Umahiri wa Rais Samia Suluhu ni kielelezo cha kuimarika kwa utawala bora nchini Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
279
500

UMAHIRI WA MHE. RAIS SAMIA SALUHU HASSAN NI KIELELEZO CHA KUIMARIKA KWA UTAWALA BORA NCHINI TANZANIA.UTAWALA BORA ni matumizi ya Mamlaka ambayo yanakuwa na Uwazi, Uwajibikaji, Ushirikishaji wa watu, Ufanisi, Tija, Uadilifu Usawa na unafuata Utawala wa sheria.

DEMOKRASIA ni dhana pana sana Kitaaluma, lakini kwa lugha nyepesi ni Utaratibu fulani wa kimaisha ambapo katika utekelezaji wake lazima pawepo na USHIRIKISHAJI WA WANANCHI katika kufikia maamuzi.

Demokrasia ni miongoni mwa misingi ya UTAWALA BORA ambayo kila Nchi hupimwa kwa vigezo ambayo ni; Uhuru wa vyombo vya habari, Uchaguzi huru na wa Haki, Uwazi na Uwajibikaji, Ushirikishaji wa Wananchi, Usawa wa Kijinsia sanjali na Ujumuishaji wa makundi yote katika nyanja za maisha N.k.

Kila tarehe 15 ya Mwezi 9 Kila mwaka Duniani ni siku maalum iliyotengwa na Umoja Wa Mataifa kuwa siku ya Demokrasia Duniani. Ni siku muhimu na adhimu sana Katika Ustawi wa Maendeleo ya Kila Nchi Duniani kwani Utawala Bora wenye Demokrasia na Maendeleo ni pande mbili za Sarafu moja.

Taifa letu Tanzania ni Miongoni mwa Nchi kihistoria inasifika kwa sio tu kuwa na Demokrasia lakini KUISHI Na Kuitekeleza KWA VITENDO.

Nchi yetu tangu nyakati za kupigania Uhuru waasisi wetu wote walisisitiza sana Ushirikishaji wa Wananchi katika kila jambo ili kila Mwananchi ajione ni Sehemu ya Maamuzi yenye tija Kwa Taifa.

Mchakato wa kuundwa Kwa TANU Na ASP na hata baadae kuunganisha na Kuwa CCM tarehe 05.02.1977 ilikuwa ni sehemu ya ushahidi kwamba Tanzania ni nchi yenye kuamini Demokrasia na kuiishi.

Mwaka 1991 Rais Mwinyi aliunda Tume ya Jaji Nyalali kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu Uanzishaji wa Mfumo wa Kidemokrasia wa vyama vingi nchini na 80% ya Watanzania Walisema tuendelee mfumo wa Chama Kimoja tu CCM, wakati 20% walisema wanataka mfumo wa Kidemokrasia wa vyama vingi. Ni Busara za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Chama Cha Mapinduzi ndio zilipelekea Nchi yetu kuingia kwenye Vyama Vingi baada ya wao kuridhia.

Hapa tunapata uthibitisho kuwa: CCM ni Baba wa Demokrasia Nchini, pia Demokrasia sio muda wote huishi katika ile Kanuni ya "Wengi wape na Wachache Wasikilizwe" Demokrasia inaweza kuwa hata Kinyume chake na hili Duniani ni Tanzania pekee ndio TUMEONESHA kwa vitendo dhana hii ya Wachache Wape. Huu ndio Upekee wa Tanzania yetu.

Mwaka huu tunaadhimisha miaka takribani 10 tangu siku hii kuidhinishwa rasmi na Umoja wa Mataifa kuwa siku ya Demokrasia Duniani na sisi kama Taifa ni Siku ya kipekee Kabisa Kwani kuna kitu Chakipekee kabisa tumeidhihirishia Dunia kwamba sisi Tanzania ni Kinara wa Demokrasia Duniani.

Demokrasia ina misingi yake na mmoja wapo ni kuachiana Madaraka kwa njia ya AMANI. Mwaka Tanzania tulimpoteza aliyekua Rais wetu Kipenzi Dr John Pombe Magufuli na katika kuidhihirishia Dunia kwamba Tanzania tunaishi na kuiheshimu Demokrasia na Utawala wa Sheria (UTAWALA BORA), Aliyekua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN aliapishwa kuwa Rais wa awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili ni jambo KUBWA la kipekee kwani Mataifa mengi Duniani linawashinda na badala yake tumekuta Jeshi likichukua Nchi na mfano mzuri Mwaka huu baada ya kifo cha aliyekua Rais wa Nchi ya Mali, Jeshi lilimtangaza Mtoto wake kuwa Rais wa Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika.

Kwakuwa Tanzania Demokrasia ni Sehemu ya Maisha yetu na kila kiongozi huiishi misingi yake, tumeshuhudia katika kipindi kifupi cha miezi 6 ya uongozi wake ameendelea kuiishi, kuiheshimu, kuisimamia na kuitekeleza Kwa Vitendo misingi ya Demokrasia.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameimarisha UTAWALA BORA hapa nchini. Tumeshuhudia kwa kauli zake mbalimbali kuchukizwa kwake kwa matumizi ya nguvu kunakofanywa na Polisi kwa wahalifu, kesi za kubambikiza na ucheleweshaji usio wa lazima wa Mashauri mbalimbali kunakotokana na kuchelewa kwa upelelezi.

Sanjali na hayo tumeshuhudia Masheikh wa Umasho wakiachiwa huru na zaidi amekuwa akisisitiza pamoja na uwepo wa Sheria lakini watekelezaji na Wasimamizi wa Sheria hizo watumie BUSARA Katika kutekeleza Sharia na hapa aliwamyooshea Kidole Watumishi wa TRA akiwaambia hataki kodi ya dhambi.

Tumeshuhudia ongezeko kubwa la fursa za Kiuongozi na Uteuzi kwa Wanawake. Katika Nchi inayoheshimu Demokrasia Duniani Wanawake wanapewa nafasi kubwa sana katika masuala ya uongozi na uwakilishi na hili tumelishuhudia kwenye Utawala huu wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ameongeza idadi ya Wanawake kwenye Serikali yake kwa kuwapa nafasi mbalimbali kubwa kuanzia kwenye Uwaziri, Wakuu wa taasisi, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi. Hata kwenye Chama anachokiongoza CCM kwa Mara ya Kwanza tangu Kuanzishwa kwake kimepata Mwenyekiti Mwanamke na Naibu Katibu Mkuu Mwanamke. Hii ni rekodi mpya Nchini na Afrika ikiwa ni Kielelezo halisi cha UTAWALA BORA hapa Tanzania.

Tumeshuhudia ongezeko kubwa la Bajeti kwenye huduma za Kijamiii, kwenye Utawala Bora lazima pawepo na huduma za Kijamii za uhakika hasa zile zinazowagusa makundi Maalum hasa Wanawake, Vijana, Wazee na watu wenye Ulemavu (Inclusiveness). Katika hili tumemuona Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akipeleka fedha nyingi kwenye Afya kwa kuwekeza vituo vya Afya 220 , kwenye Elimu, Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Hata mengine mengi ni ushahidi tosha Mhe. Rais anaishi misingi ya Demokrasia kama inavyosisitizwa na Umoja wa Mataifa.

Kuhusu Uhuru wa Maoni na vyombo vya habari. Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi kwa umma kwamba Kwanza vyombo vyote vya Habari ambavyo vilifungiwa vifunguliwe vikiwemo Online Tv's , Lakini akaweka bayana kwamba yupo tayari kukosolewa na kwamba Wananchi wawe Huru kutoa Maoni yao. Hiki ni kiwango cha juu Kabisa cha Kuiishi Demokrasia kinachooneshwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan na ni dhahiri Kuwa Mwanademokrasia Mahiri Duniani.

Kuhusu Mtazamo wa Kimataifa Kuhusu Demokrasia, Nchi yetu tumepiga hatua kubwa sana katika kuienzi, Kuiishi na kuitekeleza kwa vitendo misingi ya UTAWALA BORA.

Kwayo; itoshe kusema kwamba, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kielelezo sahihi kwa maneno na vitendo vyake kama Mkuu wa Nchi ambayo inaenenda MISINGI YA UTAWALA BORA.

Kazi Iendeleee🇹🇿

IMG-20210914-WA0006.jpg

IMG-20210914-WA0001.jpg

IMG-20210914-WA0004.jpg
 

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,106
2,000
Ubambikizaji kesi
Kishamiri kwa matukio ya kigaidi (Mbowe na Hamza Kama mfano)
Ongezeko la Kodi mfano Tozo
Kukosekana kwa soko la nafaka
Kudorora kwa utalii
Kususiwa kwa Covid19 vaccine

Hayo yote bado Hangaya ni Bora?
Mimi nishaamua Hangaya nae ni garasa Kama watangulizi wake tuu
 

kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,285
2,000
Hahaaaaaa....tutasifia kila mtawala anayeingia Magogoni, siku zinakwenda...miaka ianakwenda tutabaki hivi hivi kushabikia mambo ambayo hayaweki msingi wa kuinua uchumi kuanzia level ya chini kabisa kwenda juu.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,027
2,000
Hivi mtu anawezaje kuandika makala ya uongo ndefu kama alivyofanya mtoa mada?!

Malipo ni kiasi gani? lengo ni nini? walengwa ni kina nani? je, ni sahihi kuwalenga wasomaji wa JF?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom