Umafia katika Usajili: Simba SC yamsainisha Niyonzima kwa Mil.100 huku Yanga FC ikipigwa butwaa

Umafia tu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya shilingi milioni 100.

Habari zilizopatikana jana jioni zinasema Niyonzima amekubali kujiunga na Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kumpa fedha hizo za usajili.

Kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, Niyonzima ambaye amebakisha mwezi mmoja kwenye mkataba wake na Yanga, alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Simba SC.


Taarifa zinadai kuwa Simba waliongea na Niyonzima kabla hajaenda Rwanda kujiunga na timu yake ya Taifa, lakini akataka viongozi hao kuwasiliana na wakala wake ambapo Simba walifanya hivyo na kupewa dau walilokuwa wakilitaka.

Aidha, Yanga iliwasiliana na Niyonzima akiwa Rwanda baada ya kusikia Simba wamewasiliana naye na hivyo wakamuahidi ofa nono ili asisajiliwe na Simba.

Baada ya kusikia Yanga wamewasiliana na Niyonzima, Simba walimtuma mtu kwenda Rwanda kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini wakala wake aliwataka wamsubiri Niyonzima Dar es salaam kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Niyonzima alipowasili nchini juzi usiku alipokelewa na kigogo mmoja wa Simba huku Yanga wakiwa hawafahamu kama nyota huyo ametua nchini.

Imeelezwa Yanga walimuandalia nyota huyo dau la milioni 60 ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini tajiri mmoja wa Simba alimuhakikishia kumpa dau la shilingi milioni 100.

Kabla ya kupewa dau hilo, Yanga waliongezea dau lao na kufikia shilingi milioni 80 ambazo hata hivyo, hazikumshawishi Nahodha huyo wa Rwanda kusaini nao mkataba mpya.

Chanzo: Nipashe
Saaaafi Simba.Hapo in maandalizi ya kupanda ndege, lazima tuwanyang'anye wachezaji wazoefu wa kupeperuka angani. Mlitaka tukasajili toka Majimaji??? Au Kurugenzi ya Njombe?
 
Bahati mbaya sana mnakuwa hamna mchezaji bora Yanga ila lazima watoke Simba.. Sasa wasajili nini?
Katika miaka 5 iliyopita hamjachukua ubingwa while Yanga amechukua mara 4 sasa hao wachezaji bora mlio nao wanafanya kazi gani ?
 
Niyonzima yupi aliesaini simba.....huyu huyu wa rwanda au siku hizi tandale nako kuna niyonzima???????.....nyie mashabiki wa mezani fc mkae mkijua niyonzima ni mchezaji wa yanga na tayari ameshaongeza mkataba wa miaka miwili
 
Mi huwaga sielewi ama!!? Mbona ulaya dau wanapewa timu inayo mmliki mchezaji wakati huku dau anapewa mchezaji??
Huku bongo timu huwa zinangoja mchezaji amalize mkataba wake ndio zinamchukua wakati ulaya watu wanavunja mkataba ndio maana wanalipa kwa klabu
 
Mi huwaga sielewi ama!!? Mbona ulaya dau wanapewa timu inayo mmliki mchezaji wakati huku dau anapewa mchezaji??
Nafikiri TFF wana taratibu zao ambazo ziko tofauti na kwingineko? Au Niyonzima alikuwa ni free agent kwa maana kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa umeshamalizika? Kama mkataba ulikuwa umeshamalizika na hajakubali kuongeza mwingine basi Yanga inakuwa haina haki ya kupata malipo yoyote. Ila kama mkataba uikuwa umebakiza hata masaa machache, anakuwa bado amefungwa na hawezi kusaini mkataba mwingine. Sasa hapo inategemea ukweli ni upi.
 
Katika miaka 5 iliyopita hamjachukua ubingwa while Yanga amechukua mara 4 sasa hao wachezaji bora mlio nao wanafanya kazi gani ?
Ubingwa wa hujuma kwa timu nyingine nao ni ubingwa? Kama si saidia baba TFF..!

Mara nyingi Simba imenyang'anywa point na Chama chenu.
 
Hivi yule mwanafunzi wa Yesu ambae Yesu alipowatokea wanafunzi wake akawa haamini kama ni Yesu wa kweli alikua anaitwa nani
Aliitwaga Tomaso.

Na wewe ni Tomaso?

Let's join Team Doubting Thomases!
 
Back
Top Bottom