Umakini wa Rais Samia unavyoibua fursa za kiuchumi

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Mwaka huu serikali chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imewezesha utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Isaka wenye thamani ya takribani Trilioni 2. Mradi huu una manufaa mengi ikiwemo kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi jirani.

Ujenzi wa miundombinu ya kimkakati kama vile reli ya kisasa (SGR) na Maboresho ya bandari ya Dar es salaam ni ushahidi wa wazi juu ya uwajibikaji wenye tija unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi. Mwaka 2021, bidhaa za Congo DRC ziliingiza mapato Bandari ya Dsm kwa kiasi cha takribani Dola Milioni 2.3.

Biashara kati ya Tanzania na Congo DRC (Export) ilifikia kiasi cha Dollar Milioni 207.2 kwa mwaka 2021. Nchi ya DRC yenye wakazi zaidi ya Milioni 90 ni fursa kubwa kwa Tanzania na hivyo uhusiano kati ya nchi hizi mbili ni wa kimkakati na wenye tija kubwa, Rais Samia anastahiri pongezi kwa kuwa na weledi na maono yanayolenga kukuza uchumi.
 
Rais Samia Suluhu amekuja na mikakati mbalimbali ya kukuza uchumi na matunda yake tunayaona Kupitia kutekelezwa kwa miradi hii ya kimkakati watanzania tunapata fursa mbalimbali ikiwemo ajira
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom