini wakazi wa Jerusalem kuliko hata wakoloni waliokuwepo hapo.
Historia zinasema ndiye aliyetoa wazo la kutenganisha kwa wanawake na wanaume katika ibada ili kusiwe na matamanio na watu wajielekeze kwenye ibada tu.
Ni Umar aliyeifuta kabisa kazi nzuri aliyoifanya Paul middle east na maeneo ya karibu kwa kusambaza uislam kote huko.
kama inavyotokea mara nyingi Mashujaa wengi hufa vifo vya kawaida. Siku moja akiwa anasoma sala ya asubuhi alivamiwa na mtumwa wa kiajemi na kumchoma visu mara sita tumboni na kumuacha damu zikibubujika ardhini na hapo ndio ukawa mwisho wa shujaa huyu

Mkuu unaweza kutupa kwa ufupi ni style/njia zipi wawili hawa walitumia kusambaza kazi walizofanya?
Sasa hapa kwenye uzi huu tuchangie nini zaidi kati ya wawili hawa?
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
2,000
Mkuu unaweza kutupa kwa ufupi ni style/njia zipi wawili hawa walitumia kusambaza kazi walizofanya?
Sasa hapa kwenye uzi huu tuchangie nini zaidi kati ya wawili hawa?
hii ni kwa ajili ya kupashana habari tu, maana ningesema niiegemeze upande flani sasa hivi pangekuwa hapakaliki, kama unaona hakuna cha kuongezea, kupinga, kukosoa,kuboresha kuhusu Manguli hawa wawili unatulia tu...
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,572
2,000
Saul au Paul hakuwa mfuasi wa Yesu wakati Yesu alipokuwa hai

Alikuwa mpinga Yesu alipokuwa Yesu yupo hai

alikuja kuwa mfuasi au kiongozi baada ya Yesu kufa
na ndio hasa muanzilishi wa Ukristo kwa maana Kanisa la Kwanza
alijenga yeye...na jina la kuwa wafuasi wa Yesu waitwe wakristo alianzisha yeye

Omar alikuwa mfuasi wa Uislam toka wakati Mtume(S A W) yupo hai
na alitazamiwa kuja kuongoza hapo baadae

kuna tofauti
 
asante kwa tofauti hizo.
Ufanano wao unakuja kwenye kazi walizozifanya kueneza imani zao japo mbinu zilikuwa tofauti.
PAUL aliupa Ukristo sura ya Kimataifa kutoka kwenye sura ya Kiyahudi zaidi,
Vivyo hivyo UMAR aliutoa uislam kwenye mazingira ya kuwa dini ya waarabu tu na kuupa sura ya Kimataifa.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,154
2,000
Wakati wengine wanagundua imani zao sijui mababu zetu walikuwa wapi.

Walikufa bila kutuachia imani, leo hii wajukuu zao wanatumia dini za watu wengine.

Dini ni kama lugha.......kama huna yako jiandae kutumia za watu wengine.
Mkuu binafsi naona kama kuna tofauti ya dini na imani,nafikiri mababu zetu hawakuwa na dini bali walikuwa na imani mbalimbali ambazo hadi leo bado zipo japo si sana. Lakini hata hivyo imani zilikuwepo na bado zipo hata huko ambapo palipoanzishwa hizi dini za uislamu na ukristo.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,293
2,000
Wakati wengine wanagundua imani zao sijui mababu zetu walikuwa wapi.

Walikufa bila kutuachia imani, leo hii wajukuu zao wanatumia dini za watu wengine.

Dini ni kama lugha.......kama huna yako jiandae kutumia za watu wengine.
Mkuu nani alikuambia babu zetu hawakuwa na dini kabla ya kuja dini hizi za mashariki ya kati? Babu zetu walikuwa wanaomba kwa miungu yao kama wafanyavyo wachina, wajapani, wakorea na wahindi. Sema sisi waafrika tumekuwa wepesi kuzipokea dini hizi za wageni kisha wakatuaminisha za kwetu hazifai. Wakati walikuwa wanatambika na mvua zinanyesha ghafla. Wenzetu wa mashariki ya mbali wao wameshikilia dini zao za asili hata baada ya ujio wa dini za wageni.
 
mamaudaku

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
707
500
Habarini za jioni wanaintellijensia na watu wa kufikiri katika nyuzi 360 kwa kila jambo.

Kama kuna kosa kubwa tunafanya ni kushika imani bila kujua japo historia kiduchu ya tulikotoka.
Dunia ya Imani imegawanyika katika makundi mawili makubwa yasiyoingiliana yaani Waislamu na Wakristo.

Paul (SAUL wa Tarso):

Historia inaonyesha Komandoo wa imani ya kikristo na mpambanaji aliyepitia kila aina ya changamoto ni PAULO aliyeitwa Sauli. Hakuna kuanzia matendo ya Mitume hadi Ufunuo hadi kesho aliyeonyesha viwango vya Paul.
Muda mwingi utamkuta kwenye boti akisafiri huku na kule, asia,ulaya,afrika kaskazini, mashariki ya kati kueneza injiri kwa ushawishi mkubwa usio na mfano.
Hakuna kama paul katika Ukristo.
Alikuwa msomi aliyetukuka linapokuja suala la elimu dunia, Hakuwa mtu wa majivuno.
Huyu kwa kazi aliyoifanya, na maandiko aliyoandika sio tu wapinzani wa ukristo yamewachanganya bali hadi wakristo wenyewe wakijikuta ktka makundi makundi kiasi cha mtu aliyekuwa mwanafunzi wa yesu PETRO kuwataadhalisha wasomaji wa maandiko yake kuwa kuna watu wasio na uelewa huyachanganya na kujichanyanya.

Mwisho wa paul, Baada ya kazi kubwa ya kusambaza Ukristo maeneo yote yenye ushawishi enzi hizo. Anakamatwa na kukatwa kichwa kama ng'ombe machinjioni. Tofauti na Ng'ombe,Mbuzi,Kitimoto au tunaowaona wakichinjwa na ISIS kwenye habari alionekana mtu mwenye furaha, kama vile Bwanaharusi anakwenda kumpokea bibi harusi.
Kifo kwake hakikuwa Tishio tena bali ni zawadi kwa kazi kubwa aliyoifanya mpiganaji huyu tayari kwa Kusubiri Taji na Medali siku ile ya Hukumu.

Haya ndio maneno yake ya Mwisho mwisho akimuandikia barua kijana shupavu Timotheo katika Usiku ule ambao wanahistoria wanasema asubuhi yake alipokea zawadi ya Kifo kwa kukatwa kichwa na shoka...
2timotheo 2:5-7
Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

UMAR Ibn Al-Khattab

Baada ya kifo cha Mtume Momammed SAW, Hakuna mtume mwingine aliyetakiwa kuwepo isipokuwa ukawepo mpango mkubwa wa muda mrefu wa kuwa na kingozi wa kidini atakayesimamia mambo ya imani na kuwa kiongozi wa dola la kiislam maarufu kama Islamic Calphate. Kiongozi wa Dora hii alijulikana kama Caliph. Katika historia Kumewahi kuwepo macaliph wanne tu tangu mtume kufariki na baada ya hapo imani iliendelea kuwepo bila ya umoja wa enzi hizo.

1:Abu Bakr.
2:Umar ibn al-Khattab.
3:Uthman ibn Affan.
4:Ali ibn Abi Talib.

Hapa tunamzungumzia Caliph wa pili kuwahi kuwepo duniani maarufu kwa jina la Umar. ZTV na nadhan Azam media wanavipidi wanaonyesha juu ya jemedali huyu na kiongozi shupavu ambae wanazuoni wanafananyisha kazi aliyoifanya katika uislam inaweza kufananishwa na PAULO kwa kazi aliyoifanya kwenye Ukristo miaka zaidi ta 500 kabla yake. Alipokea Uislam mwaka 616ACE kama SAUL Umar alikuwa katika harakati ya Kutafuta kumuua Mohammad kabla ya kukutana na watu wake wa karibu ambao tayari walikuwa wameshakuwa waislam. alishawishiwa na maneno ya quran na akajikuta nia yake ovu akiijutia na usilimu...

Alikuwa mtu hodari kwa kusambaza Uslam. Ukiona leo waislam wamesambaa karibu dunia nzima huwezi kuwatenga na kazi ya huyu jamaa aliyejiita commander of the faithful” (amīr al-muʾminīn). Ndiye aliyebadili taswira ya Uislam kutoka kwa waarabu tu na kusambaa dunia nzima.Leo kuna waislam wachina,wahindi,wazungu,weusi n.k
Anaheshimika duniani kote kwa kutawala kwa kufuata haki. Alianzisha mifumo thabiti ya kidini na kiutawala.
Tofauti na wengi wanavyodhani, Siku walipoiteka Jerusalem, kulikuwemo na wayahudi na wakristo. Umar aliingia jijini hapo siku kadhaa baadae kwa staili ya aina yake ya kujinyenyekeza. Yaani aliingia akiwa amembeba mfayakazi wake kwenye punda huku yeye akivuta kamba ya punda yule. Kwa kiongozi kama yule watu hawakutegemea. Alipofika alitoa fundisho ambalo kwangu ni naliona kama ni la muhimu sana. Aliwaagiza waislamu wote wasimlazimishe mtu yoyote kuwa muislamu kwa lazima. bali waishi maisha mema ya mfano ili wakristo na mayahudi wawe waislamu kwa mvuto wa maisha ya waislamu wanaozunguka. aliagiza kuwe na haki sawa kwenye ardhi kwa watu wote. Aliwatoza kodi ya chini wakazi wa Jerusalem kuliko hata wakoloni waliokuwepo hapo.
Historia zinasema ndiye aliyetoa wazo la kutenganisha kwa wanawake na wanaume katika ibada ili kusiwe na matamanio na watu wajielekeze kwenye ibada tu.
Ni Umar aliyeifuta kabisa kazi nzuri aliyoifanya Paul middle east na maeneo ya karibu kwa kusambaza uislam kote huko.
kama inavyotokea mara nyingi Mashujaa wengi hufa vifo vya kawaida. Siku moja akiwa anasoma sala ya asubuhi alivamiwa na mtumwa wa kiajemi na kumchoma visu mara sita tumboni na kumuacha damu zikibubujika ardhini na hapo ndio ukawa mwisho wa shujaa huyu
kuna mengi alifanya hapa wataalam zaidi wanaweza kuchambua.

karibuni,
mashehe,wachungaji, wananzuoni na maulamaa tujadili watu mashuhuri hawa katika imani hizi kinzani bila jazba, ugomvi,fitna na maneno ya kejeli.
naweza kuwa sijaweka mzigo wote ila yaliyobaki yanabaki kama changamoto na mianya kwa wachangiaji.

Ma shaa Allah alikuwa mtu shujaa saidna Omar nimepata bahati ya kwenda madina na kuona kaburi lake ambalo kazikwa karibu na mtume muhamad na Abubakar swidik ndani ya msiki wa nabii muhamad masjd nabawiya na hata vijiwe vyao vilikuwa karibu vyote kazikwa humo
f50051640f6584ac718e040dc5fc000d.jpg
 
Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,696
2,000
kwa upande wa paul ni kweli kabisa ilio yafanya juu ya ukristo baada ya kuongoka ni makuu sana na wala hakujiinua wala hakujifananisha na mitume wa yesu alijiona ni mdogo kwao na wala hakukaa darasani kuisoma injili lakini aliifundisha kwa ufasaha.
 
Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,696
2,000
tena alifurahisha zaidi pale alipomuonya petro juu mwenendo wake ilhali ndie aliekabidhiwa uongozi wa kanisa.

ila sasa niulize tuu mkuu MSEZA MKULU inasemekana yeye paulo ndie alieupotosha ukristo ni kwa namna gani labda?
 
BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
2,000
kwanini uislam na ukiristo tu wakati kuna dini nyingi? kwani ni umar na paul wakati kuna wapambanaji wengi tu wa dini zao? mfano Sidharta gautma ambae ndie alikekua muanzilishi wa dini yenye wumini wengi sana huko asia ya kibudha, vipi kuhusu akina krishna na akina mithra? kwanini tujifungie tu ndani ya box la uislam na ukiristo?
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
29,039
2,000
asante kwa tofauti hizo.
Ufanano wao unakuja kwenye kazi walizozifanya kueneza imani zao japo mbinu zilikuwa tofauti.
PAUL aliupa Ukristo sura ya Kimataifa kutoka kwenye sura ya Kiyahudi zaidi,
Vivyo hivyo UMAR aliutoa uislam kwenye mazingira ya kuwa dini ya waarabu tu na kuupa sura ya Kimataifa.
Labda nikuulize swali.paulo ni nani asaa katika ukristo,ni nabii au ni mwanafunzi wa yesu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom