Umahiri wa kutoa matamko yenye dhana mfu humaliza thamani ya utu wa mtu

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kuna misemo mingi ya kiswahili ambayo tumekuwa tukiitumia katika kufikisha ujumbe katika jamii ambayo iliasisiwa na wazee wetu tangu enzi hizo,lakini misemo hiyo na nahau zake ililenga kutoa fundisho katika jamii husika na hata wakati mwingine iliweza kujenga jamii kusudiwa.

Ningependa nami leo hii nianze na msemo husemao kitokacho mtu chake akimtapishi japokuwa huenda kikamshushia heshima yake ndani ya jamii na wanajamii wanao mzunguka.Nimechelea kusema hivi kutokana na mambo ambayo yamekuwa hayana mashiko katika jamii yetu kupewa kipau mbele kuliko hata matatizo ambayo yanatukabili.

Marehemu manju wa nyimbo za Kinyamwezi mzee Mwanamila aliwali kusema kwenye moja ya nyimbo zake kuwa mzushi na muongo bora muongo.Alijua fika kuwa mzushi akiamua kuzusha jambo lake linaweza hata kuchafua hali ya hewa kwa amani kuvunjika,lakini cha kushangaza leo viongozi wetu wamegeuka kuwa wazushi bila hata kufanyia uchunguzi mambo wanayoyazusha.Ndiyo maana hata leo utasikia misemo kamavile waja wakikuchukia mengi watakuzushia.

Lengo hasa la uzi ni kuwaonya viongozi wetu ambao tumewapa dhamana ya kutungoza na kuacha kazi zao za kuleta maendeleo kwa ustawi wa taifa na watu wake na kugeuza ofisi zetu za umma kama sehemu ya kuzusha mambo yasiyo na tija katika nchi yetu.

Tunapoamua kufanya propagandabasi propaganda hizo zisiwe za wakufitinisha watu katika jamii ili hali hakuna ukweli wowote uliogusiwa.Nimekuwa wakati mwingine nikiwalaumu hata viongozi wetu kwa kushindwa kutetea kile walichoamini na kujua nini uhalisia wake kutokana na ujuzi wa elimu waliyokwisha kuipata lakini wakakaa kimya kunyamazia na kuyaacha yachukue nafasi katika jamii husika ilihali ukweli unajulikana.

Tukikubali kila jambo linalo zushwa bila kufanyika uchunguzi wa kina basi nasi tutakuwa na vichwa vya samaki.Maana akili ya samaki ni nyepesi kusahau na ni ngumu kuelewa.

Napenda kusema hivi kutokana na viongozi wetu kushindwa kusoma alama za nyakati na kukosa mbinu mbadala za kuweza kutatua matatizo ya wananchi na kuamua kuzusha mambo yasiyo na msingi katika nchi yetu.Sina lengo la kutaka kumtetea mtu lakini Watanzania tumekuwa wathiri wakubwa wao ombwe la uongozi ndani yanchi yetu kutokana na ufinyu wa fikra uliowagubika viongozi wetu.

Taifa limekosa fikra pevu ndani ya serikali yetu za kuweza kutafuta tiba mujarabu wa matatizo yetu na kuzifanyia utatuzi changamoto zinazotukabili kwa viognozi wetu kuamua kufanya siasa hata kwenye mambo ya msingi yanayogusa maisha ya Mtanzania moja kwa moja.Kwanini kama umepewa dhamana ya kuongoza usichuje mambo unayotakiwa kuyasema hasa ukizingatia kuna mambo ya mazito unayo jaribu kuya kwepa kuyasemea kwa kuwa tu ni mmojawapo wawaliochangia masuala hayo kukosa ufanisi.

Mi nilidhani ingekuwa busara kama kiongozi anapo shindwa kuyatekeleza majukumu yake kwa ufasaha angeweka hadharani na kusema jamani ee mzigo huu mlionipa mzito nahitaji mtu wa kunitua kuliko kutumia mbinu finyu ya kukwepa majukumu kwa kuzusha mambo yatakayo potesha ukweli na uzushi huo usilete tija katika jamii.

Njia ya kuzusha mambo ili uweze kuficha uliyoyaboronga imekuwa ikitumiwa sana na viongozi wetu bila kuiona huruma kwa wanyonge ambao ndiyo waathirka wakuu.Mathalani,unaposimama na kumzungumzia mtu fulani ambaye hayupo ndani ya system ya utendaji wa kila siku wa kazi za serikali inatatua vipi matatizo ambayo wewe kama kiongzozi na chama chako ndicho kimeshikila dola kuna saidia nini kama si ufinyu wa kifikra.

Wafalisayo walikuwa wana uwezo mkubwa wa kuongza na kutawala,lakini walikuwa hawapendi kabisa kadhia hiyo kwa kuwa walijua uongzi ni dhima.Kama kiongozi unawezaje kupata usingizi ikiwa wananchi wako wanalala na njaa.Yanayoropokwa leo hii na tuliowapa dhamana ya maisha yetu ni sawa kabisa na alivyoropoka mke wa mfalme wa Ufaransa pale wananchi wake wake walipoandamana na kudai bei ya mkate imeongezeka na kuwataka kama mkate umeongezeka kwanini wasile keki.Leo kuzungumzia kadi ya Dr. Slaa wakati wananchi hawajui siku yao ya leo itaisha vipi ina tofauti gani na kejeli aliyotoa mke wa mfalme?

Kauli zenu mlioshiba zinatakiwa zitoe dira na mwelekeo wa maisha yetu,maana kama ni kodi mnatuminya sana lakini hatuoni matunda ya kodi zetu kutokana na kushindwa kutatua lindi la umasikini uliotugubika.Kadi ya Dr. Slaa sipendi kuamini kama ndiyo ilikuwa agenda kuu ya mkutano mkuu wa CCM huko Dodoma.

Tungependa Dr. Slaa ahukumiwe kwa utendaji wake na si kadi kama ambavyo mh.Nape alitaka kutuaminisha.Si kadi tu hata suala la mheshimiwa si hoja katika kipindi hiki nchi inataka mapinduzi ya kweli ya kijani.Kauli kama hizi ni njia mojawapo ya kushusha heshima na kuwadharau Watanzania wenzenu wasio na uhakika na mlo mmoja wa siku ilihali ninyi mnakula na kusaza.Tafakarini kabla ya kuropoka,nchi hii kila jambo litakalo tamko litapimwa kwa vigezo nwakati uliopo.
 
Back
Top Bottom