JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Matumizi ya feni nyumbani ni salama kwa mzunguko wa hewa kati ya wanafamilia wanaoishi pamoja ambao hawajaambukizwa na virusi vya Korona
Lakini, feni zinapaswa kuepukwa wakati ambapo watu ambao sio sehemu ya familia ya karibu wanapotembelea
Hii ni kwa sababu upepo unaovuma kutoka kwa mtu aliyeambukizwa kwenye sehemu zilizofungwa kama ndani unaweza kuongeza maambukizi ya virusi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
Nyumbani, ofisini au shuleni, ikiwa matumizi ya feni ni lazima ni muhimu kuongeza mzunguko wa hewa kwa kufungua madirisha na kuruhusu upepo wa njee kuingia ndani na hewa ya ndani kwenda nje badala ya kuzunguka humo ndani