Umachinga ni 'social behavior', siyo rahisi kuibadili kwa Sheria au kwa Matamko

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-alaekoum Wana-JF

Nianze kwa kurudia 'mantra' yangu kuhusu maamuzi ya wanasiasa na watawala wetu katika MFUMO tulionao:

THE HALLMARKS OF BAD GOVERNANCE:

1. Ambiguity
2. Arbitrariness
3. Capriciousness

Maana ya mantra hii ni kwamba huwezi kuwa na Utawala Bora kwa maamuzi:

1. YA KUKINZANA, [Ambiguity]
2. YA KIHOLELA, [Arbitrariness]
2. YA HILA. (mizengwe) [Caprice]

Lengo la andiko hili ni kujadili sera na maamuzi ya wanasiasa na watawala wetu katika masuala ya maendeleo na ustawi wa jamii hasahasa katika masuala ya siasa na sera za CCM za social engineering na mipangomiji, pamoja na usafi wa mazingira na ujasiriamali kwa ujumla wake katika muktadha wa (in the context of) mantra yangu hapa juu kuhusu haki za binadamu na UTAWALA BORA.

Tamko la UN kuhusu ajira ni kwamba ajira ni haki ya kila mtu. Kama ilivyo haki ya kuishi. Na kwenye Tamko hilo hakuna ambiguity kuhusu tafsiri ya neno AJIRA.

Sera ya CCM ni kwamba ajira ni "kujiajiri mwenyewe" au "ujasiriamali". Kujikanganya kwa sera kunaanzia hapo. Kwasababu kauli hii ni ya kisiasa tu na haiendani na tamko la UN kuhusu ajira. Kwasababu jukumu la serikali ni kuzalisha nafasi za ajira. Hii maana yake siyo kwamba serikali iajiri raia, hapana. Bali ni jukumu la serikali Kubuni sera zitakazozaa VYANZO VYA AJIRA. Serikali yetu badala ya kubuni vyanzo vya ajira kila siku inabuni vyanzo vya kodi!

Sera hii ndiyo iliyotufikisha katika kero au tatizo la machinga nchi nzima, pamoja na bodaboda, mamantilie, daladala, bajaji nk. Haya ni makundi ya vijana, wanawake, wazee nk wanaotumiwa na CCM kwenye kura wakati wa kampeni za uchaguzi na upigaji kura.

Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 Hayati JPM alianzisha vitambulisho rasmi vya ujasiriamali. Nimeshasema mahali pengine humu kwamba CCM walilifungua chupa la jini. Lakini JPM akaenda mbali zaidi kwa kulitoa ndani ya chupa na kuliweka 'SEBULENI' kwao.

Ulikuwa uamuzi holela, usiozingatia kanuni za mipangomiji usafi wa mazingira na njia za kiuchumi au kisayansi (social economic policies) za ubunifu wa AJIRA katika misingi ya tamko la UN kuhusu haki ya ajira.

Ulikuwa uamuzi wa hila pia (wa mizengwe) kwa madhumuni ya kuwatumia wahusika kisiasa dhidi ya upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Machinga ni kaa la moto hawagusiki. Bodaboda nao kupitia siasa za CCM wamepewa kiburi cha kukiuka sheria za usalama barabarani!
Hulka au tabia asili ya makundi haya (croud behavior) ni kutumia status kama makundi ya wapigakura wa CHAMA TAWALA na wingi wao kulinda maslahi yao. Wingi wao unaotumiwa kisiasa umewapa nguvu ya ajabu mbele ya local government na traffic policing.

Halafu kuna phenomenon katika town planning inaitwa "attractive nuisance" (kero mtego) ukiitengeneza au kuiruhusu iwepo, ni ngumu sana kuiondoa.

Jalala au dampo ni kero mtego wenye chambo (an attractive nuisance) unaovutia uzembe.

Kwamfano ukirihusu watu watupe takataka eneo fulani kwa muda fulani, utakuwa umeanzisha jalala au dampo, an attractive nuisance. Kila mwenye taka zake ataziweka hapo. Na wengine watakuja kushinda hapo wakisakula.

Si rahisi baada ya muda fulani kuzuia watu wasitupe taka hapo au kuwaondoa wasakulaji. Utakuwa umebadili social behavior ya jamii husika ambayo ni ngumu kuibadili. Binadamu wanakuwa kama nzi wanaovutiwa na uchafu!

Kwa mantiki hiyo umachinga ni social behavior. Ni hulka ya jamii au kundi la jamii. Hata bodaboda ni kundi la watu waliozoezwa kuvunja sheria za usalama barabarani na usafi wa mazingira. Huwezi kuwabadili tabia yao kirahisi, haswa unapowatumia kisiasa. Unawapa nguvu dhidi ya mamlaka zinazosimamia mipangomiji na mazingira nk.

Kitu cha tatu katika mantra yangu ni AMBIGUITY.

Huwezi kuwa na Utawala Bora hata kama lengo ni kubuni vyanzo vya ajira, kwa maamuzi yanayokinzana.

Unaajiri wataalamu wa mipangomiji, wa afya ya jamii, wataalamu wa mazingira nk.; Halafu unawapa wajasiriamali vitambulisho rasmi vya kufanya biashara POPOTE'!

Ukweli hapa bni kwamba hujabuni ajira wala VYANZO VYA AJIRA endelevu kwa misingi ya tamko la UN kuhusu ajira.

Rais SSH alipokiwa Mwanza alisema anajua kwamba baadhi ya machinga huwauzia wafanyabiashara wakubwa mbele ya maduka yao, akawaonya kwamba wanaziba njia za waenda kwa miguu na kuleta msongamano barabarani!

Zoezi hili linaonyesha kwamba siri ya wajasiriamali hawa ni wafanyabiashara wenye MITAJI MIKUBWA wanaowapa "AJIRA" baadhi ya wamachinga (kwa mlago wa nyuma) na kufanya watawala kudai kwamba wamezalisha ajira!

Kwa fikra za kawaida serikali ingeboresha mazingira ya wafanyabiashara wenye MITAJI MIKUBWA ili wawape ajira hao wanaopanga bidhaa barabarani nayo serikali ipate kodi zaidi. Badala yake sera za CCM zinawaumiza wafanyabiashara wakubwa wanaolipakodi kwa EFD kwasababu hawaupendi mfumo wenyewe, na wengine humfanya mbinu za kuuhujumu. Halafu pia serikali haipati kodi inayostahili toka kwa machinga hata kama baadhi yao wana mitaji mikubwa. Ilimradi wamepata vitambulisho rasmi na kuvivaa shingoni. Hawagusiki!

Huko Morogoro DC na Mkurugenzi wa Jiji wamefutwa kazi kwa suala la machinga; tena kupitia tamko la hadharani kule Mwanza! Mimi bado sijaelewa kama Rais SSH alishauriwa na waziri yupi katika serikali yake?

Kwasababu suala la kubuni au kuhamisha maeneo ya biashara za machinga ni la mamlaka za miji na wizara mtambuka. Lakini uamuzi wake ulifanywa papo kwa papo siku chache tu baada ya vurugu kati ya Mgambo na machinga huko Morogoro! Ni mfano nzuri wa 'arbitrary decision' uamuzi wa holela.

Tumefika mahali hata bungeni Mbunge wa CCM anasema kwamfano kwamba: Mtukufu Rais ameamua katika bajeti ya mwaka huu "kuongeza kodi ya vifurushi vya simu" au"kuwapandisha vyeo na mishahara walimu". Yaani mbunge anasahau kwamba yuko bungeni kusemea wananchi na kuiwahibisha serikali katika kutumikia wananchi wote kwa usawa. Na kwamba mapato na matumizi ya Serikali (budget) yanaidhinishwa na bunge.

Nimalizie kwa kusema kwamba sera ya CCM ya ELIMU ni kuwezesha kijana kujiajiri, si kuajiriwa. Hapo hapo sera ya CCM ya UCHUMI ni kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda.

Swali gumu ni kwamba ni nani watakaoajiriwa kwenye viwanda hivyo? Ajira katika dunia ya sasa na baadae inahitaji elimu ya kimataifa pamoja na lugha, katika nyanja mbalimbali za uchumi. Hii sera ya elimu ya kujiajiri ni potofu, inakinzana na lengo la kupeleka nchi kwenye UCHUMI WA JUU.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Umachinga ni staili ya maisha, jamani msitusumbue mlituuzia kitambulisho cha machinga wenyewe
 
Shida kubwa ya hii 'inji' ni kuchanganya professional issues (mambo ya kitaalamu) na political issues (mambo ya kisiasa).

Kibaya zaidi, politicians ndo wenye nguvu ya kimaamuzi kuliko professionals. Yaani bado tunaenda kwa 'one man show' na wote inabidi tucheze mziki kulingana na biti kutoka kwa 'one man show'
 
Umeandika vizuri Sana lakini sijaona popote ulipo define AJIRA kwa mujibu wa UN Kama ulipogusia.

Uhalisia wa maisha ya afrika hasa Tanzania, huwezi kutumia sera iliyoko Marekani ikafanikiwa Tanzania.

Machinga, bodaboda ni Kama kundi la watu wenye kero hivi iwapo tu tungekuwa na nguvu kiuchumi na ajira nyingi.

Serikali inakosa ujasiri wa kuwawajibisha hawa watu kwa kuwa inajijuwa yenyewe haijawapa mazingira wezeshi hawa watu.

Sijajua Kama kweli taifa letu linatambua na Lina sera madhubuti kuhusu hizi ajira za;
(i) bodaboda
(ii) mama ntilie.
(iii) wapiga debe

Serikali imejikuta ikijichanganya yenyewe iwapo hawa watu wafanye kazi zao kiholela ( popote ) ndani ya miji au watengewe maeneo maalumu ( mara nyingi hawataki kutengewa maeneo)

All in all nakushukuru mleta mada, ni mada fikirishi Sana ambayo inagusa sera za umoja wa mataifa kuhusu ajira na utunzaji mazingira. Pia inagusa sera za mipango miji chini ya serikali za mitaa.
 
Asante Mkuu!

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante kwa andiko bora la siku.
Hawa jamaa hawagusiki! Wamedumazwa na mamlaka kwa maslahi ya wanasiasa.
Wamekuwa kama 'chokoraa'.
Ramani za mipango miji zinaonyesha maeneo ya huduma za jamii, kama masoko n.k,.
Kwa sasa vijana hawataki sekta nyingine kama kilimo n.k.
Kuna haja ya kuanza upya!
 
Umeongea vizuri sana na umeonyesha mapungufu ya serikali ya ccm .

Maswali matatu kwako !

1: Kwa nini hujaorodhesha hayo mazingira mazuri ya kufanya biashara yaweje! kwa hao matajiri wakubwa ukiachana na hilo la kulalamika kodi ? Hii ina maana hata wewe ukipewa nafasi utaanza kutuuliza na sisi mazingira bora ni yapi kama bado hujayatambua.

Kuna msemo unasema ndege wafananao huruka pamoja. Tueleze hayo mazingira.

2 : Hujatuambia mifano ya kujiajiri ( hembu toa mifano serikali ilitakiwa ibuni nini na nini watu wajiajiri ) useme gap hapo ilitakiwa ianzishe nini ?

Kwa mfano badala ya veta kwa ajili kuwatngeza mafundi umeme, fundi rangi, mafundi wa magali na kuchomelea iwe hivi ? Ili watu wajiajiri.

3: Halafu umesema social nature ndio inasukuma mambo kua hivyo yalivyo juu ya machinga na kibaya zaidi serikali haifati mipango mji ! Je unapendekeza machinga wakae wapi ? na kivipi bila kuharibu fursa zao au wateja wao ?

Vilevile bila kuwanyima fursa wateja ambao hupatiwa huduma zao kwa mfano vibanda vya M-pesa vimelahisisha huduma ya fedha na ndio wako njiani na wengineo .

Kikubwa nimeona umeweka malalamiko peke yake ila umeacha kusema mapendekezo kwa kuyasema kwa mifano badala ya kuyaongelea kwa ujumla.

Mwisho : Navyofahamu biashara huwa inafanyika sehemu yenye population( watu wengi) , njiani mtu akiwa anatoka kazini au kurudi kazini, na maeneo husika ukiachana na magulio.

Hapa niseme kuna maeneo watu wanalzimisha mschinga wawepo na kuna maeneo sio lazima.

Nielewavyo mimi huwezi kuweka kibanda kama hio sehemu haina uhitaji wa watu ! Kwa maana hio ukimzuia machinga umemzuia mnunuaji ambae hataki kwenda mbali.

Hii inaitwa growthy pole kutokana na uvumbuzi pamoja na teknoljia ya sehemu inasogeza huduma na kukuza huduma za mji kutokana na asili ya eneo. Sasa kama asili yetu iko hivyo na fursa kwa machinga iko katikati ya mji ? Kwa nini tuone hawafai ? Wakati tunaweza kuwaacha walipo na kuhitaji waweke mazingira safi na vibanda viboreshwe ?

Mkiwatoa hizo sehemu kwa maana watu wanao pita na kununua wabadili root zao mnaharibu mfumo wa pesa na maisha ya mtoa huduma na mpokea huduma

"pili machinga waende sehemu isiyo na asili au msisimko wa biashara ili kupisha mazingira je ikitokea wakafatwa na watu mji ukakua mtawatoa tena huko " kwa sababu wanechafua mazingira.

NAHITIMISHA HIVI, sisi waafrika hatujui asili yetu, elimu tuliyo nayo ni ilifaa kuiendeleza europe ndio maana tunaharibu kila kitu tunashindwa kujijua asili yetu ila tunalazimisha iwe kama tulivyosoma YAANI HATUBORESHI AU KUREKEBISHA ILI KIWE BORA TUNAONA KILA KITU NI TATIZO HIVYO LITOLEWE.
 
Agreed!

Umachinga ni 'behaviour' ambayo imezaa 'habit' ambayo imechangiwa na 'Free riding'

Ni ngumu sana kumaliza umachinga wa kutembeza vitu mtaani na kujenga mabanda pembezoni mwa barabara.
 
Asalam-alaekoum Wana-JF

Nianze kwa kurudia 'mantra' yangu kuhusu maamuzi ya wanasiasa na watawala wetu katika MFUMO tulionao:

THE HALLMARKS OF BAD GOVERNANCE:

1. Ambiguity
2. Arbitrariness
3. Capriciousness

Maana ya mantra hii ni kwamba huwezi kuwa na Utawala Bora kwa maamuzi:

1. YA KUKINZANA, [Ambiguity]
2. YA KIHOLELA, [Arbitrariness]
2. YA HILA. (mizengwe) [Caprice]

Lengo la andiko hili ni kujadili sera na maamuzi ya wanasiasa na watawala wetu katika masuala ya maendeleo na ustawi wa jamii hasahasa katika masuala ya siasa na sera za CCM za social engineering na mipangomiji, pamoja na usafi wa mazingira na ujasiriamali kwa ujumla wake katika muktadha wa (in the context of) mantra yangu hapa juu kuhusu haki za binadamu na UTAWALA BORA.

Tamko la UN kuhusu ajira ni kwamba ajira ni haki ya kila mtu. Kama ilivyo haki ya kuishi. Na kwenye Tamko hilo hakuna ambiguity kuhusu tafsiri ya neno AJIRA.

Sera ya CCM ni kwamba ajira ni "kujiajiri mwenyewe" au "ujasiriamali". Kujikanganya kwa sera kunaanzia hapo. Kwasababu kauli hii ni ya kisiasa tu na haiendani na tamko la UN kuhusu ajira. Kwasababu jukumu la serikali ni kuzalisha nafasi za ajira. Hii maana yake siyo kwamba serikali iajiri raia, hapana. Bali ni jukumu la serikali Kubuni sera zitakazozaa VYANZO VYA AJIRA. Serikali yetu badala ya kubuni vyanzo vya ajira kila siku inabuni vyanzo vya kodi!

Sera hii ndiyo iliyotufikisha katika kero au tatizo la machinga nchi nzima, pamoja na bodaboda, mamantilie, daladala, bajaji nk. Haya ni makundi ya vijana, wanawake, wazee nk wanaotumiwa na CCM kwenye kura wakati wa kampeni za uchaguzi na upigaji kura.

Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 Hayati JPM alianzisha vitambulisho rasmi vya ujasiriamali. Nimeshasema mahali pengine humu kwamba CCM walilifungua chupa la jini. Lakini JPM akaenda mbali zaidi kwa kulitoa ndani ya chupa na kuliweka 'SEBULENI' kwao.

Ulikuwa uamuzi holela, usiozingatia kanuni za mipangomiji usafi wa mazingira na njia za kiuchumi au kisayansi (social economic policies) za ubunifu wa AJIRA katika misingi ya tamko la UN kuhusu haki ya ajira.

Ulikuwa uamuzi wa hila pia (wa mizengwe) kwa madhumuni ya kuwatumia wahusika kisiasa dhidi ya upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Machinga ni kaa la moto hawagusiki. Bodaboda nao kupitia siasa za CCM wamepewa kiburi cha kukiuka sheria za usalama barabarani!
Hulka au tabia asili ya makundi haya (croud behavior) ni kutumia status kama makundi ya wapigakura wa CHAMA TAWALA na wingi wao kulinda maslahi yao. Wingi wao unaotumiwa kisiasa umewapa nguvu ya ajabu mbele ya local government na traffic policing.

Halafu kuna phenomenon katika town planning inaitwa "attractive nuisance" (kero mtego) ukiitengeneza au kuiruhusu iwepo, ni ngumu sana kuiondoa.

Jalala au dampo ni kero mtego wenye chambo (an attractive nuisance) unaovutia uzembe.

Kwamfano ukirihusu watu watupe takataka eneo fulani kwa muda fulani, utakuwa umeanzisha jalala au dampo, an attractive nuisance. Kila mwenye taka zake ataziweka hapo. Na wengine watakuja kushinda hapo wakisakula.

Si rahisi baada ya muda fulani kuzuia watu wasitupe taka hapo au kuwaondoa wasakulaji. Utakuwa umebadili social behavior ya jamii husika ambayo ni ngumu kuibadili. Binadamu wanakuwa kama nzi wanaovutiwa na uchafu!

Kwa mantiki hiyo umachinga ni social behavior. Ni hulka ya jamii au kundi la jamii. Hata bodaboda ni kundi la watu waliozoezwa kuvunja sheria za usalama barabarani na usafi wa mazingira. Huwezi kuwabadili tabia yao kirahisi, haswa unapowatumia kisiasa. Unawapa nguvu dhidi ya mamlaka zinazosimamia mipangomiji na mazingira nk.

Kitu cha tatu katika mantra yangu ni AMBIGUITY.

Huwezi kuwa na Utawala Bora hata kama lengo ni kubuni vyanzo vya ajira, kwa maamuzi yanayokinzana.

Unaajiri wataalamu wa mipangomiji, wa afya ya jamii, wataalamu wa mazingira nk.; Halafu unawapa wajasiriamali vitambulisho rasmi vya kufanya biashara POPOTE'!

Ukweli hapa bni kwamba hujabuni ajira wala VYANZO VYA AJIRA endelevu kwa misingi ya tamko la UN kuhusu ajira.

Rais SSH alipokiwa Mwanza alisema anajua kwamba baadhi ya machinga huwauzia wafanyabiashara wakubwa mbele ya maduka yao, akawaonya kwamba wanaziba njia za waenda kwa miguu na kuleta msongamano barabarani!

Zoezi hili linaonyesha kwamba siri ya wajasiriamali hawa ni wafanyabiashara wenye MITAJI MIKUBWA wanaowapa "AJIRA" baadhi ya wamachinga (kwa mlago wa nyuma) na kufanya watawala kudai kwamba wamezalisha ajira!

Kwa fikra za kawaida serikali ingeboresha mazingira ya wafanyabiashara wenye MITAJI MIKUBWA ili wawape ajira hao wanaopanga bidhaa barabarani nayo serikali ipate kodi zaidi. Badala yake sera za CCM zinawaumiza wafanyabiashara wakubwa wanaolipakodi kwa EFD kwasababu hawaupendi mfumo wenyewe, na wengine humfanya mbinu za kuuhujumu. Halafu pia serikali haipati kodi inayostahili toka kwa machinga hata kama baadhi yao wana mitaji mikubwa. Ilimradi wamepata vitambulisho rasmi na kuvivaa shingoni. Hawagusiki!

Huko Morogoro DC na Mkurugenzi wa Jiji wamefutwa kazi kwa suala la machinga; tena kupitia tamko la hadharani kule Mwanza! Mimi bado sijaelewa kama Rais SSH alishauriwa na waziri yupi katika serikali yake?

Kwasababu suala la kubuni au kuhamisha maeneo ya biashara za machinga ni la mamlaka za miji na wizara mtambuka. Lakini uamuzi wake ulifanywa papo kwa papo siku chache tu baada ya vurugu kati ya Mgambo na machinga huko Morogoro! Ni mfano nzuri wa 'arbitrary decision' uamuzi wa holela.

Tumefika mahali hata bungeni Mbunge wa CCM anasema kwamfano kwamba: Mtukufu Rais ameamua katika bajeti ya mwaka huu "kuongeza kodi ya vifurushi vya simu" au"kuwapandisha vyeo na mishahara walimu". Yaani mbunge anasahau kwamba yuko bungeni kusemea wananchi na kuiwahibisha serikali katika kutumikia wananchi wote kwa usawa. Na kwamba mapato na matumizi ya Serikali (budget) yanaidhinishwa na bunge.

Nimalizie kwa kusema kwamba sera ya CCM ya ELIMU ni kuwezesha kijana kujiajiri, si kuajiriwa. Hapo hapo sera ya CCM ya UCHUMI ni kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda.

Swali gumu ni kwamba ni nani watakaoajiriwa kwenye viwanda hivyo? Ajira katika dunia ya sasa na baadae inahitaji elimu ya kimataifa pamoja na lugha, katika nyanja mbalimbali za uchumi. Hii sera ya elimu ya kujiajiri ni potofu, inakinzana na lengo la kupeleka nchi kwenye UCHUMI WA JUU.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
Active and success societies,depend on up and running governments systems,Democratic elections and cultural behavior of the people'Unyumbu'Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of fear or panic (amydgala) hayo yako kwenye kitabu changu cha ujasiriamali kwenye somo linaloitwa mjasiriamali na jamii iliyo nyamaza
 
Tatizo wao na wanaojiita bodaboda wanataka serekali iwachukulie kama disabled group au kundi linalohitaji uangalizi zaidi kama wazee , wanawake na watoto ( vulnerable group) na hivyo kuona ni hakiwao kuweka biashara popote hata kama uwezo wa kupanga frem wanao na serikali au jamii ikiwaambia wafuate utaratibu wanaanza vurugu au kuilazimisha serikli iwatfutie aehemu kana kwamba serikali inamtafutia kazi kila mwananchi
 
Back
Top Bottom