Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Kama mtoto anayedekezwa alivyo ndivyo taasisi yoyote ile isiyokosolewa au kukubali kukosolewa ndivyo inavyoharibika. Taasisi zote duniani zinaongozwa na wanadamu na si malaika.
Kwa kipindi kirefu sana humu ndani ya JF au CHADEMA kwenyewe inaonekana kukosoa mambo mabaya yanayofanywa na chama hicho kama ni kupinga mabadiliko. Mtu akimkosoa Mbowe anaitwa kibaraka wa mafisadi.
Watu wakihoji busara ya kutajataja watu kwa kuwatuhumu (bila sababu za msingi, siyo mafisadi) anaitwa mbumbumbu au fisadi. CHADEMA lazima ikubali kwamba hata wao kama binadamu wanaoongoza taasisi kubwa na inayokubalika kwa jamii na katika kuongoza kwao wakati mwingine huwa wanakosea.
Mwalimu Nyerere wengi tunamkubali kama alikuwa ni Genius lakini hata yeye aliwahi kuandika kitabu kinaitwa "tujisahihishe" lengo likiwa ni kuwazindua viongozi kwamba hata wao wanakosea. CHADEMA ijisahihishe.