Umafia katika Usajili: Simba SC yamsainisha Niyonzima kwa Mil.100 huku Yanga FC ikipigwa butwaa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,410
2,000
Umafia tu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kudaiwa kujiunga na Klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kupewa ofa ya shilingi milioni 100.

Habari zilizopatikana jana jioni zinasema Niyonzima amekubali kujiunga na Simba baada ya viongozi wa klabu hiyo kumpa fedha hizo za usajili.

Kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara, Niyonzima ambaye amebakisha mwezi mmoja kwenye mkataba wake na Yanga, alikuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Simba SC.


Taarifa zinadai kuwa Simba waliongea na Niyonzima kabla hajaenda Rwanda kujiunga na timu yake ya Taifa, lakini akataka viongozi hao kuwasiliana na wakala wake ambapo Simba walifanya hivyo na kupewa dau walilokuwa wakilitaka.

Aidha, Yanga iliwasiliana na Niyonzima akiwa Rwanda baada ya kusikia Simba wamewasiliana naye na hivyo wakamuahidi ofa nono ili asisajiliwe na Simba.

Baada ya kusikia Yanga wamewasiliana na Niyonzima, Simba walimtuma mtu kwenda Rwanda kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini wakala wake aliwataka wamsubiri Niyonzima Dar es salaam kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Niyonzima alipowasili nchini juzi usiku alipokelewa na kigogo mmoja wa Simba huku Yanga wakiwa hawafahamu kama nyota huyo ametua nchini.

Imeelezwa Yanga walimuandalia nyota huyo dau la milioni 60 ili asaini mkataba wa miaka miwili, lakini tajiri mmoja wa Simba alimuhakikishia kumpa dau la shilingi milioni 100.

Kabla ya kupewa dau hilo, Yanga waliongezea dau lao na kufikia shilingi milioni 80 ambazo hata hivyo, hazikumshawishi Nahodha huyo wa Rwanda kusaini nao mkataba mpya.

Chanzo: Nipashe
 

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,529
2,000
Lazima washangilie,mara ya mwisho Simba kusajili mchezaji toka Yanga sijui ilikuwa lini.Lakini Yanga kila wakimtaka mchezaji wa Simba wanamsajili
 

jac salum

Senior Member
Mar 23, 2017
179
250
Mi huwaga sielewi ama!!? Mbona ulaya dau wanapewa timu inayo mmliki mchezaji wakati huku dau anapewa mchezaji??
Usajili wa kuvizia , yaani wanategea mchezaji kumaliza mkataba na timu ndipo wamsajili. Sijaona timu kati ya Simba na Yanga zikichukuliana wachezaji kwa kuvunja mikataba yao. Huwa wanasubiria wanapomaliza mkataba tu wanafanya mishe za usajili
 

Jaslaws

JF-Expert Member
May 31, 2011
6,038
2,000
Hahaaaaah.. Simba bhana, wanahangaika na kikosi cha Yanga, wanaamini nini ndani ya kikosi hiki....
Simba wamemsaini nani kutoka yanga!?huyo niyonzima Mwenyewe Ni tetesi tu,yanga ndo huwa mnatabia zakukomoana kwenye mpira,Leo simba wamewafanya mlichokuwa mkifanya mnabaki kulialia tu..!!ajib si mkichukua!?tulieni basi.
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,055
2,000
Mi huwaga sielewi ama!!? Mbona ulaya dau wanapewa timu inayo mmliki mchezaji wakati huku dau anapewa mchezaji??
Huku kwetu wachezaji wengi wanahama tumu baada ya mikataba kwisha. Ingekuwa bado anamkataba wa muda mrefu ingelipwa club. Hata ulaya ivoivo
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,410
2,000
Lazima washangilie,mara ya mwisho Simba kusajili mchezaji toka Yanga sijui ilikuwa lini.Lakini Yanga kila wakimtaka mchezaji wa Simba wanamsajili
Bahati mbaya sana mnakuwa hamna mchezaji bora Yanga ila lazima watoke Simba.. Sasa wasajili nini?
 

sonjames

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
292
500
Lazima washangilie,mara ya mwisho Simba kusajili mchezaji toka Yanga sijui ilikuwa lini.Lakini Yanga kila wakimtaka mchezaji wa Simba wanamsajili
Sio kwa kipindi hiki ambacho yanga ina hali mbaya kiuchumi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom