Umakini na usalama wa magari tunapoyapaki hata kama yamefungwa security system

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
4,688
3,395
Jana Jumapili nikiwa katika matembezi ya hapa na pale nikiwa na familia, nilipita katika duka/supermarket moja ili niweze kupata mahitaji ya nyumbani. Mke wangu aliingia dukani kwamanunuzi mimi nikiwa nimebaki ndani ya gari na watoto, ambapo baada ya mudaniliamua kutoka ndani ya gari pamoja na watoto ili kunyoosha miguu kidogo.

Nikiwa chini niliamua kuweka switch on ili niweze kupandisha vioo vyote kwa usalama, kwa bahati mbaya switch ikiwa bado on, nilijisahau nikafunga mlango ndipo milango yoteikaji-lock (imefungwa security system). Bahati mbaya hata funguo za chumbani zilikua ndani ya gari hiloambapo ningeweza kwenda kuchukua ignition key na remote ya akiba, kumbuka wakati huo wote switch iko on.

Nikaamua kuchukuaTaxi kwenda nyumbani nikiwa najua kwenye gari lingine lililopo nyumbani kunafunguo za chumbani, hata hivyo baada ya kufika niligundua kwamba key za garihilo nazo ziko chumba hivyo siwezi kulifungua, nikawa nimekwama pia.

Yule driver tax akaniambia mbona ni rahisi tu kulifungua gari lako (Toyota premio), akachukua kutoka kwa gariyake wheel spanner ambayo iko bevel na waya akabetua mlango kwa juu huku akiwa ameweka kitambaa ili asichubue rangi na baada ya kupata kaupenyo akaingiza ulewaya hadi pale kwenye LOCK/UNLOCK button akabonyeza, milango ikawa wazi. Nikitendo cha dakika zisizozidi tano.

Baada ya kufunguamlango wa gari nilitafuta funguo za chumbani zile nilizodhani ziko ndani yagari nazo sikuziona kumbe nazo zilikua kwenye gari ile iliyoji-lock, ndiponikaona sasa zoezi hili la waya likatumike hata kwa ile gari niliyoiacha kuledukani/supermarket. Tukarudi na yule driver, akaniambia kwa gari hii zoezi hili litakua gumu kidogo kwa namna milango ilivyokaa (Toyota Spacio).

Hata hivyo alitumia utaratibu ule ule na tukafanikiwa ingawa ilichukua muda kidogo safari hii, lakini bila madhara yoyote. Wakati zoezi hili likiendelea walikuja watejawengine waliokua wakiingia hapo dukani ambao walisema kama ikiwasumbua sana tuwapeni namba za jamaa ambao ni wataalamu wa zoezi hilo, ingawa liliwezekana kabla ya kuchukua hizo namba.

Nimependa kuchangiana mawazo haya ili watu tujue kwamba, huko kufunga magari hata kama ni kwa security system (ndio alarm zinapiga kelele baada ya kufungua), ni vema ukachukua TAHADHARI kubwa zaidi maana unaweza kuibiwa mali zako ndani ya gari kwa utaratibu kama huo.

Nawasilisha.
 
Hiyo ya kufungua lock kwa njia ya waya ipo toka kitambo kaka. Binadamu na udhaifu wetu wa usahaulifu, hakuna jinsi zaidi ya kukubali hali hii. Ni kuwa muangalifu tu unapopaki gari, labda kuwe na mtu yupo karibu ama unapaki karibu na askari kwa maagizo na ukirudi unamuona kidiogo...maisha yanaendelea.
 
Hii hata mimi ilinitokea siku nipo garage mafundi walifungia funguo na milango ikaji-lock...akaja fundi umeme wa magari akafanya kama ulivyoelezea hapo juu na nikajua labda ni kwa sababu yeye ni fundi na kwa sababu funguo ipo kwenye switch ndio maana ikawezekana...ila nilinotice kwamba ili kufanikisha zoezi hilo vioo havipaswi kuwa vimefunga hadi juu kabisa sasa sijui kama I got it wrong siku hiyo... all in all wizi wa magari nadhani ni kitu rahisi sana kwa hawa jamaa watunduwatundu
 
Hata kama funguo haziko kwenye switch, na hilo la vioo kua havijafunga kabisa kwako ilikua ni bahati tu (kama alipitishia hapo kwenye kioo), lakini wanabetua mlango hata vioo vikiwa vimefungwa.
 
Aisee ukiwaza sana unaweza libeba gari lako km pochi ila ndo hivyo teena...me namuachiaga Mungu tu
 
Hiyo ya kufungua lock kwa njia ya waya ipo toka kitambo kaka. Binadamu na udhaifu wetu wa usahaulifu, hakuna jinsi zaidi ya kukubali hali hii. Ni kuwa muangalifu tu unapopaki gari, labda kuwe na mtu yupo karibu ama unapaki karibu na askari kwa maagizo na ukirudi unamuona kidiogo...maisha yanaendelea.

Ndio mkuu, shukurani kwa mchango ni sahihi kabisa kwamba haya mambo ni ya toka kitambo, lakini tukumbuke kua vizazi vinazidi kuja vipya hivyo tuzidi kubadilishana mawazo.
 
Hata kama funguo haziko kwenye switch, na hilo la vioo kua havijafunga kabisa kwako ilikua ni bahati tu (kama alipitishia hapo kwenye kioo), lakini wanabetua mlango hata vioo vikiwa vimefungwa.
Hatari sana....
 
Back
Top Bottom