Umalaya ni kitendo cha mtu kutoa huduma ya ngono kwa lengo la kujipatia faida

Umalaya ni kujihusisha kimapenzi na watu (wengi) tofauti tofauti. Ukahaba ni kujihusisha na ngono kwa malipo

Upo Sawa.
Ila vyote ni Visawe vinavyorejelea maana Ile Ile ya msingi.
Umalaya na ukahaba wote umelenga kujipatia faida, yaweza kuwa faida ya kiuchumi au kihisia au vyovyote vile
 
Naomba kukurekebisha. Malaya ni mtu anaefurahia kufanya ngono kama hobby na sio namna ya kujipatia kipato.

Ndio maana neno malaya hutumika kwa wanawake na wanaume pia.

Kahaba ni mtu anaetumia mwili wake kumburudisha mwingine kwa malipo au ujira. Ndio maana neno kahaba linatumika sana kwa wanawake na sio kwa wanaume....


Hivyo ni Visawe ambavyo maana zake zinarejelea Jambo moja
 
MALAYA NA UMALAYA

Na, Robert Heriel

Leo tuzungumze kidogo kuhusu Malaya na umalaya kwa ujumla wake.

Umalaya ni kitendo cha mtu kutoa huduma ya ngono kwa lengo la kujipatia faida, iwe ni faida ya kipesa, mali, kazi au hata jambo fulani. Mtu anayefanya kazi ya Umalaya huitwa MALAYA. Jina jingine la Malaya ni Kahaba, na kitendo cha kufanya umalaya pia huitwa Ukahaba.

Umalaya ni moja ya fani au taaluma kongwe hapa duniani. Asili ya umalaya ilianzia pale mwanamke alipoanza kutaka kumiliki uchumi kama mwanaume.

Biashara ya umalaya kisheria inaweza kuwa halali au haramu kulingana na nchi na nchi. Kidini Umalaya ni dhambi, pia kimaadili umalaya kwenye jamii nyingi duniani ni kosa na uvunjifu wa maadili.

Biashara ya umalaya ni kongwe kuliko biashara nyingi hapa duniani. Sio rahisi kuzuia biashara hii kutokana na nature ya biashara yenyewe ilivyo.

Aina za Umalaya
  1. Umalaya wa Kitaaluma
  2. Umalaya wa kiasili
  3. Umalaya wa kimazingira

1. UMALAYA WA KITAALUMA
Huu ni umalaya ambao unazingatia zaidi taaluma ya kufanya ngono ambapo Malaya(mtoa huduma) anakuwa na elimu, ujuzi, uzoefu wa kazi ya kufanya ngono. Aina hii ya umalaya ni aina bora kwani huichukulia kazi hii kama kazi zingine.
Malaya atajifunza umalaya kama kazi na kujua miiko yake katika kazi yake.
Malaya atajifunza lugha mbalimbali za wateja wake kulingana na wingi wa wateja wake.
Malaya atajifunza matumizi ya viungo vya wateja wake
Malaya atajifunza matumizi ya dhana za kufanyia kazi zake.
Malaya atajifunza mavazi ya kazi yake na matumizi yake
Malaya atajifunza mapozi, mitego, mikogo, katika kazi yake.
Malaya atajifunza kozi ya saikolojia ili kuwaelewa wateja wake.
Katika aina hii hakuna ubabaishaji, gharama zake zipo juu kutokana na malaya kuwa wa viwango vya kitaaluma.
Malaya wa aina hii huwa hawana familia, hawa hujiona walizaliwa kwa ajili ya kuwahudumia wanaume, kuwapa raha wanaume na kuwaburudisha.

2. UMALAYA WA KIASILI
Huu ni umalaya ambapo malaya hufanya biashara ya umalaya kwa sababu Mama yake alikuwa malaya au ukoo wake ulikuwa malaya. Aina hii, malaya hazingatii taaluma bali anachozingatia zaidi ni pesa bila kujali ni shilingi ngapi.
Malaya wa dizaini hii huweza kuwa ameolewa na anafamilia.
Wanachosukumwa zaidi ni hisia kutoka kwenye miili yao kwani ni tabia ya kurithi kutoka kwa wazazi wake. Wakati mwingine hata bila ya pesa huweza kufanya umalaya.

3. UMALAYA WA KIMAZINGIRA
Huu ni umalaya ambapo mwanamke hujiingiza kwenye umalaya kutokana na mazingira maalumu. Huenda ni shida, shinikizo fulani, matatizo n.k
Mwanamke hujikuta kwenye biashara ya umalaya baada ya kukutwa na shida fulani. Biashara hii huwa ya msimu. Mtu hufanya pale anapokabiliwa na shinikizo, au shida fulani

MAZINGIRA YA KAZI YA UMALAYA
Bar, Lodge na kwenye Mahoteli makubwa
Umalaya hufanywa zaidi maeneo hayo.
Magari Makubwa ya kusafirisha mizigo.
Hapa dereva na Kondakta baadhi yao huwabeba malaya ndani ya gari kutoka mji mmoja kwenye mji mwingine. Hufanyia ngono ndani ya gari, pia wakifika huchukua lodge na kuendelea na kazi hiyo.
Barabarani
Hapa Malaya hujipanga usiku kwenye barabara na kuanza kujiuza.
Madanguro
Hapa malaya hukodisha nyumba nzima kisha huita wateja wao na kazi hufanyika humo humo.
Majumbani
Hapa Mke/mume hugeuza nyumba au chumba chake kuwa sehemu ya kufanyia uhuni na wanawake wengine. Huvizia mume/mke akienda kazini au asipokuwepo na kumuita mteja wake.
Sehemu za Masaji
Hizi kwa sehemu kubwa zipo mijini. Baadhi ya sehemu za Masaji huwa na chumba kingine kwa ajili ya huduma za ngono
Fukwe pia ni sehemu muhimu kwa kazi hizi. Malaya huzitumia kujipatia wateja na kufanyia kazi zao.

WATEJA WA KAZI ZA UMALAYA
Wanaume kwa sehemu kubwa ndani ya nchi
Watalii wa nchi za nje
Wasagaji
Mashoga

MUDA WA KAZI YA UMALAYA
Umalaya hauna muda maalumu. Muda wowote kazi inafanyika. Inategemea Malaya anatumia aina gani ya Umalaya.
Malaya hana likizo maalumu. Ni pale afya yake inapokuwa njema

DHANA/ VIFAA VYA KUFANYIA KAZI YA UMALAYA
Nguo nzuri zenye kuvutia
Vipodozi, marashi, manukato n.k
Simu kwa ajili ya mawasiliano( japo wengi hawatoi namba zao kwa wateja wa mara moja. Wengi husema hawana simu)
Shanga, bangili, Hereni, mkufu
Kondomu na vidonge kwa kuzuia mimba
Vilainishi

WASHIRIKA WA KAZI ZA UMALAYA
Watu wa saluni. Hawa huwapamba lakini pia huwa ni sehemu za kuzugia kama nao ni wasusi lakini kumbe sio.
Mapolisi wasiowaaminifu(Hawa hutumika kama sehemu ya ulinzi na usalama wao. Endapo wakikamatwa na polisi basi huwatumia polisi kuwatoa
Ving'asti. Hawa huwa kama maboardguard wa malaya wawapo Bar au kwenye Club
Makuwadi. Hawa huwatafutia malaya wateja, iwe kwa vigogo wa serikali, watu mashuhuri kama wasanii, watalii n.k. Malaya wa kimataifa lazima awe na kuwadi yaani Agenti wa kumuunganisha na watu wenye pesa.
BodaBoda na Uba. Hawa hutumiwa kwenye ishu za usafiri

UMRI WA KUANZA KAZI YA UMALAYA
Kazi ya umalaya huanza pale mwanamke anapopevuka. Hivyo kuanzia miaka 12 mpaka 60
Pia inategemea na maumbile ya mwanamke mwenyewe.
Wenye umri mdogo soko lao lipo juu zaidi ya wale ambapo umri umeenda.

BEI ZA KAZI YA UMALAYA
Malaya malipo yake inategemea na mahali anapofanyia kazi, uzuri wake, umri wake, rangi, maumbile, elimu yake, Agenti wake, na pia kama ameajiriwa au kajiajiri mwenyewe.
Kwa Tanzania, Bei ya chini kabisa ni 2000/= na ya juu kabisa ni 1,000, 000/= kwa level za juu.

UMALAYA WA KICHAWI
Wapo watu huchukuliwa kimazingira na wachawi na kisha kuuzwa kwa ajili ya kufanya kazi za umalaya katika falme za kichawi. Hapa wataonekana wamekufa duniani lakini kumbe wapo kwenye ulimwengu mwingine

UMALAYA WA KUVUKA BODA
Huu ni ule umalaya ambao malaya hutoka nchi yake na kwenda nchi nyingine kwenda kufanya kazi ya ukahaba. Umalaya huu haukuanza leo. Ni tokea nze na enzi. Hata hapa Tanzania wapo malaya ambao wameenda nchi za mbali kwa kazi hii.
Katika Umalaya huu kuna aina mbili;
  1. Umalaya wa kukaa nchi husika
  2. Umalaya wa kuzunguka ndani ya chombo

1. UMALAYA WA KUKAA NCHI HUSIKA
Ni ule umalaya ambao malaya hukaa sehemu moja bila kuhama hama. Yaani kama Malaya katoka Tanzania kwenda Brazil au Dubai basi atakaa Dubai tuu akifanya kazi zake. Hii hufanywa na wengi.

2. UMALAYA WA KUZUNGUKA NDANI YA CHOMBO
Huu ni umalaya ambao malaya hakai sehemu mmoja. Huzunguka na chombo kama vile meli, ndege, magari. Hapa malaya huwaburudisha wasafiri waliomo ndani ya meli hiyo. Biashara hii hufanywa na malaya wachache sana, na wengi huwa majasusi na wauza madawa ya kulevya.

UMALAYA NA FAIDA ZAKE
Umalaya ni sehemu ya huduma zinazoingiza pesa kwa baadhi ya familia na chanzo cha mapato kwa baadhi ya nchi.
Malaya ni msaada kwa wanaume ambao hawajaoa hasa wanaotafuta maisha mijini kwani huwasaidia kupata huduma ya ngono.
Malaya hupunguza kesi nyingi za ubakaji
Umalaya hutumiwa kama sehemu ya nyenzo za Ujasusi
Umalaya huzi-boost baadhi ya biashara za usiku kama vile Bar, Matamasha ya muziki, madereva wa masafa marefu, Makasino miongoni mwa biashara zingine.
Umalaya ni nguzo kuu katika filamu za ngono, filamu za mapenzi
Umalaya hutumiwa kwenye biashara za wanamitindo, Ma-miss wa kitaifa na dunia kwani hutumia mavazi ya kikahaba. Biashara hizo ni sehemu ya umalaya.
Umalaya ni sehemu ya kivutio cha utalii, kwani baadhi ya watalii wengi hupenda wakifika nchi fulani waone wanawake wazuri wa nchi husika

UMALAYA NA HASARA ZAKE
Umalaya ni chanzo kikuu cha ndoa nyingi kuvunjika hasa ndoa za Kiafrika
Umalaya hasa ule usio wa kitaaluma ni chanzo kikuu cha maambukizi ya magonjwa ya ngono kama UKIMWI.
Umalaya ni hasa ule usio wa kitaaluma ni chanzo cha watoto wa mitaani wasio na Baba. Hii ni kutokana na kuwa mimba nyingi za wanawake malaya hutelekezwa. Na hapa ni nchi za Afrika na Asia.
Umalaya ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili ikiwa utachanganywa na fani nyingine kama Muziki, filamu, na fasheni ambapo vijana wengi wa kike watataka wavae na kufanya yale waliyoyaona kwenye luninga.
Umalaya hufungamana na biashara zingine haramu kama madawa ya kulevya
Umalaya huvunja kanuni ya kidini ambapo ni dhambi.
Umalaya humfanya mtu, au ukoo kuonekana unalaana na kamwe hauheshimiki.
Umalaya huongeza idadi kubwa ya wanawake wasioolewa wenye watoto

JINSI YA KUPUNGUZA UMALAYA NCHINI
1. Serikali iandae mpango wa kuwasajili Malaya wote na kuwapa leseni kisha walipe kodi. Kodi yao iwe juu ili kupunguza idadi yao.

2. Serikali kupitia wizara ya elimu iunde kozi maalumu ya kusomoea umalaya; ambapo mtu asiyesomea kozi hiyo na asiye na cheti hatapaswa kujihusisha na kazi hiyo. Kozi hiyo iwe na ada kubwa ili kupunguza idadi yao.

3. Iundwe sheria na isimamiwe vilivyo kwa watakaokiuka taratibu zilizowekwa za umalaya.

4. Elimu ya dini inayokemea umalaya itolewe ili watu wapunguze kama sio kuondoa kabisa fani hiyo.

Mwisho Nimalize kwa kusema: Biashara hii haifai katika jamii iliyostaarabika na inayoshika neno la Mungu. Watu waache kama itawezekana.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Pamoja na kujifanya unajua kila kitu, umeboronga ulipodai wateja wengi wa malaya ni wasiooa. Takwimu zinaonesha kuwa waliooa ndiyo wateja wakuu wa malaya kuliko wanaume ambao ni maseja
 
Pamoja na kujifanya unajua kila kitu, umeboronga ulipodai wateja wengi wa malaya ni wasiooa. Takwimu zinaonesha kuwa waliooa ndiyo wateja wakuu wa malaya kuliko wanaume ambao ni maseja


Naomba uninukuu kwenye hiyo Aya nilivyosema hayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom