Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Tangu kuzinduliwa kwa bunge hili la kumi wananchi wengi wamekuwa wakionyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wake. Chazo cha kutokuwa na imani na bunge hilo hasa kinatokana na hisia zilizojengeka miongoni mwa watu wengi ya kwamba spika wa sasa wa bunge hilo alipandikizwa na mafisadi na hivyo yuko pale kulinda maslahi yao na siyo ya wananchi. Wasiwasi huo wa wananchi juu ya utendaji kazi wa bunge la sasa umezidi kuongezeka kutokana na namna linavyoshughulikia huu muswada wa mabadiriko ya katiba; kwa maoni ya watu wengi kwa bunge makini huu muswada wa mabadiriko ya katiba haukustahili kupelekwa kwa wananchi kwaajili ya kupata maoni yao kwakuwa kwa vigezo vyovyote vile bado haukidhi haja. hivyo ulistahili kurejeshwa serikalini katika ngazi ya kamati ili uandikwe upya. Nasema haukidhi haja kwanza kwasababu unazungumzia suala la marekebisho ya katiba iliyopo wakati kinachodaiwa na wananchi ni katiba mpya, na vile vile maudhui ya muswada huo yanakiuka msingi wa utungaji wa katiba ambao unataka wananchi wenyewe ndio waongoze mchakato huo na wala siyo rais.